Wananchi Paje wataka ushirikishwaji ujenzi uwanja wa ndege

Wananchi Paje wataka ushirikishwaji ujenzi uwanja wa ndege

Unguja. Wananchi zaidi ya 400 katika Kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja, wameingiwa wasiwasi kuhusu kuhamishwa eneo hilo,  kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege wakidai hawajashirikishwa.

Wasiwasi huo unatokana na kuwapo mpango wa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kutaka kujenga uwanja wa ndege katika eneo hilo.

Wamesema wamekuwa wakiona wataalamu wanaenda kupima maeneo yao lakini hawana taarifa yoyote wala kushirikishwa.

Mkazi wa eneo hilo, Haji Nuru Said amesema wao hawapingani na mipango ya Serikali, lakini wanachotaka ni ushirikishwaji ili watambue iwapo wakihamishwa wapi wanakwenda au vinginevyo.

“Kuna utata unaojitokeza watu wanakuja kupima kwenye maeneo yetu lakini hatuna taarifa na hatushirikishwi, tunaomba mchakato wote tushirikishwe na kujua kinachoendela,” amesema. 

Kauli hiyo imeungwa mkono na Abubakar Mtumwa anayesema: “Sisi hatupingi maendeleo lakini tunasikia huko tu hatushirikishwi kwenye hatua zote ili kuridhia au kama tutatakiwa kuondoka tujue ni wapi tunakwenda na katika misingi gani.”

Hata hivyo, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk Khalid Salum Mohamed  amewataka wananchi hao walio karibu na eneo hilo linalotarajiwa kujengwa uwanja wa ndege,  kuondoa wasiwasi kwani Serikali haiwezi kufanya uamuzi bila kuwashirikisha wananchi wa eneo husika.

Dk Khalid amesema bado mchakato huo upo kwenye hatua za awali, kwa hiyo iwapo kukiwa na uamuzi wa kujenga uwanja huo, lazima wananchi watashirikishwa na ikiwezekana hata watakaotakiwa kupisha watalipwa fidia.

“Serikali haiwezi kufanya jambo bila kuwashirikisha na hakuna mwananchi atakayeondolewa kwenye eneo lake. Kinachofanyika kwa sasa bado ni upembuzi yakinifu iwapo uamuzi ukifikiwa kila kitu kitakuwa sawa,” amesema Dk Khalid.

Kwa sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ina mipango ya kujenga viwanja vya ndege katika maeneo ya utalii ili kurahisisha ufikaji.

Miongoni mwa maeneo hayo ni Paje Mkoa wa Kusini Unguja na Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

EXIM Bank to raise 300m/- over the next three years for financing essential services and infrastructure upgrades in mental health facilities.

The bank’s Head of Marketing and Communications Stanley Kafu unveiled this when introducing Exim Bima Festival 2024 as a platform for bringing together individuals, organisations and various sectors for raising the funds.

“Exim’s initiative aligns with the government’s broader goals to ensure that every citizen has access to quality healthcare, including mental health services,” he said.

The initiative, which is one of the events for celebrating the bank’s 27th anniversary is scheduled for Wednesday this week in Dar es Salaam.

Mr Kafu highlights that this year’s festival is not only about raising awareness of the importance of insurance in the society but also focuses on enhancing access to mental health services and improving the overall well-being of the nation.

Statistics from the Ministry of Health shows a staggering 82 per cent increase in mental health cases over the past decade.

Mental cases have risen from 386,358 in 2012 to 2,102,726 in 2021, making the need for mental health services more urgent than ever.

ALSO READ: NBC’s Saving Campaign Empowers Customers Nationwide

Unfortunately, the country’s ability to address this growing challenge is hindered by a shortage of mental health professionals, infrastructure, medical equipment and essential medication.

For example, out of the 28 regions in the country, only five have facilities that provide adequate mental health services.

The most affected group is the youth aged 15 to 39, who represent the nation’s workforce, underscoring the need for intensified efforts to safeguard this generation for Tanzania’s future well-being and development.

Mr Kafu said by improving mental health services, Exim aims to contribute to the creation of a network of communities that can access care quickly and affordably.

Exim Insurance Department Manager Tike Mwakyoma said they are appreciating the support from partners in the insurance industry, who have stood by them since the last festival.

“Let’s continue this unity for the development of all Tanzanians and our nation as a whole,” the manager said.

Source: allafrica.com

Continue Reading