Zanzibar: Bandari Yazorotesha Uwekezaji Mangapwani

Zanzibar: Bandari Yazorotesha Uwekezaji Mangapwani

Mangapwani Port Zanzibar

Wawekezaji wa makampuni ya Gesi wamelilalamikia Shirika la Bandari Zanzibar kwa Urasimu usiokuwa na ulazima katika juu ya eneo la Bandari la Uwekezaji Mangapwani.

Mnamo Novemba 2021 serikali ya Zanzibar ilieleza azma yake ya kufanikiwa katika mradi mkubwa wa maendeleo katika Bandari ya Uwekezaji ya Mangwani.

Chini ya mradi huu unaojumuisha wote wa Mangapwani, Zanzibar ilikuwa ni kujenga bandari kubwa ya kisasa yenye vituo kadhaa vya kontena na vya jumla vya mizigo, vikiwemo mafuta, meli za uvuvi, mafuta na gesi asilia.

Mwaka mmoja baadae…

Habari kutoka vyanzo mbalimbali ndani ya Serikali, Wawekezaji na wadau wengine wa matumizi ya gesi wanasema kuwa Shirika la Bandari linachelewesha kwa makusudi mchakato wa utoaji vitalu.

Ofisa mmoja kutoka Kampuni ya Puma alisema kwamba ni zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu walipowasilisha maombi ya kutaka kupatiwa eneo kwa ajili ya kuweka gesi na Mafuta katika Eneo la Mangapwani,lakini kila wanapofuatilia Shirika la Bandari ndilo linaloonekana kutokuwa tayari.

” Sisi tumeomba eneo la Mangapwani kuweka kituo chetu, pamoja na kukamilisha taratibu zote,lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea” Alisema Ofisa Mmoja wa Kampuni ya Puma.

Watendaji wengine wa Makapuni ya uuzaji gesi na Mafuta ambao hawakupenda kutaja majina yao, wamesema wanashangazwa na Watendaji wa Shirika la Bandari kuwazungusha kila siku.

Habari zaidi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Maji na Nishati Zanzibar( ZURA) zinasema kuwa kwa upande wao wamekamilisha yale yanayowahusu na kilichobakia ni kwa Shirika la Bandari kutoa ruhusa kwa makampuni yaliyoomba kuweza kuwekeza sekta ya gesi na nishati.

“Hatuelewi kwanini kumekuwa na urasimu katika jambo hili, kila walichotwambia tumewapelekea” Alisema Ofisa Mwandamizi katika Kampuni ya Gesi ya ORXY.

Awali, suala la uwekezaji katika eneo la Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja lilikuwa likiratibiwa na ZURA ,lakini lilihamishwa na kupelekwa Shirika la Bandari ambalo halina ujuzi na utaalamu katika masuala ya nishati na gesi.

Kwa mujibu wa mpango wa Serikali, eneo la Mangapwani limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Bandari na Mji wa Kisasa.

Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar, Nahaat Mahfoudh hazikuweza kufanikiwa.

Angalia pia

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories