Waliomba kazi TRA, kufanyiwa usaili hapa

Waliomba kazi TRA, kufanyiwa usaili hapa

Dar es Salaam. Watu 112,952 wameitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika (Written Interview), baada ya kukidhi vigezo vya maombi ya ajira katika nafasi 1596 zilizotangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA).

Februari 6, 2025, TRA ilitangaza nafasi za ajira 1596  katika fani mbalimbali, ambapo watu 135,027 waliomba nafasi hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jioni, Machi 21, 2025, kuhusiana na mchakato wa kuwapata waombaji hao, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka TRA, Moshi Kabengwe,  amesema TRA ilipitia kwa umakini maombi ya kazi 135,027 na kupata maombi 112,952 ambao ndio wenye vigezo vya kuitwa kwenye usaili.

Amesema majina ya watu hao waliokidhi vigezo hivyo, yatatangazwa kesho Machi 22, 2025 katika tovuti ya Mamlaka hiyo ya mapato.

“TRA imepitia kwa umakini mkubwa maombi yote 135,027 yaliyopokelewa na kupata waomba kazi 112,952 ambao wamekidhi vigezo vilivyowekwa na hivyo wanastahili kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika( Written Interview) unaotarajia kufanyika Machi 29 na Machi 30, 2025 katika kanda tisa zilizoanishwa na TRA,” amesema Kabengwe na kuongeza.

“Mbali na majina kuwekwa kwenye tovuti ya TRA, pia taarifa itatumwa moja kwa moja kwa kila muombaji kupitia barua pepe yake aliyotumia wakati wa kuomba kazi, vilevile tarehe, mahali na muda wa usaili zimeonyeshwa kwenye wito huo” amefafanua.

Amesema mwitikio wa watu kuomba nafasi za kazi umekuwa mkubwa,  kwani TRA ilitangaza nafasi za kazi 1,596, lakini hadi Februari 19, 2025 walipokamilisha siku ya mwisho ya kupokea maombi walioomba walikuwa ni 135,027.

Kabengwe amebainisha kuwa usaili wa mchujo huo utafanyika katika mikoa tisa, ambapo Dar es Salaam itahusisha waombaji kutoka Dar es Salaam na Pwani.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) Moshi Kabengwe, akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) wakati akitangaza idadi ya watu walioitwa kwenye usaili wa mchujo wa awali, baada ya kukidhi vigezo vya maombi ya kazi yaliyotangazwa na Mamlaka hiyo. Picha na Hadija Jumanne

“Kituo cha usaili cha Zanzibar itahusisha waombaji kutoka Unguja na Pemba, wakati kituo cha usaili cha Dodoma itahusisha waombaji kutoka mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Iringa na Tabora” amesema.

Amesema kwa upande wa kaskazini, kituo cha usaili kutakuwa Arusha, ambapo kitahusisha waombaji kutoka mkoa wa Manyara, Kilimanjaro, Arusha yenyewe na Tanga.

Kwa upande wa mikoa ya Kusini, eneo la usajili litakuwa Mtwara ambapo itahusisha waombaji kutoka Lindi, Mtwara na Ruvuma.

“Pia Mwanza itakuwa ni kituo cha usaili kwa waombaji kutoka mikoa ya Shinyanga, Mara, Mwanza na Simiyu,” amesema.

Vilevile kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini, kituo cha usaili kitakuwa Mbeya ambapo kitahusisha waombaji kutoka Songwe, Mbeya na Rukwa.

Vilevile kituo cha usaili cha Kigoma, kitahusisha waombaji kutoka mkoa wa Katavi na Kigoma yenyewe wakati kwa kituo cha usaili cha Kagera kitahusisha waombaji kutoka Geita na Kagera yenyewe.

“Utaratibu maalum umeandaliwa kwa waombaji kazi wenye mahitaji maalum waliofanikiwa kuitwa kwenye usaili wa mchujo wa kuandika ili waweze kufanya usaili huo bila usumbufu” amesema.

Kabengwe alifafanua kuwa mchakato huo wa ajira utaendeshwa na Mshauri mtaalamu na Mamlaka itasimamia kwa karibu ili kuhakikisha haki inatendeka kwa waombaji wote.

“Waombaji watakao faulu kwenye usaili wa mchujo wa kuandika wataitwa kwenye usaili wa mahojiano kwa tarehe itakayopangwa” amesema.

Vilevile, ameitaka jamii pamoja na waombaji wa nafasi hizo za kazi kuepuka utapeli unaoweza kufanywa na watu ambao sio waaminifu na kwamba TRA itaweka namba maalumu kwa ajili ya mawasiliano baina ya waombaji ili kuepuka utapeli.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

EXIM Bank to raise 300m/- over the next three years for financing essential services and infrastructure upgrades in mental health facilities.

The bank’s Head of Marketing and Communications Stanley Kafu unveiled this when introducing Exim Bima Festival 2024 as a platform for bringing together individuals, organisations and various sectors for raising the funds.

“Exim’s initiative aligns with the government’s broader goals to ensure that every citizen has access to quality healthcare, including mental health services,” he said.

The initiative, which is one of the events for celebrating the bank’s 27th anniversary is scheduled for Wednesday this week in Dar es Salaam.

Mr Kafu highlights that this year’s festival is not only about raising awareness of the importance of insurance in the society but also focuses on enhancing access to mental health services and improving the overall well-being of the nation.

Statistics from the Ministry of Health shows a staggering 82 per cent increase in mental health cases over the past decade.

Mental cases have risen from 386,358 in 2012 to 2,102,726 in 2021, making the need for mental health services more urgent than ever.

ALSO READ: NBC’s Saving Campaign Empowers Customers Nationwide

Unfortunately, the country’s ability to address this growing challenge is hindered by a shortage of mental health professionals, infrastructure, medical equipment and essential medication.

For example, out of the 28 regions in the country, only five have facilities that provide adequate mental health services.

The most affected group is the youth aged 15 to 39, who represent the nation’s workforce, underscoring the need for intensified efforts to safeguard this generation for Tanzania’s future well-being and development.

Mr Kafu said by improving mental health services, Exim aims to contribute to the creation of a network of communities that can access care quickly and affordably.

Exim Insurance Department Manager Tike Mwakyoma said they are appreciating the support from partners in the insurance industry, who have stood by them since the last festival.

“Let’s continue this unity for the development of all Tanzanians and our nation as a whole,” the manager said.

Source: allafrica.com

Continue Reading

Popular
Chief Editor

Insecurity prompts Zanzibar to review its lucrative island leasing

The Tanzanian central government is planning to boost its security presence in the Zanzibar archipelago. A commission tasked with auditing the country’s security forces was appointed in July by President Samia Suluhu Hassan. It says it is concerned about the situation in the country’s Indian Ocean islands that are under the control of the semi-autonomous Zanzibar local government.Continue Reading