TMA yatoa angalizo uwepo wa mvua kubwa

TMA yatoa angalizo uwepo wa mvua kubwa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza uwepo wa mvua kubwa kwa siku tano mfululizo katika mikoa kadhaa kuanzia leo Aprili 13, 2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, mvua zitanyesha kuanzia leo hadi Aprili 17, 2024.

Kwa siku ya leo tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa imetolewa kwenye maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Tahadhari ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,” imeandikwa kwenye taarifa hiyo.

TMA imetoa pia angalizo la uwepo wa athari kubwa, ikitabiriwa kuwapo mafuriko kwa baadhi ya maeneo na kuathiriwa baadhi ya shughuli za kiuchumi, uvuvi na usafirishaji baharini.

Aprili 14, 2024

TMA imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Tahadhari ya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili, imetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba),” imeeleza TMA.

Aprili 15, 2024

Mvua kubwa inatarajiwa kunyesha katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Aprili 16, 2024

Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

Taarifa imeeleza pia uwepo wa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi (mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara (pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Aprili 17, 2024

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara (pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba) inatarajiwa kuwa na mvua kubwa.

TMA pia imetoa angalizo la upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili, kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani ya Bahari ya Hindi mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara (pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories