Serikali, wadau kuwapa wanawake ujuzi wa teknolojia

Serikali, wadau kuwapa wanawake ujuzi wa teknolojia

Dar es Salaam. Katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika matumizi ya teknolojia, Serikali imeweka mkakati wa kushirikiana na wadau kutoa elimu ili kufikia usawa wa kijinsia katika uga huo.

Hayo yamesemwa leo Juni 3 jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu, Dk Dorothy Gwajima katika hafla ya ugawaji wa kompyuta mpakato kwa mabinti wanufaika wa mradi wa ‘Binti Digital.’

Amesema Tanzania pia imekuwa na sera mahususi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na masuala mbalimbali ikiwamo yale yanahusu sayansi na teknolojia.

“Juhudi hizi zimesababisha ongezeko kubwa la uandikishwaji wa wasichana shuleni katika miaka ya hivi karibuni, jambo ambalo ni muhimu katika kufikia usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana.”

Pia, amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya mawasiliano katika maeneo mbalimbali nchini.

Amesema teknolojia ni muhimu katika kukuza uchumi, ubunifu na kuboresha maendeleo ya jamii na Tanzania kama ilivyo nchi nyingine inashuhudia mapinduzi ya kidijitali yanayotoa fursa kwa wanawake na wanaume katika nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Hata hivyo, ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa vijana hasa mabinti waliopata mafunzo hayo ya teknolojia kutumia fursa zinazopatika kutokana na ukuaji wa teknolojia katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Mwakilishi Mkazi wa UN Women, Peterson Magoola amesema ili kufikia usawa wa kijinsia katika masuala ya teknolojia, wameanzisha programu mbalimbali ikiwamo ya ‘Binti Dijital’ ambayo imelenga kuwawezesha mabinti wenye umri kati ya miaka 17 hadi 25 kwa kuwapatia mafunzo yatakayowawezesha kufanya ubunifu katika masuala ya teknolojia.

Amesema kwa mwaka 2023 programu hiyo iliwafikia mabinti zaidi ya 100 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

“Baadhi yao baada ya kupata mafunzo wamejiajiri, kuajiriwa na hata kuja na bunifu wa aina mbalimbali,”

Ameongeza kuwa mradi huo utafanyika tena kwa awamu nyingine na sasa unatarajiwa kuwanufaisha mabinti waliopo katika maeneo ya vijijini.

Mtaalamu wa kuwawezesha wanawake kiuchumi kutoka UN-Women, Lilian Mwamdanga amesema utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa asilimia 90 ya kazi zote zinahitaji kuwa na maarifa kuhusu masuala ya teknolojia, hivyo uwepo wa mafunzo hayo yatasaidia kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake.

Mkuu wa Idara ya Uhusiano katika balozi wa Ubelgij hapa nchini, Fanny Heyler amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwa na kuimarika hapa nchini.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

Monrovia — The Director General of the African Centers for Disease Control, Jean Kaseya, has said the center stands ready to support Tanzania and other countries in the region where suspected cases of the infectious Marburg Virus Disease have been identified. The World Health Organization earlier this week issued an alert warning of a possible outbreak in the country, although the Tanzanian Health Ministry has said tests conducted on available samples did not show the existence of Marburg in the East African nation.

“As of the 15 of January 2025, laboratory results from all suspected individuals were negative for Marburg Virus,” Tanzanian Health Minister Jenista Mhagama said in a statement. This would have marked the country’s second experience with the highly infectious disease that recently killed over a dozen people in neighboring Rwanda. Tanzania previously reported an outbreak of Marburg in 2023 in the  Kegara region, said to have been the epicenter of the new suspected cases.

At the Africa CDC online briefing on Thursday, Kaseya also said another infectious disease, Mpox, “remains a public health concern”. He said that while in December 2024, the disease had afflicted 20 countries, a new country – Sierra Leone – has been added to the number after recent outbreak there. Sierra Leonean health authorities said on January 10 that two cases of Mpox had been confirmed in the country and dozens of contacts are being traced.

With thousands of confirmed cases of Mpox across Africa and more than 1000 people having died of the disease  – mainly in Central Africa – Kaseya emphasized the need to increase testing, a theme he’s heralded before. The Africa CDC boss said over the next few months the continental health watchdog will deploy additional epidemiologists and community health workers to areas considered hot spots of infectious diseases in the region.

Source: allafrica.com

Continue Reading

High Court rejects Transworld’s application
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

High Court rejects Transworld’s application

The High Court in Dar es Salaam has struck out an application in which Transworld Aviation, a ground handler at the Abeid Aman Karume International Airport (AAKIA) was seeking permission to sue the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).Continue Reading