Watafiti Russia waleta ujuzi wa misitu nchini

Watafiti Russia waleta ujuzi wa misitu nchini

Watafiti Russia waleta ujuzi wa misitu nchini

Morogoro. Wataalamu wa misitu kutoka Russia wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (Tafori), ambapo wamejadiliana mambo mbalimbali ya kuitafiti yatayosaidia kuifanya sekta ya misitu nchini kuwa bora zaidi.

Katika mazungumzo hayo yaliyowahusisha pia maofisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wakiongozwa na kamishna wa uhifadhi, Profesa Dos Santos Silayo, watalaamu hao waliobobea katika masuala ya utafiti wa kisayansi wa misitu walijikita kuimarisha uhusiano wa kisayansi, kielimu na kiteknolojia kati ya Tanzania na Russia kwenye sekta ya misitu na uhifadhi wa mazingira.

Katika ziara ya wataalamu hao walioongozwa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ufundi wa Misitu cha Jimbo la Saint Petersburg, Chuo Kikuu cha Petrozavodsk na Chuo Kikuu cha Misitu na Teknolojia cha Jimbo la Voronezh walijadili maeneo ya utafiti wa pamoja, ambapo Tafori iliwasilisha tafiti muhimu ikibainisha fursa za kushirikiana katika nyanja za ikolojia, usimamizi wa misitu na teknolojia za uhifadhi wa mazingira.

Akizungumzia ushirikiano huo, Profesa Silayo amesema wanalenga katika kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya misitu ikiwamo mabadiliko ya tabianchi, magonjwa ya mimea na matumizi ya teknolojia za kisasa kwa kutumia setilaiti na ndege zisizo na rubani (drones) katika usimamizi wa misitu.

“Ushirikiano huu unaleta pamoja wataalamu wa Tanzania na Russia na tutafaidika kupitia kubadilishana maarifa na uzoefu wa kisayansi,” amesema Profesa Silayo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tafori, Dk Revocatus Mushumbusi amesema watashirikiana katika utafiti wa misitu, hasa katika kukabiliana na changamoto za moto wa msitu na kuendeleza mbinu za kisasa za utafiti.

“Ushirikiano huu utatufundisha mbinu mpya na teknolojia zinazotumika Urusi, ambazo zinaweza kusaidia kuboresha uhifadhi wetu wa misitu,” amesema Dk Mushumbusi.

Katika majadiliano hayo, watafiti kutoka Russia walizungumzia mafanikio waliyoyapa kwenye matumizi ya teknolojia za kisasa za utafiti wa misitu kwa kutumia setilaiti na ndege zisizo na rubani kutathmini hali ya misitu kwa ufanisi.

Vilevile waligusia umuhimu wa utafiti wa pamoja katika maeneo ya uzalishaji wa miti bora, entomolojia na usimamizi wa misitu kwa kutumia teknolojia ya akili mnemba (AI).

Mtafiti Mkuu wa Tafori, Dk Chelestino Peter Balama amesema wamefanikiwa katika eneo la uhifadhi wa mazingira na kulinda mimea inayo hatarini kutoweka.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories