‘Watoto wapewe fursa kutoa maoni Tanzania waitakayo’

‘Watoto wapewe fursa kutoa maoni Tanzania waitakayo’

Dar es Salaam. Katika mchakato wa utoaji wa maoni ya maendeleo ya nchi, watoto zaidi ya 14,000 wamepata fursa ya kuchangia maoni yao katika Dira ya Taifa ya Maendeleo yam waka 2050. 

Akizungumza jana Septemba 13, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi maoni ya watoto, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) Tanzania, Elke Wisch amesema watoto hao wamewasilisha ndoto na matarajio ya mamilioni ya watoto wa Tanzania.

“Wadau wote wana jukumu la kusikiliza mawazo waliyonayo kuhusu Tanzania waitakayo,” amesema.

Akieleza mchakato wa kukusanya maoni hayo, Wisch amesema mwaka huu Serikali ya Tanzania ilianzisha mchakato wa uwazi na jumuishi kwa Watanzania wa makundi mbalimbali kutoa maoni na maono yao juu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

“Kufuatia mchakato huo, Unicef, kwa kushirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Tume ya Mipango ya Taifa, ilifanya ukusanyaji wa maoni ya watoto nchini.

“Zaidi ya watoto 400 wenye umri wa kati ya miaka saba na 17 kutoka mikoa ya Kigoma, Mwanza, Dar es Salaam na Unguja walishiriki katika mikutano hiyo. Pia watoto wengine 14,000 kutoka pande mbalimbali za Tanzania walitoa maoni yao kupitia jukwaa la kidijitali la U-Report,” amesema.

Akiwasilisha maoni hayo Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Tanzania (JCURT), Raphael Charles, amesema watoto wametaja maeneo muhimu ya kuzingatia kuifikia Tanzania wanayoitaka.

Maeneo hayo ni pamoja na upatikanaji wa elimu bora, huduma bora za afya, kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi, kukomesha ukatili kwa watoto na kuendelea kuwashirikisha watoto katika majukwaa mbalimbali ya maamuzi.

Akipokea maoni hayo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dk Mursali Milanzi amesema watoto ni wadau muhimu katika utengenezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo, kwa sababu ifikapo mwaka 2050 watoto hawa watakuwa na umri wa miaka 32 hadi 42.

“Muda huo ukifika tunatarajia wengi wao watakuwa katika nafasi za kufanya uamuzi, jambo ambalo linaonyesha umuhimu wa kusikia sauti zao leo kuhusu Tanzania wanayoiona kwa siku zijazo,” amesema Dk Mursali.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk  Dorothy Gwajima, amesema:

“Mustakabali wa nchi hii ni wa watoto na kuwashirikisha katika mchakato wa mipango ya maendeleo ni jambo la muhimu sana.’’

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal

Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.

The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading