Wenye fani, sifa hizi ajira nje nje Polisi

Wenye fani, sifa hizi ajira nje nje Polisi

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limetangaza nafasi mbalimbali za ajira kwa vijana wenye elimu ya shahada, astashahada, kidato cha sita na nne, huku moja ya sifa kwa muombaji lazima awe raia wa Tanzania wa kuzaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi makao makuu Dodoma Mei 9,2024,  imeeleza miongoni mwa nafasi  hizo kwa upande wa shahada ni 74, diploma 66, na upande wa ngazi ya cheti (astashahada  ni 66).

Fani zinazotakiwa kwa kila ngazi ya elimu ni pamoja na uuguzi, famasia, wahandisi wa vyombo vya majini, kompyuta, muziki, wapima ardhi, usimamizi wa michezo na utawala.

“Waombaji wanatakiwa waandike barua kwa mkono na wasisahau namba za simu na wanapaswa kutumia anuani ya Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 Dodoma.

“Waombaji wote wafanye maombi kupitia kwenye mfumo wa ajira wa Polisi (Tanzania Police Force -Recruitment Portal) unaopatikana kwenye tovuti ya jeshi hilo ya; www Polisi.go.tz na mwisho wa kupokea maombi hayo ni Juni 16, 2024,” imesema taarifa hiyo

sifa za waombaji

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sifa nyingine muombaji awe  amehitimu wa kidato cha nne na sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.

“Kwa waombaji waliohitimu kidato cha nne, sita na wenye stashahada wawe na umri wa kuanzia miaka 18 hadi 25 .Wale wa  kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la nne  wawe na ufaulu wa alama 26 hadi 28,” imesema taarifa hiyo.

Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu.Wahitimu wa shahada au stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.

Pia waombaji wawe na urefu usiopungua futi tano na nchi nane (5″8″) kwa wanaume na futi tano nchi nne (5″4″) kwa wanawake, waanapaswa kuwa na utambulisho kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),awe na uwezo wa kuongea kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza,” imesema

“Anapaswa kuwa na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali na awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.

Wenye tattoo hawahusiki

“Asiwe na alama za kuchorwa mwili (tatoo), asiwe na kumbukumbu ya uhalifu na kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha shahada (NTA levo 8) Shahada (NTA levo 6) na astashahada level (NTA  levo 5 au NVA level 3) wanatakiwa wawe na fani zilizoanishwa kwenye tangazo hilo.,” limesema  tangazo

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Top News
Investment News Editor

ZSSF money not for projects, says Ali Karume

Unguja. Veteran politician and diplomat Ali Karume has called on authorities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) to refrain from using the Zanzibar Social Security Fund money for establishing commercial projects.Continue Reading