Umeliona hilo goli la Brazil, Richarlison?

Umeliona hilo goli la Brazil, Richarlison?

Goli hilo kutoka kwa Richarlison!

Richarlison alikuwa mchezaji bora wa saa katika mechi ya ufunguzi ya Brazil ya Kombe la Dunia la 2022 dhidi ya Serbia kwenye Uwanja wa Lusail Iconic nchini Qatar.

Mshambulizi huyo wa Brazil alifunga bao la kuvutia kwa kiki ya kimiujiza ya mkasi, na kusaidia kikosi chake kuishinda Serbia, 2-0.

Dakika ya 73, Richarlison alipokea mpira kwenye eneo la hatari akiwa amejifunga goli. Kutoka hapo, kwa mwendo mmoja, Richarlison alirusha mpira hewani alipogusa mara ya kwanza na kuuzungusha mwili wake ili kufanya teke la mkasi wa hali ya juu. Kombora lake lilimpita beki wa Serbia Miloš Veljković na kumpita kipa Vanja Milinkovic-Savic.

Richarlison: Mfahamu mshambuliaji wa Brazil aliyezima matumaini ya Serbia

Kituo cha basi kilichojengwa na matofali mekundu katika mji mdogo wa Nova Venecia nchini Brazili kina hadithi ya kusimulia.

Kikiegemea rasi na mkahwa unaoweza kula chochote kwa £ 2 , hali inayowafanya walevi kunywa hadi kuzimia , ni alama ya mwanzo wa safari ya Richarlison kwenye Ligi ya Premia.

Akiwa na umri wa miaka 17 na kukatishwa tamaa na kukataliwa mara kwa mara, ni kutoka hapa ndiposa aliondoka nyumbani kwa safari ya saa 11, kilomita 600 hadi eneo la Belo Horizonte, akiwa na buti za kuazima na kukosa  pesa za tikiti ya kurudi.

Ilikuwa 2014. Majaribio ya klabu za Avai na Figueirense hayakuzaa matunda , wakati ambapo timu yake ya taifa ilikuwa imedhalilishwa katika ardhi ya nyumbani kwenye Kombe la Dunia. Huku akivutia watu wachache licha ya kuwa mfungaji bora akiichezea Real Noroeste kwa wachezaji wlio chini ya miaka 20, Mshambuliaji huyo chipukizi alikuwa akipoteza matumaini.

Alijaribu safari ya basi kuelekea magharibi – kwa majaribio na timu ya daraja la pili America-MG – nafasi yake kubwa ya mwisho. Aliamua kutokukata tamaa.

“Nakumbuka siku hiyo,” rafiki wake wa utotoni Pedro Emanuel aliambia BBC Sport.

“Aliniambia anaenda, lakini hakuwa na buti. Kwa kweli, alikuwa na jozi nyeusi lakini zilikuwa zimekatika. Nilimwambia:  kuna jozi hapa, za bluu na nyekundu zinazovutia macho. , unapaswa kuzichukua.’ Namshukuru Mungu kila kitu kilifanikiwa.”

Hakika alifanikiwa, jaribio hilo likamfanya kucheza misimu mitano mfululizo kwenye ligi ya Premier  na klabu za Watford na Everton. Katika hatua ya kimataifa Richarlison ni mshindi wa Copa America, mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki ya 2020, na uhakika wa kushinda Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar akiwa na Brazil.

Lakini yote hayo yangekuwa tofauti .

Wazazi wa Richarlison walitengana alipokuwa na umri wa miaka sita, hivyo alitumia miaka mitatu akiishi na baba yake Antonio, akifanya kazi kwenye shamba la babu yake akisaidia kuvuna maharagwe ya kahawa, akisafiri safari ndefu kila wikendi ili kucheza mechi.

Kufikia umri wa miaka saba, watu walikuwa wakimwambia Antonio awekeze kwa mtoto wake kwa sababu alikuwa na talanta maalum. Alijibu kwa kununua mipira kumi  10 na kumpeleka kuishi na yake shangazi huko Nova Venecia.

