Sh350 milioni zakusanywa CRDB Bank Marathon, Dk Biteko atoa ujumbe

Sh350 milioni zakusanywa CRDB Bank Marathon, Dk Biteko atoa ujumbe

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko ameipongeza taasisi ya CRDB Bank Foundation kwa kuendelea kuandaa mbio za CRDB Bank Marathon ambazo zimejielekeza kusaidia jitihada za Serikali kuboresha sekta ya afya, kusaidia wenye uhitaji pamoja na kukuza ustawi wa jamii.

Dk Biteko ametoa pongezi hizo wakati wa kilele cha msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon ambazo zimekusanya Sh350 milioni kwa ajili ya kusaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI), huduma za afya kwa wakinamama wenye ujauzito hatarishi Hospitali ya CCBRT na uwezeshaji wa vijana.

“Niwapongeze kwa kuendelea kusaidia matibabu ya kinamama na watoto wetu. Kinamama ndio wamebeba uchumi wa Taifa letu, pia ndio waangalizi wa familia zetu hususan watoto,” amesema.

Amesema ukiimarisha afya ya mama na mtoto umeimarisha afya ya Taifa.

Akizungumzia mbio hizo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro amesema imesaidia kuchochea ari ya michezo nchini.

Amesema zimekuwa jukwaa muhimu kwa wanariadha nchini kuonyesha vipaji vyao katika jukwaa la kimataifa, kwani mbio hizo zimesajiliwa kimataifa na Shirikisho la Upimaji Mbio Kimataifa (AIMS) na Shirikisho la Riadha Duniani (World Athletic).

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema katika fedha kilichokusanywa, Sh100 milioni zitasaidia watoto wenye uhitaji wa upasuaji wa moyo JKCI.

Amesema kitita kingine kama hicho kitasaidia huduma za afya kwa kinamama wenye ujauzito hatarishi waliopo Hospitali ya CCBRT na Sh150 milioni zitasaidia uwezeshwaji kwa vijana.

Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB Bank Foundation, Martin Warioba amesema mbio hizo zimeshirikisha wanamichezo zaidi ya 8,000.

Amesema washindi wamezawadiwa Sh98.7 milioni katika mbio za kilomita 42, 21, 10 na kilomita 5, pamoja na wa mbio za baiskeli za kilomita 65.

Amesema lengo lao mwakani ni kupata washiriki 10,000 wa Tanzania, huku malengo ya washiriki wa Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) yakiwa ni 3,000 kila nchi.

Katika mbio hizo, Joyloyce Kemuma alishinda kwa wanawake wakati kwa wanaume, Moses Nengichi alishinda wote kutoka Kenya.

Katika mbio ya Kilomita 21 upande wa wanawake ni Sara Ramadhan na Joseph Panga wote Watanzania.

Kwenye kilomita 10, Hamida Nasoro wa aliibuka mshindi na kwa upande wa wanaume, Mao Hindo Ako alishinda ambapo wote ni Watanzania.

Kwenye mbio za baiskeli, Paul Lumoria alishinda na kufuatiwa na Richard Laizer na Joseph Thuku ambapo kwa upande wa wanawake mshindi alikuwa Jamila Abdallah na kufuatiwa na Monica Jelimo na Julia Miringu.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Top News
Investment News Editor

ZSSF money not for projects, says Ali Karume

Unguja. Veteran politician and diplomat Ali Karume has called on authorities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) to refrain from using the Zanzibar Social Security Fund money for establishing commercial projects.Continue Reading