Shirika la Umeme Zanzibar ZECO likitumbuiza
Utendaji kazi katika Shirika la Umeme umeporomoka kwa kiwango kikubwa huku wananchi wakilalamikia huduma zisizoridhisha.
Habari kutoka ZECO zinasema kuwa wateja wanaoomba kufungiwa mita katika mitaa yao wanasuburi kwa muda mrefu wengine miezi miwili, mitatu hadi sita.
Mbali na mita, huduma nyengine ambazo wananchi wanalalamikia ni pamoja na matengenezo ya dharura pale panapotokea hililafu, mafundi wa ZECO inawachukua muda mkubwa kurekebisha.
Habari zaidi kutoka shirika hilo zinasema kuwa kumekuwa na makundi yanayotishia ufanisi wa kazi huku wafanyakazi hasa wa ngazi ya chini wakilalamikia maslahi duni wanayopata na kuchelewa kushughulikia kwa madai yao mbalimbali.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar na kiongozi wa wafanyabiashara wa serikali katika Baraza hilo mwezi Disemba alisema kuwa serikali inafanya juhudi kuhakikisha kunakuwepo na fursa sawa katika kutoa huduma za umma.
Hivi karibuni, serikali ya Zanzibar ilipunguza gharama za kuunganishiwa umeme, mpango ambao ulikuwa na lengo mahususi kuweka mazingira ya wateja kupata huduma ya umeme.
“Serikali imepunguza gharama za umeme kwa wananchi wake. Sasa ni jukumu la Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kuhakikisha wananchi wanaohitaji umeme wanaunganishwa mara baada ya kufanya malipo. Kusiwe na ucheleweshaji usio wa lazima,” alisema na kuwataka wafanyakazi kuachana na rushwa, wizi na urasimu, badala yake wafanye kazi kwa uadilifu,” Hemed Suleiman Abdulla alisema.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya ZECO Gulioni ambapo hakuridhishwa na haki ya utendaji kazi.
Katika ziara yake hiyo, Makamu wa Pili wa Rais alionekana kama vile hakuridhishwa na uendeshaji hatua ambayo inapelekea kuonesha kushindwa kujiendesha ipasavyo.
Akizungumzia suala la uungwaji umeme kwa wananchi, Makamu wa Pili wa Rais alisema kuna zaidi ya watu 3000 wanasubiri kuunganishiwa umeme.
Ametoa muda wa Mwezi Mmoja Wananchi hao wawe tayari wameunganishiwa huduma hiyo.
Amesema suala la ucheleweshaji kuungiwa umeme wananchi hao inaonesha wazi uwepo wa mianya ya Rushwa kwa watendaji na kueleza kuwa Serikali haitamvumilia mtendaji yoyote atakaejaribu kujihusisha na aina yoyote ya Rushwa.
Pamoja na hayo Mhe. Hemed ameonesha kutoridhishwa na masuala ya kifedha hasa ukusanyaji na kuwataka kuziba mianya iliyokuwepo ili kudhibiti ukusanyaji huo na kuongeza pato la Taifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameushauri Uongozi wa Shirika la Umeme Zanzibar kuandaa Mfumo mzuri wa Malipo mfumo ambao utapelekea kuwajua wenye madeni.
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Zanzibar Airport Authority to audit ground handlers
Unguja. The Zanzibar Airports Authority (ZAA) is set to conduct an audit on ground handling companies that currently operate at the Abeid Amani Karume Airport with effect from Monday. The week-long audit is set to include Transworld, ZAT and the newcomer Dnata Zanzibar who were licensed in June plus exclusive rights to manage Terminal 3 building by ZAA.Continue Reading
ACT Unaware of Mwinyi’s joint committee on Zanzibar reforms
Opposition party ACT Wazalendo has said it is not aware of a special committee on reforms and has directed the party’s leadership to follow up on the decision of the Central Committee which directed its leaders to meet with President Hussein Ali Mwinyi.Continue Reading
High Court rejects Transworld’s application
The High Court in Dar es Salaam has struck out an application in which Transworld Aviation, a ground handler at the Abeid Aman Karume International Airport (AAKIA) was seeking permission to sue the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).Continue Reading