Wawili waenda jela maisha kwa kusafirisha mirungi 

Wawili waenda jela maisha kwa kusafirisha mirungi 

Moshi. Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na   Uhujumu Uchumi Kanda ya Moshi, imewahukumu kifungo cha maisha jela, Abdalah Halfan Mkwizu na Samwel Eliud Lyakurya wakazi wa Rombo, baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha kilo 690.767 za dawa za kulevya aina ya mirungi.

Mbali na kifungo hicho, Mahakama hiyo imeamuru kutaifishwa kwa gari aina ya Toyota Mark 11 lililotumika kusafirisha dawa hizo kuwa mali ya Serikali.

Hukumu ya kesi ilitolewa Mei 29, 2023 na Jaji, Jaji Elineza Luvanda. 

Katika hukumu huyo, Jaji Luvanda amesema Mahakama hiyo imejiridhisha pasipo shaka kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 (1) (A) cha Sheria ya Upambanaji na Udhibiti wa dawa za kulevya namba 15 ya mwaka 2015, kama ilivyofanyiwa marekebisho ya kifungu cha 8 cha sheria ya Udhibiti na Upambanaji wa dawa za kulevya sheria namba 15 ya mwaka 2017.

Akirejea mwenendo wa shauri hilo, jaji amesema Desemba 6, mwaka 2017 watuhumiwa hao wakiwa katika eneo la Marangu Kitowo, Wilaya ya Rombo walikutwa wakisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari aina ya Toyota Mark 11 . 

“Washtakiwa walikuwa wakisukuma gari  lililokuwa limekwama kwenye matope kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha, Washtakiwa hao waliomba msaada kwa aliyekuwa diwani wa eneo hilo, Dionis Happymark Shirima na hapo ndipo askari waliokuwepo doria walifika kwenye gari hilo na kubaini lilikuwa na dawa hizo za kulevya.”

Baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mbili, Jaji amesema Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo na hivyo walitiwa hatiani kwa kuhusika na usafirishaji wa dawa kulevya.

“Kwa mshtakiwa wa kwanza na wa pili wametiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya kinyume na sheria na hivyo kuhukumiwa adhabu hiyo.

“Mahakama hii imejiridhisha pasipo shaka kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo na mshtakiwa wa kwanza na wa pili wanahukumiwa kifungo cha maisha jela, pia  Mahakama imeamuru gari aina ya Toyota Mark 11 lenye namba za usajili T656 BYA ambalo lilitumika kusafirisha dawa hizo linataifaishwa na kuwa mali ya Serikali,”

Upande wa Jamhuri uliongozwa na mawakili wa Serikali Marietha Maguta na Bora Mfinanga na washtakiwa wakitetewa na Denis Maro na Rashid Shaban.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Zanzibar Commerce
Top News
Investment News Editor

Zanzibar Airports Authority enforces Dnata monopoly

. Airlines that have not joined the Zanzibar Airports Authority’s (ZAA) preferred ground handler, Dnata, at the Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA) face eviction from the Terminal Three building Dnata is the sole ground handler authorised to provide services for flights that operate at Terminal 3.Continue Reading

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

Monrovia — The Director General of the African Centers for Disease Control, Jean Kaseya, has said the center stands ready to support Tanzania and other countries in the region where suspected cases of the infectious Marburg Virus Disease have been identified. The World Health Organization earlier this week issued an alert warning of a possible outbreak in the country, although the Tanzanian Health Ministry has said tests conducted on available samples did not show the existence of Marburg in the East African nation.

“As of the 15 of January 2025, laboratory results from all suspected individuals were negative for Marburg Virus,” Tanzanian Health Minister Jenista Mhagama said in a statement. This would have marked the country’s second experience with the highly infectious disease that recently killed over a dozen people in neighboring Rwanda. Tanzania previously reported an outbreak of Marburg in 2023 in the  Kegara region, said to have been the epicenter of the new suspected cases.

At the Africa CDC online briefing on Thursday, Kaseya also said another infectious disease, Mpox, “remains a public health concern”. He said that while in December 2024, the disease had afflicted 20 countries, a new country – Sierra Leone – has been added to the number after recent outbreak there. Sierra Leonean health authorities said on January 10 that two cases of Mpox had been confirmed in the country and dozens of contacts are being traced.

With thousands of confirmed cases of Mpox across Africa and more than 1000 people having died of the disease  – mainly in Central Africa – Kaseya emphasized the need to increase testing, a theme he’s heralded before. The Africa CDC boss said over the next few months the continental health watchdog will deploy additional epidemiologists and community health workers to areas considered hot spots of infectious diseases in the region.

Source: allafrica.com

Continue Reading