Tanzania yafanya vizuri chanjo ya Uviko-19-WHO

Tanzania yafanya vizuri chanjo ya Uviko-19-WHO

Dar es Salaam. Wakati Tanzania ikiongoza mataifa ya barani Afrika kufikia malengo ya utoaji wa chanjo ya Uviko-19, wadau mbalimbali wametoa maoni tofauti huku wakipongeza.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania imeibuka nchi iliyofanya vizuri zaidi kati ya 34 za Afrika katika utoaji wa chanjo hiyo kutoka idadi ndogo ya asilimia 2.8 ya waliochanjwa Januari 2022 kabla ya kurekodi ongezeko kubwa hadi kufikia asilimia 49 Januari 2023.

Tanzania imefanya vizuri zaidi kati ya nchi 34 zilizokuwa chini ya asilimia 10 ya watu waliolengwa, kabla ya WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) na Gavi lilizindua ushirikiano wa pamoja wa utoaji chanjo (CoVDP) Januari 2022. Ili kupata matokeo chanya ya CoVDP, ilisaidia nchi kuondokana na vikwazo vya kupata chanjo.

Mwakilishi wa WHO Tanzania, Dk Zabulon Yoti alisema, “Ongezeko la kasi la chanjo ya Uviko-19 ni matokeo ya kujitolea zaidi kwa viongozi wa kisiasa katika ngazi ya kitaifa, kikanda na wilaya.”

Tanzania ilianza rasmi kuchanja watu wake Julai 28, 2021 ikiwa nyuma kati ya nchi nyingi za Afrika zilizoanza mapema kutoa kinga hiyo kwa watu wake.

Hatua hiyo ilifuata baada ya Tanzania kupokea zaidi ya dozi milioni 1.05 za chanjo aina ya Johnson & Johnson Julai 2021 zilizotolewa na Marekani kupitia mpango wa upatikanaji wa chanjo Covax.

Katika mpango huo, baadhi ya watu waliopingana na harakati hizo wakieleza chanjo hizo sio salama na wapo waliounga mkono, lakini Rais wa Samia Suluhu Hassan aliwaondoa hofu wananchi kuhusiana na hilo.

Rais Samia alisema yeye ni mama wa watoto wanne, ni bibi wa wajukuu kadhaa wanaompenda sana na yeye kuwapenda, ni mke pia lakini mbali ya yote ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi wa nchi hii, “nategemewa kama mama, kama bibi, kama Rais, kama Amiri Jeshi Mkuu, nisingejitoa mwenyewe nikajipeleka kwenye kifo, nikajipeleka kwenye hatari nikijua kwamba nina majukumu yote haya yananitegemea.

“Lakini nimetoka kuonyesha umma wanaonifuata nyuma nikijua kama Rais ni mchungaji na nina watu wengi nyuma nawachunga na wananitazama mimi hivyo nisingetoka kujihatarisha.”

Alizindua kwa kuchanja yeye kwanza na hadi kufikia Februari mwaka huu, takwimu za WHO zinaonyesha zaidi ya dozi 38,900,000 za chanjo zilipokewa bara na Zanzibar kupitia makubaliano ya pande mbili na Kituo cha Covax na jumla ya dozi zaidi ya asilimia 90 zilisambazwa mikoani.

Tangu mwanzoni mwa 2022, takwimu nchini zinaonyesha kupungua kwa idadi ya wanaolazwa hospitalini kutokana na Uviko-19, huku nchi ikikumbwa na mawimbi manne ya mlipuko wa ugonjwa huo.

Katika kufikia malengo ya uchanjaji, kulichukua muda mwingi lakini zaidi kulihusisha watu wengi wakiwamo wafadhili, wataalamu wa masuala ya afya kama madaktari, wauguzi, viongozi wa dini pamoja na Serikali za Mitaa.

“Nilipanga ratiba zangu za siku kwamba leo nitatembelea majumbani au kwenye mikusanyiko, masoko na kadhalika. Kisha saa mbili ninafika katika Zahanati ya Buigiri hufanya kazi mpaka saa 8, huwa ninawasiliana na mtoa huduma kituo cha afya kama ni siku ya chanjo ya Uviko au huduma mkoba za chanjo kwa watoto,” alisema Faraja Mbishai (25), mhudumu wa afya ngazi ya jamii katika kijiji cha Buigiri wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Dk Venance Mgaiga alisema wahudumu wa afya ngazi ya jamii wana mchango mkubwa na nguvu kwenye jamii kuhusiana na masuala ya huduma za afya ni mfano ambao Chamwino wameuona kwenye chanjo, zaidi ya asilimia 60 ya waliochanjwa Uviko-19 ni mchango wao.

Miongoni mwa wadau muhimu zaidi katika kufanikisha hilo ni daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Elisha Osati ambaye hapa anaelezea hatua kwa hatua.

“Tumefanya vizuri sana kwenye Uviko-19, kwanza ni kuipongeza Serikali kwa sababu ilikuwa tayari tulivyobadili msimamo kutoka kutohitaji chanjo mpaka tunazihitaji na Rais Samia Suluhu Hassan aliridhia.

Akizungumza jana Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo, Dk Florian Tinuga alisema Wizara ya Afya imekua ikiratibu upatikanaji wa chanjo dhidi ya Uviko-19 kupitia COVAX na misaada kutoka nchi rafiki.

“Hadi kufikia Machi, 2023 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokewa ambapo dozi 41,815,470 sawa na asilimia 89 ya dozi zote zilizopokelewa zilikuwa zimesambazwa nchi nzima, na dozi zilizotumika hadi sasa ni 38,598,718,” alisema.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal

Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.

The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading