Vyuo vya mafunzo ya amali kutoa fursa vijana kujiajiri

Vyuo vya mafunzo ya amali kutoa fursa vijana kujiajiri

Unguja. Vyuo vya mafunzo ya amali vimetajwa kuwa ni fursa muhimu kwa vijana kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar, Dk Bakari Ali Silima ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Septemba 10, 2024 wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha nne wa shule mbalimbali kwenye ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya mafunzo ya amali, yanayofanyika katika Chuo cha Amali Mwanakwerekwe, Unguja.

 “Juhudi za Serikali kujenga vyuo vya amali kila wilaya zinaendelea, ili kuona vijana wanapomaliza masomo yao wanapata fursa ya kujiunga katika vyuo hivyo kupata ujuzi na maarifa bora,” amesema Dk Silima.

Amewataka wanafunzi hao kuzitumia fursa zinazotolewa na Serikali wanapomaliza elimu yao ya sekondari ili kupata ujuzi utakaowajengea mustakabali mwema wa maisha yao.

Mbali na hayo, amewataka wanafunzi hao kuwa mabalozi kwa wengine ili wanapomaliza masomo yao kuacha kukaa mitaani na kufanya matukio yasiostahiki na badala yake kujiwekeza katika eneo hilo ili kujipatia maendeleo. 

Kwa upande wake, Mkaguzi Mkuu wa Vyuo vya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali, Ibrahim Salim Haji amesema wiki ya mafunzo ya amali inasaidia kumjenga mwanafunzi na kumpa mwamko mzuri wa maisha yake ya baadaye. 

Amesema kupitia hatua hiyo mwanafunzi anaonyeshwa fursa ya kuchagua anachoweza kufanya. 

“Tumeaandaa maonyesho haya kupitia vyuo vyote vya Unguja na Pemba ikiwa ni moja na kuwashajihisha vijana, jamii na wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza masomo yao, kutembelea katika vyuo hivyo,” amesema.

Baadhi ya wanafunzi waliofanya ziara katika chuo hicho wameelezafarijika kupata fursa ya kujua faida zinazopatikana chuoni hapo. 

Maonyesho hayo ya wiki moja yameanza Septemba 9 na yanatarajiwa kufungwa Septemba 15, 2024.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Top News
Investment News Editor

ZSSF money not for projects, says Ali Karume

Unguja. Veteran politician and diplomat Ali Karume has called on authorities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) to refrain from using the Zanzibar Social Security Fund money for establishing commercial projects.Continue Reading