“Tulikuwa maskini sana wakati huo,” Antonio aliambia BBC Sport, akiwa amevalia jezi ya mazoezi ya Nova Venecia FC, ambayo yeye ni rais na mwanawe ni balozi.

“Maisha ya utotoni yalikuwa magumu sana kwake na kwangu pia ulikuwa wakati mgumu kwa sababu tuliishi mashambani na kila wiki tulilazimika kupanda nyuma ya lori kwenda kwenye mechi za mpira wa miguu. Watu waliendelea kusema kwamba ana maisha ya baadaye, kwa hivyo wakati alitimiza miaka tisa nilimwacha na dada yangu.”

Richarlison alijisaidia kimaisha kwa kufanya kazi ya kuuza ice cream na chokoleti mitaani, kuosha magari, kufanya kazi katika mikahawa na mjomba wake Elton, mbali na kuwa msaidzi wa fundi matofali.

Ingawa Antonio anakiri kwamba mwanawe hakuwa mszuri sana katika masomo, wafanyakazi katika shule ya Tito dos Santos Neves katika kitongoji cha Rubia wanamuelezea kuwa mvulana mwenye tabia nzuri, mwenye nywele zilizotiwa rangi ya manjano kama Neymar – mchezaji anayemuenzi. Mlinzi wa shule hiyo anamkumbuka akitumia lango la mbele la siku na kukimbia moja kwa moja kuelekea uani nyuma kucheza kandanda. Walimu wanakumbuka unyenyekevu wake na tabia njema.

“Hakupenda kusoma, lakini alikuwa na nidhamu,” anasema Elisangela Monteiro Guidi, ambaye alimfundisha Richarlison alipokuwa na umri wa miaka 11.

“Sikuzote alikuwa na tabia nzuri; hakuwa mvulana muasi kwa vyovyote vile. Alikuwa na heshima kwa walimu wake na hiyo ilitokana na familia yake, ambao ni watu wema. Kwa hakika, wakati huo na katika eneo hili, angeweza kujihusisha na dawa za kulevya na ghasia, lakini sikuzote aliweza kuepuka hilo.”

Sio kila wakati. Akiwa na umri wa miaka 14, Richarlison alishikiwa bunduki na mchuuzi wa eneo hilo ambaye aliamini kuwa alikuwa akijaribu kuvamia eneo lake. Naye Antonio anakumbuka alipoitwa na shule siku nyingine baada ya mwanawe kushikwa na polisi barabarani.

“Tulikuwa na wasiwasi kwa sababu eneo hilo wakati huo lilikuwa hatari,” Antonio anasema. “Lakini ilikuwa ni kesi ya kupatikana katikati. Kwa bahati mbaya, marafiki zake wengi walienda njia mbaya.”

.

CHANZO CHA PICHA,BBCSPORT

 
Maelezo ya picha,

Shule ya zamani ya Richarlison

 

Richarlison anamsifu kocha wake wa kwanza wa vijana, Fidel Carvalho, polisi, kama mwingine aliyemsaidia kujiepusha na maisha ya uhalifu. “Usikate tamaa,” ilikuwa kauli mbiu ya Carvalho. Anakumbuka kuwabana wachezaji wanane wa timu hiyo kwenye VW Gol kugombea fainali nje ya mji. Mshambuliaji huyo wa baadaye wa Everton alisafiri kwenye buti na wakarudi kama mabingwa.

Kufikia umri wa miaka 16, Richarlison alikuwa akicheza kama mchezaji mchanga  na klabu ya Real Noroeste na kutawala katika timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20 huku nguvu na kasi yake ikionekana kuwa tatizo hata kwa wale wakubwa wa miaka ishirini na mitatu.

Mambo hayakwenda vyema wakati mazungumzo na klabu hiyo yaliposhuhudia uhamisho wake wa 2014 kwenda America-MG kukaribia kuporomoka.

Baada ya mgogoro wa mjuda mrefu ,Real iliruhusiwa kubaki na asilimia fulani ya haki zake, lakini msimamo wa klabu hiyo uliathiri afya ya akili ya Antonio, ambaye tayari alikuwa na msongo wa mawazo. Hadi leo, Richarlison hapendi kuzungumza juu ya kipindi hicho.

