Wenye betri ya moyo ushauri hii inawafaa

Wenye betri ya moyo ushauri hii inawafaa

Wenye betri ya moyo ushauri hii inawafaa

Dar es Salaam. Kama una shida ya moyo na umepandikizwa betri ya moyo,  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshauri matumizi ya simu yasiwe karibu na eneo lenye kifaa hicho kuepusha mawasiliano baina ya vifaa hivyo.

Kitaalamu, betri ya moyo (Pacemaker) ni kifaa maalumu kinachosaidia kurekebisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida, kifaa hiki hufanya kazi kama jenereta, kikirejesha mfumo wa umeme wa moyo ili kuhakikisha unafanya kazi kwa mpangilio sahihi.

Ushauri huo wa TCRA wa kuepuka matumizi ya simu karibu na eneo lenye kifaa hicho ni kufuatilia swali la mwandishi wa habari juu ya nadharia zinazoelezwa kwenye jamii kuwa matumizi ya simu karibu na kifua husababisha matatizo ya moyo.

“Kama utakuwa na suala la kiafya peacemaker si vizuri simu au kifaa cha mawasiliano kukaa karibu  na ile kwa sababu nayo inawasiliana, kama ambavyo tunavyosema masafa hii na hii inawasiliana vikiingiliana vinaweza kuleta shida,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabiri Bakari.

Dk Bakari ametoa ushauri huo leo Machi 28, 2025 wakati akizungumza na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotembelea mradi wa maabara ya uidhinishaji wa vifaa vya mawasiliano vya kielektroniki.

Wakati Dk Bakari akitoa ushauri huo kwa wagonjwa wa moyo wenye betri, takwimu za  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zinaonyesha Watanzania takriban 25 wanapandikizwa betri ya moyo kila mwezi, sawa na watu 300 kwa mwaka. Hili ni ongezeko kutoka watu 150 waliopandikizwa betri hiyo mwaka 2015/16,

Akizungumza  kuhusu usalama wa vifaa vya mawasiliano nchini Dk Bakari amesema kutokana na uwepo wa maabara hiyo vifaa feki vya mawasiliano havitafanya kazi nchini.

“Vifaa feki vitakuwa vimepungua sana, lakini ukikiwasha kifaa cha namna hiyo hapa (Tanzania) kinazima, kifaa hicho hatukusomi kama kimepita kwenye maabara yetu pia hakijazingatia viwango vya kimataifa hivyo hakiwezi kufanya kazi unaweza kuwasha simu ikazimika hapohapo,” amesema.

Dk Bakari amesema vifaa vyote vya mawasiliano vinavyotarajiwa kuingizwa nchini kwa ajili ya matumizi lazima wahakiki ubora wake lazima mzalishaji awasilishe sampuli ndani ya mamlaka hiyo kwa ajili ya kuangaliwa ubora.

“Kwanza kuangalia hakitakuwa hatarishi kwa mtumishi, jambo la pili tunahakikisha kifaa kinacholetwa nchini kina viwango na vinafanya kazi kulingana na masafa yaliyotengenezwa kwa ajili hiyo na isiingilie masafa mengine,” amesema.

Pia, amesema mamlaka hiyo inatarajia kuongeza mitambo ya kupima namna vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki vinavyoweza kujikinga au kusababisha mwingiliano wa sumaku -umeme na vifaa vingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa PAC Nagenjwa Kaboyoka amesema ujenzi wa maabara hiyo umeniweka Tanzania katika hatua ya kimataifa.

“Watu wamekuwa na wasiwasi kwamba simu wanazotumia hazina ubora ‘feki’ lakini wataalamu wametuhakikisha simu wanazotumia wananchi haziwezi kuwadhuru,

“Maabara hii ni ya kimataifa na nchi zingine zinakuja kujifunza kuona namna ambavyo mitambo ya kielektroniki haiwezi kuingizwa nchini, pia yapo mitambo mbalimbali iliyopo hapa ni rahisi mtu mwenye mtambo wake ambao haukubaliki kukamatwa,” ameeleza.

Kutokana na uwepo wa maabara hiyo, Nagenjwa amesema Tanzania haina hofu ya kuingizwa vifaa feki’ nchini akisisitiza TCRA ijikite kujitangaza ili mataifa mengine yahamasike kufika nchini kutumia maabara hiyo.

Mbali na Tanzania mataifa mengine yenye maabara hiyo ni Tunisia, Afrika Kusini, Ghana, Nigeria, Cameroon, Benin, Guinea, Togo, Senegal, Mali na Mauritania.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’
Top News
Chief Editor

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Monrovia — The Rwanda Minister of State responsible for Health, Dr. Yvan Butera, cautioned that while the country is beginning to see positive signals in its fight against the Marburg virus, the outbreak is “not yet over”. He, however, expressed hope that  “we are headed in that direction”. The minister said the epidemiology trend, since the disease was first discovered in the country more than a month ago, is moving towards fewer cases.

Dr. Butera, who was giving updates during an online briefing yesterday, said in the past two weeks, only two deaths were recorded while 14 people recovered from the disease. He said Rwanda was expanding its testing capacity with 16,000 people already inoculated against the disease.

The priority right now, Butera said, is “rapid testing and detection”.

Marburg is a highly virulent disease transmitted through human-to-human contact or contact with an infected animal. The fatality rate of cases, which has varied over the period, is more than 50%, according to the World Health Organization.  WHO said the highest number of new confirmed cases in Rwanda were reported in the first two weeks of the outbreak. There’s been a “sharp decline” in the last few weeks, with the country now tackling over 60 cases.

At Thursday’s briefing, a senior official of the Africa Centers for Disease Control, Dr. Ngashi Ngongo, said mpox – the other infectious disease outbreak that countries in the region are fighting – was been reported in 19 countries, with Mauritius being the latest country to confirm a case. He said although no new cases have been recorded in recent weeks in several countries where outbreaks occurred previously –  including Cameroon, South Africa, Guinea, and Gabon – Uganda confirmed its first Mpox death. This, he said, is one of two fatalities reported outside Central Africa.

Dr. Ngashi revealed that there was an increase in cases in Liberia and Uganda. He said mpox cases were still on an upward trend.

“The situation is not yet under control.”

Source: allafrica.com

Continue Reading

Popular
Swahili News Editor

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading