Wizara ya Kazi, Uwekezaji kuzalisha ajira 18,500 Zanzibar

Wizara ya Kazi, Uwekezaji kuzalisha ajira 18,500 Zanzibar

Unguja. Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji imeainisha vipaumbele vyake ikiwemo kuratibu upatikanaji wa ajira za staha 3,500 nje ya nchi na ajira rasmi 15,000 za ndani.

Pia, itaimarisha usalama na afya kazini kwa ununuzi wa vifaa vya uchunguzi, kufanya ukaguzi kazi katika maeneo 600 ya kazi (Unguja 500 na Pemba 100) na kuimarisha majadiliano na kutatua migogoro 162 ya kazi.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 23, 2024 na Waziri wa wizara hiyo, Shariff Ali Shariff wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kwenye mkutano wa 15 wa Baraza la Wawakilishi.

Waziri Shariff ameomba Baraza hilo liidhinishe  Sh75.2 bilioni.

Kipaumbele kingine ni uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kufanya mageuzi ya vyama vya ushirika na kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali 26,000 kwa kuongeza programu za uwezeshaji.

Pia inalenga kulea na kukuza wajasiriamali kwa kujenga kituo kimoja, kutoa mafunzo kwa wajasiriamali 8,612 na kuwaunganisha na masoko wajasiriamali 450.

“Kipaumbele kingine ni kukuza na kuimarisha uwekezaji kwa kuweka mikakati ya kutangaza fursa na kusajili miradi 110ya uwekezaji, miradi ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) pamoja na kuimarisha miundombinu ya ujenzi wa barabara za ndani katika zoni B, eneo la Micheweni,” amesema

Vilevile, amesema Serikali inalenga kufanya mageuzi ya ofisi yake kwa kuimarisha mazingira ya kazi, nyenzo, kukuza ujuzi wa wafanyakazi, kuweka mazingira wezeshi ya kazi, kuongeza masilahi ya wafanyakazi na kutumia mifumo ya kidijitali.

Amesema katika kipindi cha miezi tisa ya mwaka wa fedha wa 2023/24, imesajili miradi 63 ya uwekezaji yenye thamani ya Dola za Marekani 1,499 millioni inayotarajia kutoa ajira 4,392.

Amesema mtaji wa miradi ya uwekezaji umekuwa kwa asilimia 209.8 kutoka Dola za Marekani 714.7 milioni (Sh1.8 bilioni) mwaka 2022/23 hadi Dola za Marekani 1.4 bilioni (Sh3.6 trilioni) mwaka 2023/24.

Vile vile amesema, ofisi yake imeimarisha huduma jumuishi za uwekezaji, kuweka mfumo wa kieletroniki unaorahisisha utoaji wa huduma, kuweka ardhi ya akiba kwa uwekezaji, kuimarisha miundombinu ya uwekezaji katika maeneo huru ya uwekezaji ikiwemo Fumba, Micheweni na Dunga.

Akizungumzia kuhusu miradi ya mashirikiano baina ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP) kwa mwaka wa fedha 2023/2024, amesema jumla ya miradi 17 imepokewa, kati ya hiyo, mitano imefanyiwa uchambuzi na kuonekana kukidhi vigezo kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi. 

Akizungumzia baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, amesema wameongeza makusanyo kutoka Sh2.7 bilioni mwaka 2022/2023 hadi Sh3.9 bilioni mwaka 2023/24 sawa na asilimia 145 ya makadirio.

Katika kipindi hicho amesema wizara imefanya ukaguzi kazi katika maeneo ya kazi 216 (Unguja 141 na Pemba 75) ili kuhakikisha utekelezwaji wa sheria za kazi katika kulinda haki na masilahi ya wafanyakazi. 

Pia amesema, ofisi yake imethibitisha mikataba ya kazi ya wafanyakazi wazawa 9,624 kati yao Unguja walikuwa 8,739 na Pemba 885, sawa na asilimia 192 ukilinganisha na lengo ya mikataba 5,000 ya mwaka wa 2023/24.

Changamoto zilizopo

Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo, amesema ni uhaba wa mitaji kwa ajili ya utoaji wa mikopo ya wajasiriamali kulingana na maombi yaliyopo, yenye thamani ya Sh95 bilioni kwa wajasiriamali 1,884 (vikundi 1,410 na wawekezaji wa ndani 474) walioomba. 

Wakichangia hotuba hiyo baadhi ya wawakilishi, Shadya Mohamed Suleiman (makundi maalumu) amesema sheria ya ajira imekuwa ya muda mrefu na inawakwaza vijana wengi, hivyo wizara iangalie namna ya kuifanyia marekebisho.