Ikiwa kuondoka Real ilikuwa ngumu, kijana huyo alizoea maisha ya Amerika kwa urahisi. Akiwa mmoja wa wavulana wawili pekee waliochaguliwa kwa majaribio, alijiunga na timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 kabla ya kufuatiliwa kwa kasi na  timu ya wacheza wasiozidi umri wa miaka  U20 kufuatia mabao yake manne katika mechi zake nne za kwanza.

Mkurugenzi wa Amerika Euler de Almeida Araujo anakumbuka kuvutiwa na nguvu na uthubutu wake – aliimarishwa kutokana na kukimbia kupanda na kushuka kwenye mitaa yenye vilima, yenye mawe ya Nova Venecia. Wiki kadhaa baadaye, alikuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza.

“Alicheza kwenye wingi na angechezewa vibaya sana lakini mara chache alianguka,” anasema Araujo.

“Mabeki wangempiga na kuanguka. Utafikiri lazima ataumia, lakini angerudi na kuendelea. Hakukata tamaa. Alikuwa kama Ronaldo mchanga kwa maana hiyo – nguvu hizo za kimwili na uamuzi katika umri mdogo kama huo.”

.

CHANZO CHA PICHA,BBCSPORT

 
Maelezo ya picha,

Richarlison alihamia Nova Venecia akiwa mvulana mdogo ili kuishi na shangazi yake

 

Ushindani wa Richarlison haukuwa kwenye uwanja pekee. Mtaalamu wa masaji nchini Marekani Silvio Junio ​​Nunes da Silva anakumbuka kwamba ilimbidi kumchukua mwanawe mchanga kazini usiku mmoja kabla ya mechi.

“Richarlison alikuwa akicheza PlayStation, kwa hivyo mwanangu aliuliza kama angeweza kucheza pia,” anasema.

“Niliwaacha wakifanye hivyo, lakini niliporudi, Richarlison alikuwa ameshinda 11-0. Nikasema: “Imetosha, jamani.” Lakini hakuwa na huruma. Alitaka kuendelea kufunga, aendelee kushinda. Alikuwa na miaka 17, mwanangu alikuwa na miaka saba. Hamu hiyo ya kushinda iko kwenye damu yake.”

Marcelo Toscano alicheza mbele na Richarlison mwaka wa 2015 Amerika ilipopandishwa daraja hadi Serie A. Anamkumbuka mchezaji mwenye kipawa, unyenyekevu – na pua kubwa.

“Nilisema tangu mwanzo kwamba angefika mbali – kwa sababu ya maadili yake ya kazi, uamuzi wake, kipaji chake, na unyenyekevu wake. Tulifunga mabao mengi msimu huo na sio bahati mbaya yuko hapa alipo leo.”

Richarlison alikaa Amerika kwa mwaka mmoja tu, akifunga mara tisa katika mechi 24 kabla ya kuuzwa kwa Fluminense kwa R$10m (ya thamani ya £1.6m leo) akiwa na umri wa miaka 18 tu. Hata hivyo aliacha hisia – na si tu kwa sababu walibakiza 20% ya haki zake za kiuchumi, na hivyo kupata mafanikio alipohamia Watford mwaka 2017 kwa £11.5m.

Ongea na mtu yeyote kwenye klabu na wana hadithi ya kushiriki kuhusu mwenzao maarufu wa zamani na mtazamo wake wa unyenyekevu.

Kwa mfano, wakati mchezaji kijana huko Amerika anapopokea mshahara wake wa kwanza wa kitaaluma, sheria za klabu zinaamuru kwamba wanapaswa kuondoka kwenye mabweni ya chuo ili kutoa nafasi kwa mtu mwingine.

Richarlison, badala ya kukodisha nyumba nzuri iliyotambuliwa na wakala wake, alipendelea kuendelea kuishi na wachezaji wenzake – na panya wa mara kwa mara ambaow alitembelea vyumba vya kulala nyakati za jioni. Aliondoa 20% tu ya mshahara wake wa kwanza na akatumia iliyobaki kusaidia familia yake nyumbani.

