Utafiti kufanyika kubaini sumu ya samaki aina ya kasa

Utafiti kufanyika kubaini sumu ya samaki aina ya kasa

Unguja. Baada ya kutokea vifo vya mara kwa mara vinavyotokana na ulaji wa samaki aina ya kasa, sasa utafanyika utafiti wa sumu asili (Biotoxin) zilizomo ndani ya samaki huyo kuzitambua na athari zake.

Baada ya kutambua sumu hizo, elimu itakayopatikana kutokana na utafiti huo itatumika katika kuelimisha jamii kuhusu athari zitokanazo na ulaji wa kasa. 

Hatua hiyo inakuja baada ya kutokea vifo na  wengine kulazwa hospitalini baada ya kula nyama ya kasa katika visiwa vya Unguja na Pemba ambapo tukio la Machi 5, mwaka huu walikufa watu tisa na wengine 98 kulazwa hospitalini baada ya kula kasa katika Kisiwapanza Pemba. 

Hayo yamebainishwa leo Jumanne, Mei 21, 2024 na Waziri mwenye dhamana, Shaaban Ali Othman katika Mkutano wa Bajeti wa 15 wa Baraza la wawakilishi unaoendelea Chukwani mjini hapa. Hata hivyo, hakusema utafiti huo unatarajia kuanza lini. 

Shaaban alikuwa akijibu swali la mwakilishi wa Kiwani, Mussa Foum Mussa aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kudhibiti vifo inavyotokana na ulaji wa samaki huyo. 

Kwa mujibu wa kifungu cha saba, sheria namba saba ya mwaka 2010 inapiga marufuku kuvua samaki huyo na ulaji wake,  lakini wavuvi wamekuwa wakiendelea kumvua na wananchi kumla bila kujali athari zake. 

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Shaaban Ali Othman akijibu maswali ya Wawakilishi katika mkutano wa 15 wa Bajeti Chukwani Unguja.

Alipouliza kitu gani kinafanyika kwa watu wanaobainika kufanya makosa hayo licha ya sheria kukataza, mwakilishi wa nafasi za wanawake, Shadya Mohamed Suleiman, Waziri Shaabani amesema wanawakamata na kuchukuliwa hatua. 

Amesema mpaka sasa kuna wavuvi wanne wameshikiliwa katika Mkoa wa Kusini Unguja na kesi zao zinaendelea kusikilizwa. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu anayevua kasa anatozwa faini kati ya Sh100,000 na Sh5 milioni au kifungo. 

Hata hivyo, Waziri Shaaban amesema wavuvi wanaoendelea kuvua kasa wanapata nguvu kutoka kwa Wawakilishi hao ambao pindi wakikamatwa wanawatumia kutaka waachiliwe, hivyo aliwataka kuacha tabia hiyo na sheria ichukue mkondo wake.

 “Hapa lazima tuseme ukweli, wapo baadhi ya wawakilishi wanaochangia suala hili liendelee kwani tunapochukua hatua za kuwakamata, tunapigiwa simu kuwa tuwaachie sasa tusaidiane tuache kufanya hivyo,” amesema.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal

Ruling party Chama Cha Mapinduzi-Zanzibar has said it is ready to task state organs to investigate some of the claims against its government that have been raised by opposition politicians on the Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA).Continue Reading