Tanzania: Ujumbe wa Dk Mpango wa Krismasi huu hapa…

Tanzania: Ujumbe wa Dk Mpango wa Krismasi huu hapa…

Dar es Salaam, Tanzania:

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewasihi Wakristo na Watanzania kutoa heshima ya pekee kwa watoto kwa kuwa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.

Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango amewasihi Wakristo na Watanzania kutoa heshima ya pekee kwa watoto kwa kuwa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.

Dk Mpango amesema sasa hivi katika nchi yanasikika mambo ya hovyo na dhuluma dhidi ya watoto ikiwemo watoto kunyanyaswa, kuuwawa na kulawitiwa.

“Tumuombe Mungu msamaha na atujalie neema ya kutambua jinsi yeye alivyowapenda watoto na sisi tufanye mengi ya kuwatunza hawa watoto na kumrudishia Mungu wakiwa weupe kama tunavyoweka ishara ya kitambaa cheupe kumrudishia Mungu,’amesema Makamu huyo wa Rais.

Katika hatua nyingine, Dk Mpango amewataka waamini hao kumshangilia Mungu kwa mvua aliyoileta na kueleza kuwa sehemu nyingine kumekuwa na hali ngumu ya ukame iliyosababisha mifugo kuanza kufa.

“Sasa Mwenyezi Mungu ametuletea neema ya mvua tuitumie vizuri, tulime mazao yetu sasa, tupande ili tuweze kupata chakula.

“Vilevile kila familia tutumie nafasi kupanda miti, tupande miti ya matunda, tupande miti ya kivuli, kila familia walau miti mitatu, miti miwili ya matunda na mmoja kwa ajili ya kivuli kwani nchi yetu imeharibika sana,”amesema.

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories