Sh26 bilioni za Aga Khan, AFD kupambana na saratani Tanzania, Kenya

Sh26 bilioni za Aga Khan, AFD kupambana na saratani Tanzania, Kenya

Sh26 bilioni za Aga Khan, AFD kupambana na saratani Tanzania, Kenya

Dar es Salaam. Serikali ya Ufaransa imeingia makubaliano na Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan ya miaka minne ya kutoa huduma ya chanjo ya saratani ya kizazi sambamba na matibabu ya saratani ya matiti kwa wanawake 800,000 Tanzania.

Mradi huo ambao pia utainufaisha nchi ya Kenya, Tanzania pekee wasichana 200,000 wenye miaka tisa watapatiwa huduma ya chanjo ya kuwakinga na saratani ya mlango wa kizazi (HPV) na wasichana 600,000 nchini Kenya wenye miaka 10 hadi 14.

Pia, wanawake 400,000 wa Tanzania watafanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti kupitia mradi huo, lengo la mradi mzima ni kutoa elimu ya saratani kwa watu milioni 7.4.

Akizungumza baada ya kuingia makubaliano hayo leo Jumanne Januari 28, 2025 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Huduma za Afya Aga Khan, Dk Zeenat Sulaiman Khan amesema mradi huo utainufaisha mikoa sita ya Tanzania.

Ameitaja mikoa hiyo ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro na Zanzibar huku akitaja pia kaunti nne za Kenya ambazo ni Mombasa, Kisumu, Kilifi na Homa bay.

Dk Zeenat amesema sababu ya mradi huo kuelekezwa katika mikoa sita ni baada ya utafiti kufanyika na kuonekana mikoa hiyo inachangamoto na pia ni kutokana na kipaumbele cha Serikali.

“Tunashirikiana kwa karibu na Serikali ya Ufaransa na msaada wao umekuwa muhimu sana kwa miaka mingi, mradi huu utaleta maendeleo katika matibabu ya saratani,” amesema Mkurugenzi mtendaji huyo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Anne Sophie Av’e amesema ni hatua nzuri kuanzisha ushirikiano na Taasisi ya Aga Khan, akisisitiza ushirikiano huo utakuwa mfano wa namna taasisi za kimataifa zinavyoshirikiana kuchochea maendeleo kwenye sekta ya afya.

“Kwa kujumuisha uwezo wetu kama Serikali ya Ufaransa na uzoefu wa wataalamu kutoka taasisi za Tanzania, hatuendi tu kujenga mfumo imara wa sekta ya afya, tunakwenda kuimarisha uhusiano wetu na kujifunza zaidi,” amesema Balozi Anne Sophie Av’e.

Amesema mwanamke anapopatwa na maradhi athari yake ni kubwa kuanzia ngazi ya familia hadi jamii, hivyo kuimarisha afya ya mwanamke ni kujenga jamii iliyobora.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo Ufaransa (AFD), Remy Rioux amesema kwa zaidi ya miaka 15 wanafanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania hususan zile za kusaidia maendeleo kwa Watanzania.

Ameyataja maeneo yanayonufaika na AFD kwa Tanzania ni pamoja na sekta maji, nishati, usafirishaji na afya.

“Tunajivunia sasa afya ni mali ya umma, tunajivunia kushirikiana na Aga Khan na kituo maarufu cha saratani cha ufaransa Institut Curie katika uzinduzi wa mradi huu wa saratani ya wanawake Africa Mashariki (EA-CWCP) kwamba unakwenda kuleta kwa wanawake wanaokumbana na changamoto ya maradhi haya,” amesema Rioux.

Awali, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Seif Shekalaghe amesema utekelezaji wa mradi huo unaendana na azma ya Serikali ya kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza akidokeza mradi huo utasaidia udhibiti wa saratani nchini.

Dk Shekalaghe amesema mradi huo unapaswa kuwajengea uwezo wataalamu wa afya kuanzia ngazi ya wilaya na siyo ngazi ya Taifa pekee, kwa sababu wagonjwa wengi wanafika Hospitali tayari ugonjwa umesambaa maeneo mengi mwilini.

“Wagonjwa wengi wanaofika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) ugonjwa unakuwa ymeshafika hatua za juu zaidi, wataalamu wa ngazi ya wilaya wakijengewa uwezo, watatambua ugonjwa katika hatua za awali,” amesema Dk Shekalaghe.

Amesisitiza utekelezaji wa mradi huo uambatane na utoaji wa elimu kwa wananchi dhidi ya dalili za awali za saratani.

Amesema lengo ni watu wachukue hatua mapema kwenda hospitali, lakini bila elimu, ugonjwa huo utazidi kuongezeka.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Aga Khan, idadi ya wagonjwa wa saratani nchini Kenya na Tanzania inaongezeka, na kwa sasa kesi mpya takribani  100,000 na vifo 60,000 hutokea kila mwaka.

“Changamoto hii ni kubwa zaidi kwa wanawake, ambao ni asilimia 61 ya kesi za saratani Afrika Mashariki. Hivyo ujio wa mradi huo unategemewa kuwanufaisha  takribani watu milioni 7.4 Tanzania na Kenya, na mradi mzima utagharimu Euro 10 milioni (takriban Sh27 bilioni,)” amesema Dk Shekalaghe.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

EXIM Bank to raise 300m/- over the next three years for financing essential services and infrastructure upgrades in mental health facilities.

The bank’s Head of Marketing and Communications Stanley Kafu unveiled this when introducing Exim Bima Festival 2024 as a platform for bringing together individuals, organisations and various sectors for raising the funds.

“Exim’s initiative aligns with the government’s broader goals to ensure that every citizen has access to quality healthcare, including mental health services,” he said.

The initiative, which is one of the events for celebrating the bank’s 27th anniversary is scheduled for Wednesday this week in Dar es Salaam.

Mr Kafu highlights that this year’s festival is not only about raising awareness of the importance of insurance in the society but also focuses on enhancing access to mental health services and improving the overall well-being of the nation.

Statistics from the Ministry of Health shows a staggering 82 per cent increase in mental health cases over the past decade.

Mental cases have risen from 386,358 in 2012 to 2,102,726 in 2021, making the need for mental health services more urgent than ever.

ALSO READ: NBC’s Saving Campaign Empowers Customers Nationwide

Unfortunately, the country’s ability to address this growing challenge is hindered by a shortage of mental health professionals, infrastructure, medical equipment and essential medication.

For example, out of the 28 regions in the country, only five have facilities that provide adequate mental health services.

The most affected group is the youth aged 15 to 39, who represent the nation’s workforce, underscoring the need for intensified efforts to safeguard this generation for Tanzania’s future well-being and development.

Mr Kafu said by improving mental health services, Exim aims to contribute to the creation of a network of communities that can access care quickly and affordably.

Exim Insurance Department Manager Tike Mwakyoma said they are appreciating the support from partners in the insurance industry, who have stood by them since the last festival.

“Let’s continue this unity for the development of all Tanzanians and our nation as a whole,” the manager said.

Source: allafrica.com

Continue Reading