Vijiji vinane Kisiwani Pemba vimekosa huduma ya maji

Vijiji vinane Kisiwani Pemba vimekosa huduma ya maji

VIJIJI 8 PEMBA WALIA NA ZAWA

Na Mwandishi Wetu, Pemba

Vijiji vinane Kisiwani Pemba vimekosa huduma ya maji safi na salama huku wakiilalamilia Mamlaka ya Maji Zanzibar kushindwa kutatua tatizo la maji katika Vijiji vyao.

Vijiji vikivyokosa maji ni katika Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba.

Wakizungumza kwa nyakato tofauti, wananchi wamesema huduma ya maji si ya uhakika, ni ya kubahatisha hali inayowafanya kupata usumbufu.

Zaidi ya wakaazi 6,000 katika Vijiji vya Kichekwani, Nduaga, Tundumwe, Mkunguni, Msasani na Momogu hawana maji safi na salama.

Magonjwa yatokanayo na maji yameondolewa kama tatizo la afya ya jamii katika maeneo mengi ya visiwa vya Pemba na Unguja, lakini maambukizi yanabaki kuwa suala ambalo maji safi hayapatikani

Wakaazi hao wamesema wanalazimika kununua maji ambayo wanayatumia kwa ajili ya kupikia na kunywa.

Wakaazi hao wanatumia maji ya bahari kwa ajili ya kukoshea vyombo na shughuli nyengine.

Kurata Bakar Said amesema huduma ya maji ya ZAWA imekuwa adimu na hawajui lini wataondokana na dhiki ya maji.

Fatma Mohamed Awadhi amesema kuwa maji ya ZAWA yamekuwa tunu kwao huku mifereji yao imebakia kuwa pambo ndani ya nyumba zao.

Sheha wa Shehia ya Shumba Mjini, Rahila Ramadhan Juma amesema amesema malalamiko ya wananchi ni mengi kuhusu ukosefu wa huduma ya maji.

” Kwa hakika, huduma ya maji ya ZAWA katika Shehia yangu ni tatizo sugu, wapo wananchi wananunua maji, wasiokuwa na uwezo wanatumia maji ya bahari” Alisema Sheha Rahila.

Tanzania, Zanzibar, Tatizo la Maji Kisiwani Pemba

Leaders in Tanzania linked to destruction of the environment

The Tanzanian government has said that there are some leaders in the country for their personal interests who are contributing to the destruction of the environment including water sources and causing rivers to dry up. 12 families of leaders including ministers, politicians and judges are accused of being involved in the destruction of the water sources of the Ruaha Mkumu River.Continue Reading

Climate change: Empty water taps for weeks, a wake-up call

Tanzania: Empty water taps for weeks wake-up call

Tanzania: Empty water taps for weeks wake-up call. At least for regulated bottled water businesses, we are assured of safety. But for the water from dubious sources, including those close to sewers, there may be a spike of diseases like cholera, and diarrhea, among others.Continue Reading

Protecting Water Sources – Tanzania State Directives

Tanzania Water Crisis: VICE-PRESIDENT Dr Philip Mpango has directed Regional Commissioners to supervise the countrywide campaign of planting water friendly trees along water sources, while ordering people who have built houses on mountainous sources of water to immediately vacate in order to protect the areas.Continue Reading

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories