Tanzania, Comoro kuimarisha ushirikiano maeneo manne

Tanzania, Comoro kuimarisha ushirikiano maeneo manne

Comoro. Tanzania na Visiwa vya Comoro zimesaini Hati nne za makubaliano kwenye kilele cha mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Comoro uliofanyika Julai 24, 2024 jijini Dar es Salaam.

Hati zilizosainiwa katika kikao hicho zinazojumuisha nyanja za ushirikiano wa kidiplomasia, afya, biashara na viwanda pamoja na teknolojia ya habari.

Utiaji saini hati hizo umeshuhudiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje wa Comoro anayeshughulikia nchi za Kiarabu, nchi zinazozungumza Kifaransa, diaspora na utangamano wa Afrika, Mohamed Mbae.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa kihistoria, Waziri Tax ameelezea umuhimu wa kusainiwa kwa hati hizo kuwa itawezesha pande hizo mbili kuwa na ushirikiano ulio katika mpangilio mzuri katika nyanja husika na hivyo kuleta tija zaidi.

“Pamoja na kutia saini hati za Makubaliano pia tumekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo mengine mengi ikiwemo miondombinu, nishati, ulinzi na usalama, uchumi wa buluu, utalii, utamaduni, sanaa na michezo na maendeleo ya vijana,” ameeleza Dk Tax.

Mbae ameeleza kufurahishwa na kufanyika kwa mkutano huo wa JPC na kuongeza kuwa umekuwa kiungo muhimu katika kuendelea kukuza na kuimarisha uhusiano na kati ya Tanzania na Comoro.

Ameipongeza Tanzania kwa kuandaa mkutano huo na hivyo kuonesha dhamira ya dhati yake katika kuendelea kushirikiana na Comoro.

Mbali na kusainiwa kwa hati hizo, mawaziri hao wameridhishwa na kupongeza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa makubaliano na maamuzi mbalimbali yaliyofikiwa kwa pamoja kati ya pande hizo mbili tangu kusainiwa kwa mkataba wa jumla wa ushirikiano mwaka 2009.

Vilevile mkutano huo umejadili na kuweka mikakati ya namna ya kuendelea kukuza biashara baina ya pande hizo mbili.

Mikakati hiyo pamoja na mambo mengine italenga kuwahimiza sekta binafsi kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili. Pia kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo na zile zinazotokana na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) na eneo huria la biashara la SADC.

Akizungumza kuhusu mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu ameeleza kuwa, Comoro ni mshirika muhimu wa Tanzania katika biashara, ambapo kwa mwaka 2023 Tanzania iliuza nchini humo bidhaa zenye thamani ya Sh148 bilioni.

Ameongeza kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo sio tu yataongeza ushirikiano wa kidiplomasia bali yanatarajiwa kuongeza kiasi cha bidhaa ambazo Tanzania inaingiza nchini humo.

Katika mkutano huo ujumbe wa Tanzania umejumuisha wataalamu na watendaji kutoka sekta mbalimbali na umeongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, Dk Stergomena Tax, ambaye pia aliongoza mkutano huo kwa kushirikiana na mwenyekiti mwenza Waziri Mbae wa Comoro.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income

Insurer and financial services provider Britam posted a 22.5 percent jump in net earnings for the half-year ended June 2024, to Sh2 billion, buoyed by increased investment income.

The rise in half-year net profit from Sh1.64 billion posted in a similar period last year came on the back of net investment income rising 2.5 times to Sh13.27 billion from Sh5.3 billion.

“We are confident in the growth and performance trend that Britam has achieved, supported by its subsidiaries in Kenya and the region. Our business is expanding its revenue base while effectively managing costs,” Britam Chief Executive Officer Tom Gitogo said.

“Our customer-centric approach is fueling growth in our customer base and product uptake, particularly through micro-insurance, partnerships, and digital channels.”

The investment income growth was fueled by interest and dividend income rising 34 percent to Sh9.1 billion, which the insurer attributed to growth in revenue and the gains from the realignment of the group’s investment portfolio.

Britam also booked a Sh3.79 billion gain on financial assets at a fair value, compared with a Sh1.8 billion loss posted in a similar period last year.

The increased investment income helped offset the 12.7 percent decline in net insurance service result to Sh2.13 billion in the wake of claims paid out rising at a faster pace than that of premiums received.

Britam said insurance revenue, which is money from written premiums, increased to Sh17.8 billion from Sh16.6 billion, primarily driven by growth in the Kenya insurance business and regional general insurance businesses, which contributed 30 percent of the revenue.

The group has a presence in seven countries in Africa namely Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, South Sudan, Mozambique, and Malawi.

Britam’s insurance service expense hit Sh13.6 billion from Sh11.3 billion, while net insurance finance expenses rose 2.6 times to Sh12.3 billion during the same period.

“Net insurance finance expenses increased mainly due to growth in interest cost for the deposit administration business driven by better investment performance. This has also been impacted by a decline in the yield curve, which has led to an increase in the insurance contract liabilities. The increase has been offset by a matching increase in fair value gain on assets,” said Britam.

Britam’s growth in profit is in line with that of other Nairobi Securities Exchange-listed insurers, which have seen a rise in profits.

Jubilee Holdings net profit in the six months increased by 22.7 percent to Sh2.5 billion on increased income from insurance, helping the insurer maintain Sh2 per share interim dividend.

CIC Insurance Group posted a 0.64 percent rise in net profit to Sh709.99 million in the same period as net earnings of Liberty Kenya nearly tripled to Sh632 million from Sh213 million, while Sanlam Kenya emerged from a loss to post a Sh282.2 million net profit.

Continue Reading