Mwakilishi wa Mwera, Mihayo Juma Nhunga amesema ipo haja ya kusimamia wanaochukua  mikopo wairejeshe ili kutatua changamoto ya ajira na kuwawezesha watu wengine kuchukua fedha hizo.

Kwa upande wake Mwakilishi Dimani, Mwanaasha Khamis Juma ameshauri Serikali iendelee kuwavutia wawekezaji wenye hadhi ili kukuza uchumi wa kisiwa hicho.

Mwakilishi wa makundi maalumu, Fatma Ramadhan Mohamed amesema ufike wawekezaji waje na vyanzo vya umeme kwani suala la umeme limeshakuwa tete, licha ya Serikali kuanzisha vyanzo vyake.

“Kwa hiyo wawekezaji waweke miundombinu yao kama wanavyofanya Tanzania bara wanakuja na vyanzo vyao, hii itasaidia umeme wetu ambao bado haujawa mzuri,” alisema.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania Confirms Outbreak of Marburg Virus Disease
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania Confirms Outbreak of Marburg Virus Disease

Dodoma — Tanzania today confirmed an outbreak of Marburg virus disease in the northwestern Kagera region after one case tested positive for the virus following investigations and laboratory analysis of suspected cases of the disease.

President of the Republic of Tanzania, Her Excellency Samia Suluhu Hassan, made the announcement during a press briefing alongside World Health Organization (WHO) Director-General, Dr Tedros Adhanom Ghebreyesus, in the country’s administrative capital Dodoma.

“Laboratory tests conducted in Kabaile Mobile Laboratory in Kagera and later confirmed in Dar es Salaam identified one patient as being infected with the Marburg virus. Fortunately, the remaining suspected patients tested negative,” the president said. “We have demonstrated in the past our ability to contain a similar outbreak and are determined to do the same this time around.”

A total of 25 suspected cases have been reported as of 20 January 2025, all of whom have tested negative and are currently under close follow-up, the president said. The cases have been reported in Biharamulo and Muleba districts in Kagera.

“We have resolved to reassure the general public in Tanzania and the international community as a whole of our collective determination to address the global health challenges, including the Marburg virus disease,” said H.E President Hassan.

WHO is supporting Tanzanian health authorities to enhance key outbreak control measures including disease surveillance, testing, treatment, infection prevention and control, case management, as well as increasing public awareness among communities to prevent further spread of the virus.

“WHO, working with its partners, is committed to supporting the government of Tanzania to bring the outbreak under control as soon as possible, and to build a healthier, safer, fairer future for all the people of Tanzania,” said Dr Tedros. “Now is a time for collaboration, and commitment, to protecting the health of all people in Tanzania, and the region, from the risks posed by this disease.”

Marburg virus disease is highly virulent and causes haemorrhagic fever. It belongs to the same family as the virus that causes Ebola virus disease. Illness caused by Marburg virus begins abruptly. Patients present with high fever, severe headache and severe malaise. They may develop severe haemorrhagic symptoms within seven days.

“The declaration by the president and the measures being taken by the government are crucial in addressing the threat of this disease at the local and national levels as well as preventing potential cross-border spread,” said Dr Matshidiso Moeti, WHO Regional Director for Africa. “Our priority is to support the government to rapidly scale up measures to effectively respond to this outbreak and safeguard the health of the population,”

Tanzania previously reported an outbreak of Marburg in March 2023 – the country’s first – in Kagera region, in which a total of nine cases (eight confirmed and one probable) and six deaths were reported, with a case fatality ratio of 67%.

In the African region, previous outbreaks and sporadic cases have been reported in Angola, the Democratic Republic of the Congo, Ghana, Kenya, Equatorial Guinea, Rwanda, South Africa and Uganda.

Marburg virus is transmitted to people from fruit bats and spreads among humans through direct contact with the bodily fluids of infected people, surfaces and materials. Although several promising candidate medical countermeasures are currently undergoing clinical trials, there is no licensed treatment or vaccine for effective management or prevention of Marburg virus disease. However, early access to treatment and supportive care – rehydration with oral or intravenous fluids – and treatment of specific symptoms, improve survival.

Source: allafrica.com

Continue Reading

ZAA to audit ground handlers
Popular
Investment News Editor

Zanzibar Airport Authority to audit ground handlers

Unguja. The Zanzibar Airports Authority (ZAA) is set to conduct an audit on ground handling companies that currently operate at the Abeid Amani Karume Airport with effect from Monday. The week-long audit is set to include Transworld, ZAT and the newcomer Dnata Zanzibar who were licensed in June plus exclusive rights to manage Terminal 3 building by ZAA.Continue Reading