Wafahamu wachezaji wa Morocco wanaoweka historia Qatar

Wafahamu wachezaji wa Morocco wanaoweka historia Qatar

Qatar 2022 

Morocco wako hatua moja kutoka kwa nafasi nzuri katika fainali ya Kombe la Dunia, huku kocha wao Walid Regragui akikumbatia “kichaa” kabla ya mechi yao ya nusu fainali na mabingwa watetezi Ufaransa.

Mafanikio yao nchini Qatar na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufika hatua hii, yamewashangaza wengi hasa baada ya kocha aliyeiongoza Atlas Lions kwenye michuano hiyo kutimuliwa mwezi Agosti.

Inasemekana kuwa miongoni mwa timu zilizofanya vibaya katika soka la Afrika Kaskazini, ambapo taji lao pekee la bara lilifika 1976.Ushindi wa 2-0 wa Morocco dhidi ya Ubelgiji katika mchezo wao wa pili wa Kundi F ulikuwa ushindi wao wa kwanza kwenye Kombe la Dunia tangu 1998 – na wameshindwa kufuzu mashindano manne mfululizo .

Kikosi cha wachezaji 14 kati ya 26 cha Morocco kilizaliwa nje ya nchi – zaidi ya timu nyingine yoyote kwenye mashindano hayo – huku mchanganyiko wa wachezaji kutoka jamii zinazokua za wahamiaji barani Ulaya ukiwasaidia kuanza mwanzo mpya.

Mabadiliko muhimu kwa timu hiyo yalikuja miezi mitatu tu kabla ya fainali hizo wakati Vahid Halilhodzic alipotimuliwa kama kocha na nafasi yake kuchukuliwa na Regragui, ambaye alishinda ligi ya nyumbani na mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na Wydad Casablanca msimu uliopita.

Mabadiliko hayo yamesaidia kutuliza mvutano kikosini, huku winga wa Chelsea, Hakim Ziyech akitoka kustaafu kimataifa, huku kuimarika kwa wachezaji uwanjani pia kukiwashangaza wengi.

Morocco imepata uungwaji mkono kwa sauti kubwa katika Kombe la Dunia la kwanza lililofanyika katika ulimwengu wa Kiarabu na mashabiki wao wataungana na wenzao ambao watasafirishwa na shirika la ndege la Royal Air Maroc Casablanca hadi Doha Jumanne na Jumatano.

Makadirio ya idadi inayobadilika-badilika ya mashabiki wa Morocco nchini Qatar ni kati ya 20,000 hadi 40,000.

Wachezaji hao wamekuwa mashujaa huku kukiwa na sherehe za furaha za ushindi kote Afrika Kaskazini, na kwa wanadiaspora barani Ulaya, – mfano wa Achraf Hakimi akimbusu mama yake baada ya ushindi na winga Sofiane Boufal akicheza na wake uwanjani baada ya kuifunga Ureno kwenye robo -fainali.

Timu hiyo pia imeonyesha imani zao za Kiislamu, wakiinama kwa sujud (kusujudu) mbele ya mashabiki wao baada ya kupiga hatua raundi ya mtoano.

Lakini ni nani anayeshiriki katika kikosi kinacholenga kuishangaza Ufaransa – wakoloni wa zamani ambao Morocco ilipata uhuru wao mnamo 1956 – kwenye Uwanja wa Al Bayt mnamo Jumatano (19:00 GMT)?

Morocco iliifunga Uhispania 3-0 kwa penalti baada ya sare ya 0-0 katika hatua ya 16 bora, huku Hakimi akifunga mkwaju wa penalti.

Bono na Maldini wa Morocco – Safu yao ya Ulinzi

Uimara wa safu ya ulinzi umekuwa jambo muhimu, baada ya kufungwa bao moja pekee katika mechi nane chini ya Regragui – bao lenyewe likiwa la kujifunga katika ushindi dhidi ya Canada.

 

Beki wa kulia Hakimi bila shaka ndiye nyota wa kikosi hicho na si mgeni kwa vilabu vikuu vya Ulaya, huku akiwa na Real Madrid, Borussia Dortmund na Inter Milan -tayari akiwa amevichezea vyote akiwa na umri wa miaka 24.

