Tanzania kunufaika uwekezaji teknolojia ya fedha

Tanzania kunufaika uwekezaji teknolojia ya fedha

Dar es Salaam. Tanzania inatarajiwa kuwa miongoni mwa mataifa yatakayonufaika na uwekezaji wa teknolijia ya fedha (FinTech), baada ya wawekezaji 10 kutoka Afrika na Marekani kutua nchini.

Wawekezaji hao wanatarajiwa kutua kwenye kongamano la wadau wa sekta hiyo lililopangwa kufanyika hapa nchini kati ya Septemba 12 hadi 13, 2024 ambapo kwa jumla wadau zaidi ya 300 watakutana.

Kongamano hilo limelenga kuleta chachu na kuongeza wawekezaji, hasa katika teknolojia ya fedha hapa nchini na Afrika kiujumla kama anavyosema Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Fintech Association (Tafina), Reuben Mwatosya alipokuwa na mkutano na waandishi wa habari jana Septemba 4, 2024 jijini Dar es Salaam.

“Kongamano hili litakwenda kuibua majadiliano baina ya wawekezaji na wawakilishi wa nchi mbalimbali zitakazohudhuria siku hiyo, ikiwa na lengo la mapinduzi ya kiteknolojia za pande zote,” amesema Mwantosya.

Aidha, kongamano hilo linatarajiwa kuwa mwanzo wa makongamano mengine na kujenga fursa kuwaleta wadau kutoka sekta mbalimbali kujadiliana na kuongea masuala ya kiteknolojia na namna gani waikuze kuendana na dunia ya sasa.

Katibu Mkuu wa Tafina, Shadrack Kamenya amesema katika kongamano hilo kutakuwa na midahalo iliyogawanyika katika aina tatu ambazo ni kiuwekezaji, kisera na ushirikiano baina ya watoa huduma.

“Kutakuwa na maonyesho ya teknolojia na namna wanavyozitoa huduma zao na pia ni eneo mahususi kwa serekali na wadau wengine kuona ni kitu gani kinafanyika duniani na kurahisisha maendeleo hasa katika sekta ya fedha hapa nchini,” amesema.

Miongoni mwa maazimio ya siku hiyo amesema ni kurahisisha mchakato wa ujumuishaji wa kifedha na urejeshaji fedha ambayo yote msingi wake ni uwezeshajiwa teknolojia ya Fintech.

Amesema kongamano hilo pia limelenga kuwakutanisha wasomi kutoka mataifa mbalimbali watakaobadilishana uzoefu kwaajili ya huduma endelevu za kifedha.

Teknolojia ya kifedha (FinTech) inashika nafasi za juu zaidi duniani katika zile teknolojia zinazokuwa kwa kasi na kuwa na matumizi mengi zaidi duniani, huku ikitanguliwa na taknolojia ya kimtandao.

Teknolojia nyingine zinazotarajiwa ni zile za matumizi ya akili bandia (AI).

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Insecurity prompts Zanzibar to review its lucrative island leasing

The Tanzanian central government is planning to boost its security presence in the Zanzibar archipelago. A commission tasked with auditing the country’s security forces was appointed in July by President Samia Suluhu Hassan. It says it is concerned about the situation in the country’s Indian Ocean islands that are under the control of the semi-autonomous Zanzibar local government.Continue Reading