Dar es Salaam, Tanzania
Januari 27, KLM iliorodhesha Kenya na Tanzania kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na tovuti rasmi kama nchi zinazokumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.
Serikali imeeleza kusikitishwa na taarifa iliyotolewa na shirika la ndege la Uholanzi (KLM) ya kuwepo kwa hali ya hatari nchini na kusitisha safari zake zilizopangwa kufanyika Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Katika taarifa iliyotolewa katika tovuti ya KLM Januari 27, shirika hilo limewatahadharisha abiria wake na kueleza kusitisha safari katika viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA).
Taarifa iliyotolewa leo Januari 28, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekanusha taarifa hizo akisema hazina msingi.
“Taarifa hii haina msingi, haina mashiko, haijali na haina umuhimu na imesababisha hofu isiyo na sababu na kiwewe kwa wananchi na sekta ya anga kwa ujumla. Umma unaaswa kuipuuza hiyo taarifa,” imesema taarifa hiyo.
Imeendelea, “Wizara inapenda kuufahamisha umma na jumuiya ya kimataifa kuwa, operesheni katika viwanja vya JNIA na KIA zinaendelea. Januari 27, 2023 katika uwanja wa JNIA, ratiba za ndege 17 kati ya 18 zikiwa na abiria 2,545 zimefanuika wakati katika uwanja wa ndege wa KIA, ndege tano zikiwa na abiria 823 zimjefanikisha safari zake4.
“Hadi leo saa 9:15 alasiri leo, safari za ndege za kimataifa 12 zimefanyika.”
Source: mwananchi.co.tz
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Zanzibar tourism investors alarmed by new mandatory insurance fee
Tourism investors in Zanzibar have voiced their concerns over the introduction of mandatory travel insurance, cautioning about its potential negative impact on the industry.Continue Reading
Huduma Zimezorota Hospitali Ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar
Huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja Zanzibar zimezidi kuzorota huku wananchi wengi wakilalamikia uongozi wa Hospitali hiyo na watendaji wake.Continue Reading
Will Tanzania agree to Starlink Internet Service?
Will the Tanzania government let Starlink, the world-famous internet service provider, operate in the country?Continue Reading