Imemlazimu kupunguza hisia zake za ushambuliaji kwa kiasi fulani, lakini nyota huyo wa Paris St-Germain alionyesha hasira na kipaji chake kupitia mkwaju wake wa penalti wa mbinu ya Panenka uliokamilisha ushindi wa hatua 16 bora dhidi ya Uhispania.

Ounami na Boufal

Nahodha Romain Saiss, aliyeitwa ‘Maldini wa Morocco’ na kocha wa zamani wa Wolves Bruno Lage, na Nayef Aguerd wa West Ham wamekuwa na nguvu kwenye safu ya beki wa kati, lakini wote wawili wakiwa na matatizo ya majeraha kwenye mechi dhidi ya Ufaransa, Jawad El Yamiq na Badr Benoun wanaweza kuitwa kuchukua mahala pao.

El Yamiq mwenye umri wa miaka 30 ambaye sasa anachezea Uhispania Real Valladolid baada ya kuichezea Italia, alikuwa sehemu ya kikosi cha Morocco kilichotwaa Ubingwa wa Mataifa ya Afrika, mashindano ya wachezaji wa nyumbani, mwaka 2018 huku Benoun mwenye urefu wa futi 6’3, alipewa jina la utani ‘Sultan’ na wachezaji wenzake wa Al Ahly kabla ya kuhama kutoka kwa wababe hao wa Misri kwenda klabu ya Qatar mwaka huu.

Huku mchezaji wa Bayern Munich, Noussair Mazraoui akiondolewa kwenye robo fainali kutokana na jeraha, Yahya Attith-Allah – mmoja wa wachezaji watatu kwenye kikosi kutoka klabu ya zamani ya Regragui ya Wydad – ameingia na kuonekana mtulivu licha ya kucheza mechi yake ya kimataifa mwezi Machi.

Ukishapita ulinzi mkali zaidi, itabidi utafute njia ya kumpita Kipa Yassine Bounou, mzaliwa wa Canada anayejulikana kama Bono.

Akirejea Urusi miaka minne iliyopita, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alishinda Ligi ya Europa akiwa na Sevilla mnamo 2020 na alishinda taji la Zamora msimu uliopita kwa kuwa kipa bora wa La Liga ya Uhispania.

“Unapokuwa na mmoja wa makipa bora zaidi duniani, inakufanya ujiamini , na Yassine anatupa hilo,” alisema Regragui baada ya timu yake kuitoa Ureno.

“Alitusaidia sana na anaposhiriki mechi, kwa hakika hatuwezi kuzuilika.”

‘Mvulana huyu anatoka wapi?’- kiungo wa kati mwenye bidii

Sofyan Amrabat amekuwa mmoja wa wachezaji bora waliosaidia Morocco kufuzu kwa hatua ya nne bora, huku kukaba kwake bila kuchoka kukiweka ukuta thabiti kwa safu ya ulinzi ya Morocco.

Kaka mdogo wa winga wa zamani wa Watford Nordin, ambaye alimbadilisha katika mchezo mmoja kwenye fainali za 2018, Sofyan mzaliwa wa Uholanzi aliiwakilisha Uholanzi katika kiwango cha wachezaji wa chini ya miaka 15 na uchezaji wake umeimarika katika klabu ya Fiorentina msimu huu.

Kando yake katika safu ya kiungo ni Azzedine Ounahi -mmoja wa wachezaji wanne katika kikosi ambao wanatoka katika Chuo cha Mohammed VI – ambaye uchezaji wake wa sanduku hadi sanduku unavutia baadhi ya vilabu vikubwa barani Ulaya.

“Mungu wangu, huyo kijana anatokea wapi?” aliuliza kocha wa Uhispania Luis Enrique baada ya kutolewa katika hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penalti.

“Anacheza kama wachezaji wa Uhispania. Hajaacha kukimbia, lazima awe amechoka.”

