Taarifa ya awali ripoti ya ajali ya ndege Ziwa Victoria

Taarifa ya awali ripoti ya ajali ya ndege Ziwa Victoria

Taarifa ya awali ripoti ya ajali ya ndege Ziwa Victoria: ‘Vikosi vya uokoaji vingefika haraka, watu wengi wangetoka hai’’

  • Taarifa ya awali ya ripoti ya ajali ya ndege ya shirika la precision iliyotokea katika eneo la Ziwa Victoria Tanzania, imetolewa na wizara ya usafirishaji nchini Tanzania, na kuonesha kuwa vikosi vya uokoaji vilichelewa kufika katika eneo la tukio.

    Ajali hiyo ilitokea majira ya saa 2 asubuhi saa za Tanzania, lakini kwa mujibu wa ripoti hiyo inaeleza kuwa boti ya kitengo cha polisi wa majini, ilifika majira ya saa saba saa za Tanzania.

    ‘’ Boti ilifika saa saba eneo la tukio, baada ya kufika walikua na changamoto ya kuishiwa mafuta na oksijeni, kabla hawajafika, mvuvi mmoja tayari alianza kutoka maiti zilokua ndani ya ndege’’ taarifa ya ripoti inasema

    Taarifa ya ripoti hiyo pia haijatoa sababu kamili ya nini kilisababisha kutokea kwa ajali, ikisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

    Mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania awali ilibainisha kuwa baada ya ripoti ya awali itafuatia ripoti ya uchunguzi wa awali inayotarajiwa kuchapishwa mwezi mmoja baada ya ajali na kisha ripoti kamili baada ya mwaka mmoja.

    Ndege hiyo ya shirika la precision ATR 42-500 yenye namba PW 494 ilianguka kwenye ziwa Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua ikitokea jijini Dar es Salaam kupitia Mwanza. Ajali hiyo imeua watu 19 kati ya 43 waliokuwemo akiwemo rubani na msaidizi wake.

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories