Serikali yajitenga na ripoti ya awali ya ajali ya ndege Bukoba
Serikali ya Tanzania imekanusha kutoa ripoti ya awali juu ya ajali ya ndege ya Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria Novemba sita na kuua watu 19, akiwemo rubani na msaidizi wake.
Ripoti inayokanushwa imesambaa mitandaoni toka Jumanne na kuripotiwa na vyombo mbali mbali vya ndani na nje ya Tanzania, na BBC News.
Serikali ya Tanzania sasa kupitia msemaji wake Gerson Msigwa inasema ripoti rasmi itatolewa itakapokuwa tayari na umma utataarifiwa.
Hata hivyo majibu hayo ya Msigwa yameibua mjadala na kupingwa na baadhi ya watu akiwemo Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo.
Zitto aliandika kupitia mtandao wa twitter, akisema yuko tayari kupelekwa Mahakamani kama taarifa ya ripoti hiyo ya awali ni ya uongo.
Social embed from twitter
Ndege hiyo ya ATR 42-500 yenye namba PW 494 iliyokuwa na watu 43 ilianguka kwenye ziwa Victoria mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba, ikijiandaa kutua ikitokea jijini Dar es Salaam kupitia Mwanza. Watu 24 walinusurika katika ajali hiyo.
Tangu kutokea kwa ajali hiyo, mjadala umekuwa nani aliyeokoa watu hao 24, baada ya taarifa kinzani zikimtaja Majaliwa Jackson mkazi wa Nyamkazi, Bukoba kama shujaa na nyingine zikitaja muhudumu wa ndege na abiria ndio waliofungua mlango wa ndege kuokoa watu.
Serikali pia imekuwa ikinyooshewa kidole kwa kinachotajwa uzembe uliosababisha vifo vya waliokuwemo, huku ripoti kamili ikisubiriwa kwa hamu.
James Mbatia, alipozungumza na BBC baada ya ajali hiyo, alishangazwa kutumika kwa teknolojia dunia ya uokoaji, licha ya kukua kwa teknolojia ulinganisha na miaka 26 iliyopita ilipotokea ajali kubwa ya meli ya MV Bukoba, akigusia teknolojia ya kutumia kamba kuivuta ndege kutoka kwenye ziwa.
‘Yaani unavuta ndege kana kwamba ndoano unavua samaki kwenye bahari, ni jambo la fedheha sana’ alisema Mbatia na kuongeza ‘wale wavuvi wao ndio wanafanya kazi hiyo (uokoaji) wakati vikosi vipo , hakujawa na utashi wa kisiasa wa kufanya kazi hiyo’.
Waziri Bashungwa, akizungumza kwenye uwanja wa Kaitaba wakati wa kuaga miili ya watu 19 waliofariki kwenye ajali hiyo alihaidi kwamba serikali imesikia na itafanyia kazi maoni ya wananchi ya kuboresha vifaa vya uokoaji.
‘Katika janga hili lenye majonzi makubwa pia tumepokea maoni ya wananchi ya namna tunavyohitaji kujipanga vyema zaidi katika kuboresha mifumo ya uokoaji na kwa serikali hii sikivu inayoongozwa na rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na tunakwenda kuyafanyia kazi’, alisema Bashungwa.
Habari Asili za BBC za Ripoti ya Awali (20 November 2022)
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Villagers on Pemba Island lack clean sanitized water
Eight villages on Pemba Island have lacked clean and safe water service while complaining to the Zanzibar Water Authority for failing to solve the water problem in their villages.Continue Reading
Rare megamouth shark found in Zanzibar for the first time – why so little is known about it
The recent sighting was only the sixth time a megamouth had ever been found off the coast of Africa.Continue Reading
Fast Satellite Internet in Kenya by June
Elon Musk’s satellite Internet firm Starlink announced it will launch in Kenya in the second quarter of this year.Continue Reading