Youssef En-Nesyri amefunga kutokana na juhudi zake zote tatu kwenye fainali za Kombe la Dunia – moja mwaka wa 2018 na mawili mwaka huu.
 

Akichezea klabu ya daraja la chini ya Angers nchini Ufaransa, mchezaji huyo wa kiufundi lakini mwenye umri wa miaka 22 alicheza mechi yake ya kimataifa mwezi Januari na kufunga mabao mawili katika ushindi wa mchujo wa kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya DR Congo miezi miwili baadaye na kuisaidia Morocco kufuzu.

 

“Simu inalia? Inalia sana,” mwenyekiti wa Angers, Said Chabane aliiambia RMC ya Ufaransa kuhusu nia ya Ounahi na mzalendo Boufal, ambaye pia ameanza kila mechi nchini Qatar.

 

Wakati huo huo, mchezaji Selim Amallah, aliyewahi kutamaniwa na meneja wa zamani wa Ubelgiji Roberto Martinez, pia amevutia ingawa hajacheza mchezo wa klabu tangu Septemba kwa sababu ya mvutano wa kandarasi na Standard Liege.

Kama Giroud kwa Ufaransa – Anatumia nguvu katika mashambulizi

Youssef En-Nesyri anaongoza safu ya mashambulizi , licha ya kutoifungia Sevilla msimu huu katika La liga , mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ana nafasi yake katika vitabu vya historia vya Kombe la Dunia la Morocco.

Mabo yake ya ushindi dhidi ya Canada na Ureno yamemfanya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa nchi yake kwenye fainali hizo akiwa amefunga mabao matatu, akiwa pia amefunga mabao katika mechi ya hatua ya makundi na Uhispania mwaka 2018.

“Siku zote nimekuwa nikimwamini Youssef kwa sababu anatoa nguvu kubwa,” Regragui alisema.

“Kocha yeyote angependa awe katika timu yake kwa sababu anafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya timu, kama (Olivier) Giroud wa Ufaransa.”

Ziyech anajulikana sana tangu alipokuwa na Ajax na Chelsea, lakini Regragui amepata ubora zaidi kutoka kwa mchezaji ambaye mchezo wake wa klabuni imekuwa ukitofautiana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa katika jangwa la kimataifa kati ya Juni 2021 na Septemba mwaka huu baada ya kutofautiana hadharani na kocha Halilhodzic, lakini sasa mechi zake nane kwenye fainali za Kombe la Dunia ni rekodi ya pamoja ya kitaifa pamoja na Hakimi.

Boufal, mmoja wa wachezaji wawili wa Morocco waliozaliwa Ufaransa (Saiss mwingine), amerejea katika kiwango chake bora cha kimataifa akiwa Angers, baada ya kufunga mabao matatu pekee katika mechi 70 za Ligi Kuu ya England katika kipindi cha miaka minne akiwa Southampton kilichomalizika 2020.

Yeye ni miongoni mwa wachezaji watano wa kikosi hicho wanaocheza kwenye ligue 1 ya Ufaransa , pamoja na Zakaria Aboukhlal (Toulouse), Achraf Dari (Brest), Hakimki na Ounahi.

Ufahamu wa ndani wa Hakimi kuhusu nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, mshirika  mwenza wa timu ya PSG mjini Paris, utakuwa jambo la msingi ikiwa Morocco inaweza kuondoa kile ambacho bila shaka kinaweza kuwa msukosuko mkubwa zaidi wa Kombe la Dunia katika historia yake.

“Hatujaridhika na nusu fainali na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufanya hivyo. Tunataka kwenda mbali zaidi,” Regragui alisema.

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories

ZAA to audit ground handlers
Popular
Investment News Editor

Zanzibar Airport Authority to audit ground handlers

Unguja. The Zanzibar Airports Authority (ZAA) is set to conduct an audit on ground handling companies that currently operate at the Abeid Amani Karume Airport with effect from Monday. The week-long audit is set to include Transworld, ZAT and the newcomer Dnata Zanzibar who were licensed in June plus exclusive rights to manage Terminal 3 building by ZAA.Continue Reading