Serikali: Fedha zinazotumika kukarabati viwanja vya CCM zitarudi kwa umma

Serikali: Fedha zinazotumika kukarabati viwanja vya CCM zitarudi kwa umma

Dodoma. Serikali ya Tanzania imewaondoa hofu Watanzania kuwa fedha zitakazotumika kukarabati viwanja vya michezo vinavyomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) zitarejeshwa kwa umma, ili zitumike kufanya mambo mengine.

Katika hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya aliyekuwa Wazira ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, aliomba Bunge kuwaidhinishia Sh10 bilioni katika mwaka 2022/23 kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vitano vya CCM.

Viwanja hivyo ni Jamhuri (Dodoma), Shekh Amri Abeid (Arusha), Sokoine (Mbeya), CCM Kirumba (Mwanza) na Mkwakwani (Tanga) pamoja na Benjamin Mkapa (Dar es Salaam) ambacho hakimilikiwi na CCM.

Kauli hiyo ya kurejesha fedha hizo imetolewa leo Jumatatu Juni 10, 2024 bungeni na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee.

Mdee amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa ni wa umma, kwa hiyo ni sahihi kwa fedha za umma kutumika katika kukarabati, lakini uwanja wa Kirumba ni wa CCM hivyo si sahihi kuukarabati kwa fedha za umma.

“Ni namna gani hizi fedha za umma zitakazotumika kukarabati huu uwanja wa CCM zitarudishwa, ili zifanye kazi nyingine za umma,” amehoji.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema kinachofanyika ni majadiliano ya namna ambavyo watavikarabati viwanja na namna ya kuviendesha pia.

“Hata mapato yatakayokuwa yanatoka katika viwanja hivi maana yake yatakuwa yanatumika kurejesha fedha ambazo zimetumika kuvikarabati.

“Kwa hiyo nimtoe wasiwasi mheshimiwa mbunge kuwa tunachokwenda kukifanya ni kwenda kuhudumia umma uleule ambao utavitumia viwanja hivi, lakini pia fedha zitakazopatikana zitarudi katika kufanyia shughuli nyingine za umma,” amesema.

Naye Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya amehoji Serikali ina mpango gani wa kushawishi timu za Simba na Yanga kucheza michezo ya kuchangisha fedha kusaidia wilaya zenye mapato duni kujenga viwanja vya michezo, ili kuwezesha wanachama wao waendelee kunufaika na siku nyingine ziende kucheza kwenye viwanja hivyo.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema timu hizo zina ratiba ambazo zimepangiwa kwa mwaka mzima na pia zenyewe hujipangia ratiba zao kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali rasmi.

“Isipokuwa ni wazo zuri na tutalifikisha kwa timu hizi kuona kama zinaweza kufanya mpango wa kurejesha kwa jamii kwa kufanya michezo ya hisani kwenye halmashauri hizi, ikiwemo Nyasa kuhakikisha wanahudumia wananchi wengi ambao ni wapenzi wa timu hizi,” amesema.

Mbunge Mbulu Vijijini, Flatei Massay amehoji lini Serikali itapeleka fedha za kuukamilisha uwanja wa Mbulu mkoani Manyara kama ilivyoahidi bungeni kuwa watapeleka fedha za kuumalizia.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema bado wanaendelea kujadiliana na wamiliki, ili kuona namna ambavyo watafanya ili kuweza kuvifanyia marekebisho na pia namna ya kuviendesha.

“Japokuwa havipo katika awamu ya kwanza (ya ukarabati), lakini vimepangwa kuangaliwa namna ambavyo tutavirekebisha na kuvifanyia utaratibu wa namna ya kuviendesha ili wananchi wapate miundombinu ya michezo katika jimbo lake,” amesema Mwinjuma.

Kwa upande wake, Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo amehoji ni nini mkakati wa Serikali kuusaidia Mkoa wa Songwe, ili upate kiwanja cha michezo kwa kuwa tayari eneo limetengwa Vwawa mkoani humo.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema atalichukua ili kuona namna wanavyoweza kusaidiana na mamlaka ya Songwe, ili kutengeneza kiwanja vya michezo hasa katika eneo walilokwisha lipanga.

Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Christine Ishengoma amehoji ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwanja cha michezo cha Jamhuri mkoani Morogoro kwa kiwango cha kisasa na kuweka taa.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema Uwanja wa Jamuhuri ni miongoni mwa viwanja vitano vya kwanza walivyoviorodhesha ambavyo wanafanya mazungumzo na wamiliki wake, ili kuanza kuvikarabati.

“Uwanja huo upo pamoja na Uwanja wa Mkwakwani (Tanga), Kirumba, Sokone (Mbeya) katika awamu ya kwanza na mara tutakapokubaliana na mmliki tutaanza ukarabati,” amesema.

Naye Mbunge wa Kibamba, Issa Mtemvu, amehoji ni upi mkakati wa Serikali kuanza ujenzi wa viwanja vya michezo ndani ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo tayari wametenga eneo la ekari 11.

Akijibu, Mwinjuma amesema kwa sasa nguvu kubwa ya Serikali ni katika kutengeneza miundombinu ya viwanja vitakavyotumika katika mashindano ya AFCON, lakini wanafahamu umuhimu wa Wilaya ya Ubungo kuwa na kiwanja chake cha michezo.

“Tutakapomalizana na hilo (AFCON) ni kuhakikishie mheshimiwa mbunge na hili litakuwa miongoni mwa masuala tutakayoyafanyia kazi kwa awali,” amesema.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Ilemela, Dk Angeline Mabula amehoji ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuweka taa katika Kiwanja cha Mpira cha CCM cha Kirumba, mkoani Mwanza.

Akijibu swali hilo, Mwinjuma amesema kiwanja cha CCM cha Kirumba ni miongoni mwa viwanja vitano ambavyo vimewekwa katika mkakati wa Serikali wa kuvirekebisha, ili kukidhi ubora na viwango vya Shiriki la Soka barani Afrika (CAF).

“Kwa sasa wizara ipo katika hatua ya majadiliano na mmiliki, ili kukubaliana namna ya kugharamia na kuviendesha viwanja hivyo, ikiwemo uwanja wa CCM Kirumba ambapo pamoja na marekebisho mengine, uwanja huu utawekewa taa kuwezesha shughuli za michezo kufanyika hata nyakati za usiku,” amesema.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Chief Editor

Insecurity prompts Zanzibar to review its lucrative island leasing

The Tanzanian central government is planning to boost its security presence in the Zanzibar archipelago. A commission tasked with auditing the country’s security forces was appointed in July by President Samia Suluhu Hassan. It says it is concerned about the situation in the country’s Indian Ocean islands that are under the control of the semi-autonomous Zanzibar local government.Continue Reading