Utafiti: Marekani huchangia misaada ya Sh7.3 trilioni Tanzania kila mwaka

Utafiti: Marekani huchangia misaada ya Sh7.3 trilioni Tanzania kila mwaka

Dar es Salaam. Wakati uhusiano kati ya Tanzania na Marekani ukifikisha miaka 63, imebainika Tanzania imekuwa ikipokea misaada inayofikia Sh7.32 trilioni kila mwaka kwa miaka 10 mfululizo tangu mwaka 2012.

Ripoti ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya William and Mary’s Global Research institute na Taasisi ya Utafiti wa Kundoa Umasikini (Repoa) imetaja sekta zilizoguswa na msaada huo ni afya, elimu, kilimo, biashara na utalii.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Juni 18, 2024 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ripoti ya Kuwekeza kwa Watu Tanzania, iliyokusanya takwimu za miaka 10 iliyopita kuanzia mwaka 2012 hadi 2023.

Akitoa matokeo ya utafiti huo, mtaalamu mwandamizi wa sera wa taasisi ya AidData, Divya Mathew amesema umejikita katika ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na Marekani.

“Tumechukua takwimu za misaada na biashara iliyofanyika ikihusisha Serikali na sekta binafsi ikiwa pamoja na mtu mmoja mmoja zikiwamo fedha zilizotolewa na Watanzania waishio Marekani.

“Tumeona kuna wastani wa Dola2.8 bilioni (Sh7.32 trilioni) zinazoingia kwenye uchumi wa Tanzania kwa miaka kwa miaka 10 mfululizo,” amesema Mathew.

Akizungumzia utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk Donald Mmari amesema utafiti huo umeonyesha kuwepo kwa mafanikio kwa pande zote mbili.

“Kwa mfano katika sekta ya afya kumekuwa na msaada ya takribani Dola 394 milioni (Sh1 trilioni) hususani katika magonjwa ya Ukimwi na malaria na kumekuwa na mafanikio ya kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa hayo,” amesema Dk Mmari.

Ametaja pia maeneo ya usalama wa chakula na sekta binafsi akisema yameguswa.

“Kuna eneo la miundombinu, Shirika la Millenium Challenge liliwekeza takribani Dola 700 milioni (Sh1.83 trilioni) katika barabara na umeme.

“Kuna maeneo ya ulinzi na usalama, kuna biashara na uwekezaji katika madini na utalii. Kuna kampuni za Tanzania zimeuza bidhaa zake katika soko la Marekani, fursa iliyotokana na Sheria ya Agoa inayotoa fursa kwa wazalishaji wa Afrika kuuza bidhaa bila kutozwa ushuru,” amesema Dk Mmari.

Ametaja pia ubadilishanaji wa wataalamu, akisema kuna walimu wa Marekani wanaokuja kufundisha Tanzania na kufanya utafiti na pia wapo wanafunzi wanaokwenda kusoma Marekani kwa ufadhili.

Mkurugenzi wa uchambuzi wa sera wa AidData, Samantha Custer amesema licha ya uhusiano wa muda mrefu wa nchi hizo mbili, viongozi na wananchi wengi wa Tanzania hawana taarifa za kutosha, hasa wakati huu ambao Tanzania inatathmini mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025.

“Ni matumaini yetu, ripoti hii itasaidia kuwaelewesha watunga sera kuona kama ushirikiano wa Marekani na Tanzania unachangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania,” amesema Dk Mmari.

Akizungumzia mchango wa Marekani katika sekta ya kilimo na usalama wa chakula nchini, Profesa David Nyange amesema miongoni mwa miradi iliyoonyesha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ilikuwa ni ujenzi wa Chuo cha Kilimo cha Morogoro kilichobadilishwa kuwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

“Chuo hiki kimechangia katika kuzalisha rasilimali katika sekta mama ya kilimo kinachozalisha chakula,” amesema Profesa Nyange.

Ametaja miradi mingine ni ushirikiano katika utafiti wa kilimo uliohusisha vyuo vikuu mbalimbali vya Marekani.

“Ushirikiano pia umeonekana kwa ushirika wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha SUA (Sugeco) kwa kuwezesha kupeleka zaidi ya wahitimu 200 nchini Marekani na kuwaunganisha na programu za kilimo biashara,” amesema Profesa Nyange.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Top News
Investment News Editor

ZSSF money not for projects, says Ali Karume

Unguja. Veteran politician and diplomat Ali Karume has called on authorities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) to refrain from using the Zanzibar Social Security Fund money for establishing commercial projects.Continue Reading

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income

Insurer and financial services provider Britam posted a 22.5 percent jump in net earnings for the half-year ended June 2024, to Sh2 billion, buoyed by increased investment income.

The rise in half-year net profit from Sh1.64 billion posted in a similar period last year came on the back of net investment income rising 2.5 times to Sh13.27 billion from Sh5.3 billion.

“We are confident in the growth and performance trend that Britam has achieved, supported by its subsidiaries in Kenya and the region. Our business is expanding its revenue base while effectively managing costs,” Britam Chief Executive Officer Tom Gitogo said.

“Our customer-centric approach is fueling growth in our customer base and product uptake, particularly through micro-insurance, partnerships, and digital channels.”

The investment income growth was fueled by interest and dividend income rising 34 percent to Sh9.1 billion, which the insurer attributed to growth in revenue and the gains from the realignment of the group’s investment portfolio.

Britam also booked a Sh3.79 billion gain on financial assets at a fair value, compared with a Sh1.8 billion loss posted in a similar period last year.

The increased investment income helped offset the 12.7 percent decline in net insurance service result to Sh2.13 billion in the wake of claims paid out rising at a faster pace than that of premiums received.

Britam said insurance revenue, which is money from written premiums, increased to Sh17.8 billion from Sh16.6 billion, primarily driven by growth in the Kenya insurance business and regional general insurance businesses, which contributed 30 percent of the revenue.

The group has a presence in seven countries in Africa namely Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, South Sudan, Mozambique, and Malawi.

Britam’s insurance service expense hit Sh13.6 billion from Sh11.3 billion, while net insurance finance expenses rose 2.6 times to Sh12.3 billion during the same period.

“Net insurance finance expenses increased mainly due to growth in interest cost for the deposit administration business driven by better investment performance. This has also been impacted by a decline in the yield curve, which has led to an increase in the insurance contract liabilities. The increase has been offset by a matching increase in fair value gain on assets,” said Britam.

Britam’s growth in profit is in line with that of other Nairobi Securities Exchange-listed insurers, which have seen a rise in profits.

Jubilee Holdings net profit in the six months increased by 22.7 percent to Sh2.5 billion on increased income from insurance, helping the insurer maintain Sh2 per share interim dividend.

CIC Insurance Group posted a 0.64 percent rise in net profit to Sh709.99 million in the same period as net earnings of Liberty Kenya nearly tripled to Sh632 million from Sh213 million, while Sanlam Kenya emerged from a loss to post a Sh282.2 million net profit.

Continue Reading