Teknolojia yatajwa kupaisha kilimo, ufugaji

Teknolojia yatajwa kupaisha kilimo, ufugaji

Unguja. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema teknolojia imeleta mabadiliko katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Hemed amesema hayo baada ya kutembelea na kukagua bidhaa za kilimo na ufugaji leo Agosti 9, 2024 katika maonyesho ya wakulima Nanenane katika viwanja vya Dole Kizimbani, Unguja.

Amesema maonyesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata taaluma ya kulima na kufuga kwa kutumia mbinu za kisasa ambazo humuwezesha kupata mavuno mengi kwa muda mfupi na gharama nafuu.

“Teknolojia ya kilimo imeleta mageuzi makubwa katika sekta hii, wakulima wanasisitizwa kuendelea kutumia teknolojia ya kisasa ili kuendana na ushindani uliopo katka soko la dunia,” amesema.

Amesema Serikali itaendelea kuliboresha eneo la maonyesho ili litoe huduma bora kwa wakulima na wananchi huku akiwahamasisha wananchi kutembelea eneo hilo kwa lengo la kujifunza kilimo cha kisasa na chenye tija.

Waziri wa Kilimo, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Shamata Shaame Khamis amesema mwamko wa wafanyabiashara katika maonyesho hayo umekuwa mkubwa na kuvuka lengo la wizara la kusajili wajasiriamali 500, jambo ambalo limewanyima fursa baadhi yao ya kushiriki katika maonyesho hayo kutokana na wingi wa maombi.

Shamata amesema kutokana na mwamko wa wajisiriamali waliojikita kwa wingi katika kilimo na ufugaji kumeongeza uzalishaji wa ndani, hususani mazao ya mboga na kupunguza kuagiza bidhaa hizo kutoka nje ya Zanzibar.

Takwimu zinaonyesha uzalishaji wa mbogamboga na matunda umeongezeka kutoka tani 66,310 mwaka 2022 na kufikia tani 87,971 mwaka 2023.

Amesema wizara inajipanga kutanua wigo zaidi wa maonyesho hayo kwa kuboresha miundombinu katika maonyesho hayo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuonyesha biashara zao katika mazingira bora yenye kuleta ufanisi wa ufanyaji wa shuhuli zao. 

Baadhi ya washiriki wameeleza manufaa waliyoyapa ikiwemo kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kibiashara.

Zaituni Ali Juma, mkulima wa mbogamboga amesema: “Tumepata faida kwani tumeongezewa elimu, tumepata fursa ya mikopo hapahapa lakini tumeunganishwa na wadau na kupanua wigo wa masoko yetu.”

Maonyesho ya Nanenane yaliyoanza Agosti Mosi yanatarajiwa kufungwa Agosti 14, 2024.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal

Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.

The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns

Kampala — The European Commission added Air Tanzania to the EU Air Safety List, banning the airline from operating within European Union airspace. This decision follows the denial of Air Tanzania’s Third Country Operator (TCO) authorization by the European Union Aviation Safety Agency (EASA), citing significant safety deficiencies.

The EU Air Safety List includes airlines that fail to meet international safety standards. Commissioner Tzitzikostas emphasized the importance of passenger safety, stating: “The decision to include Air Tanzania in the EU Air Safety List underscores our unwavering commitment to ensuring the highest safety standards. We strongly urge Air Tanzania to take swift action to address these safety issues. The Commission has offered its assistance to Tanzanian authorities to enhance safety performance and achieve compliance with international aviation standards.”

Air Tanzania joins several African airlines banned from EU airspace, including carriers from Angola, the Democratic Republic of Congo, Sudan, and Kenya. Notable names include Congo Airways, Sudan Airways, and Kenyan carriers Silverstone Air Services and Skyward Express. The ban reflects the EU’s strict approach to aviation safety worldwide.

Source: allafrica.com

Continue Reading