“Alikuwa mtu wa kawaida, mnyenyekevu sana, na mtu mzuri sana ambaye alimsaidia kila mtu ambaye angeweza,” anasema Ze Ricardo, beki wa kushoto wa Marekani ambaye aliishi na Richarlison kwenye mabweni.

“Wavulana ambao hawakuwa na buti, aliwapa zake. Ana moyo mzuri sana.”

Unyenyekevu na huruma hiyo imesalia hata kama kazi yake inatikisa.

Antonio anaongeza: “Alikuwa na uhusiano wa karibu sana na babu yake – kila mtu anasema mambo sawa kuwahusu; watu wanyenyekevu, wachapa kazi.

“Siku zote tulimfundisha kuwa hivyo . Hata leo, huwa nasema kwamba lazima asipoteze maadili hayo , lazima awe mkakamavu.

“Na yeye hufanya hivyo. Kila anapokuja Nova Venecia anamsaidia yeyote anayeweza. Kama ingekuwa juu yake, bado angetembea huku na huko kwenye barabara zake, akicheza mpira na watoto shambani, kama ilivyokuwa akifanya hapo awali. Kwa bahati mbaya, ni hatari zaidi kwake sasa, kwa hivyo anafanya zaidi mtandaoni.”

.

CHANZO CHA PICHA,BBCSPORT

 
Maelezo ya picha,

Babake Richarlison Antonio katika eno la kufanyia zoezi la klabu ya Nova Venecia

 

Wachezaji wachache wanaocheza, ikiwa wapo, wanazungumza kama Richarlison linapokuja suala la maswala ya kijamii. Amesaidia kuongeza uhamasishaji na ufadhili katika wigo mpana wa kazi ya hisani ikijumuisha ukataji miti, mzozo wa ubakaji wa Brazili, kupambana na Covid-19 na umuhimu wa kupiga kura katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu.

Mnamo 2019, muda mfupi baada ya kulilipia kundi la wanafunzi wa Brazili kusafiri kwa ndege hadi Taiwan ili kushindana katika maswali ya kimataifa ya hesabu, alivunja itifaki alipopokea tuzo ya kifahari inayopatikana kwa mwanariadha katika jimbo la nyumbani la Espirito Santo. Akiomba nafasi ya kuhutubia, aliitaka serikali ya mkoa kuwekeza zaidi katika elimu.

Mwaka mmoja baadaye na baada ya kuandaa mechi ya hisani huko Nova Venecia ambayo ilizalisha tani 6.4 za chakula kwa wale waliohitaji, alitajwa Bingwa wa Jumuiya ya Everton ya PFA.

“Sisi sote tunaocheza ligi kubwa na tuna nafasi kwenye vyombo vya habari, tuna jukumu kubwa la kijamii,” aliambia tovuti rasmi ya klabu.

“Mwanzoni, nilitaka tu kuwanunulia wazazi wangu nyumba, lakini nikaona kwamba ningeweza kufanya mambo makubwa zaidi.”

Huenda isiwe tabia ambayo mara nyingi huhusishwa na wanasoka wa Brazil, lakini ni ishara nzuri kwa nafasi yake ya kufanikiwa katika Kombe lake la kwanza la Dunia.

“Ni ndoto ambayo amekuwa nayo tangu akiwa mtoto akimtazama Ronaldo mwaka wa 2002,” anasema Antonio, umbali mfupi tu kutoka kituo cha mabasi cha matofali mekundu ambako yote yalianza.

“wakati wa fainali hiyo, alikuwa mvulana mdogo tu; sasa, anashiriki katika kombe la Dunia

“Na, ili pia nilimwambia atakuwa mfungaji bora, basi wacha tusubiri…”

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal

Ruling party Chama Cha Mapinduzi-Zanzibar has said it is ready to task state organs to investigate some of the claims against its government that have been raised by opposition politicians on the Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA).Continue Reading

Karume faults lease of Zanzibar Islets
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

Karume faults lease of Zanzibar Islets

Diplomat Ali Karume has faulted the decision by the revolutionary government of Zanzibar to lease the islets that surround the islands of Unguja and Pemba to private developers saying it was absolutely not in Zanzibar’s national interests.Continue Reading