Sakata la uraia wa ‘mchongo’ wachezaji wa Singida lachukua sura mpya

Sakata la uraia wa ‘mchongo’ wachezaji wa Singida lachukua sura mpya

Sakata la uraia wa ‘mchongo’ wachezaji wa Singida lachukua sura mpya

Moshi/Dar. Sakata la wachezaji watatu wa timu ya Singida Black Stars (SBS), waliopewa uraia wa Tanzania, limechukua sura mpya baada ya Wakili Peter Madeleka kutangaza kufungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu.

Leo Jumamosi Januari 25, 2025 saa 2:14 asubuhi, wakili Madeleka kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter) na baadaye kuzungumza na gazeti hili, alidai uraia wa Tanzania hauwezi kutolewa kiholela au kwa utashi wa waziri.

Alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia uamuzi huo wa Madeleka, Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Paul Mselle hakutaka kuzungumzia jambo hilo kwa madai kwamba hajasoma wala kumsikia akizungumza.

“Sina la kuzungumza kwa sababu sijui kama kuna kitu kama hicho, labda nifuatilie kujua…hata huko X sijaona,” alisema Mselle.

Tangu wachezaji hao, Emmanuel Keyekeh raia wa Ghana, Josephat Bada wa Ivory Coast na Muhamed Camara wa Guinea wapewe uraia, kumekuwa na mijadala mizito mitandaoni kuhusu uhalali huo.

Wengi wanaohoji uamuzi huo, wanadai kuna utaratibu uliokiukwa kwa kuwa wachezaji hao hawajaishi nchini kwa miaka 10, lakini wachezaji hao wanadaiwa kutokidhi kigezo hicho kwani walisajiliwa Julai 2024.

“Tatizo ninaloliona ni kumeonekana kama kuna kaupendeleo fulani au shinikizo kutoka kwa mtu mwenye nguvu kuwapa uraia hao wachezaji walioishi muda mfupi sana,” alidokeza ofisa mmoja wa Uhamiaji.

“Kuna wakimbizi wameishi miaka zaidi ya 10 na wameomba uraia lakini hawapewi, kuna wawekezaji na wafanyabiashara wanalipa kodi na wameomba uraia lakini hawapewi. Shida inaanzia hapo,” amesisitiza.

Takwimu zinaonesha kati ya Julai 2023 hadi Aprili 2024, wageni 3,504 walipatiwa uraia wa Tanzania baada ya kukidhi vigezo ukilinganisha na wageni 190 waliopewa uraia mwaka 2022/2023.

Kati ya wageni hao, ni wageni 3,319 ambao ni wahamiaji walowezi wasiohamishika wenye asili ya mataifa ya Comoro, Msumbiji, Burundi na Rwanda huku Msumbiji pekee wakiwa ni 3,166 na Comoro 147.

Wageni 185 kati ya 3,504 walitoka mataifa ya Afrika Kusini, Burundi, DR Congo, Cuba, India, Iran, Italia, Lebanon, Kenya, Pakistan, Rwanda, Somalia, Syria, Uganda, Uingereza, Msumbiji, Yemen na Zimbabwe.

Takwimu hizo zilitolewa bungeni Jijini Dodoma na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni wakati wakiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/2025.

Kwa mujibu wa sheria ya Uhamiaji Tanzania, sura ya 357, ili mgeni aweze kupewa uraia wa Tanzania lazima awe ametimiza vigezo kadhaa mojawapo awe anaelewa vizuri lugha ya Kiswahili au Kiingereza.

Masharti mengine mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi na awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa miezi 12 mfululizo kabla ya kutuma maombi yake ya kuomba uraia.

Katika muda huo wa miaka 10, lazima awe ameishi ndani ya Tanzania kwa muda usiopungua miaka saba, awe na tabia njema na awe amechangia ukuzaji uchumi, sayansi na tekinolojia na utamaduni wa Tanzania.

Alichokisema Madeleka

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Januari 25, 2025, Wakili Madeleka amesema Katiba ya Tanzania ambayo ndiyo sheria mama ya nchi, inataka kila mtu aitii lakini ibara ya 26(2) imetoa wajibu kwa mtu yeyote kulinda Katiba na sheria.

“Sheria ya uraia inasema ili mtu aweze kupewa uraia kwa njia ya Tajnisi, pamoja na mambo mengine, awe amekaa nchini kwa miaka saba. Hicho kilichofanyika kwa wachezaji SBS kinyume cha sheria na ni kosa,”alisema.

“Sasa sheria inasema waziri ndiye mwenye maamuzi ya mwisho pale ambapo atakuwa amefanya kwa usahihi. Waziri siyo mwenye kauli ya mwisho kwenye maamuzi ya sheria ndio maana kuna mahakama,” amesema.

“Ibara ya 13(1) ya Katiba inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria kwa hiyo hata huyo waziri linapokuja suala la sheria yuko sawa na watu wengine akiivunja atapelekwa mahakamani,”amesisitiza wakili Madeleka.

“Kwa hiyo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji tunampeleka mahakamani. Huo uamuzi haujakidhi matakwa ya hivyo vifungu vya sheria ya uraia ya Tanzania ndiyo maana sisi tunakwenda mahakamani,”ameeleza wakili.

“Tutakwenda kwenye mahakama ya kikatiba kuiomba itamke kwamba kilichofanywa kwa wachezaji hao ni kinyume cha sheria lakini iende mbali itoe amri ya kuwavua uraia kwa sababu wamevunja sheria,” ameongeza.

Jitihada za kumpata Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Anna Makakala jana, hazikufanikiwa kwani hakupokea simu yake ya mkononi wala kujibu ujumbe mfupi aliotumiwa ili kufafanua zaidi kuhusu kukiukwa kwa sheria katika utoaji wa uraia kwa wachezaji hao.

Hata hivyo, juzi, taarifa ya Uhamiaji iliyosainiwa na Mselle ilieleza kwamba wachezaji hao waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia Tanzania.

“Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutarifu umma kuwa watajwa (wachezaji hao watatu wa SBS) ni raia kwa Tajnisi,” ilisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI), Mselle.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Britam half-year net profit hits Sh2bn on higher investment income

Insurer and financial services provider Britam posted a 22.5 percent jump in net earnings for the half-year ended June 2024, to Sh2 billion, buoyed by increased investment income.

The rise in half-year net profit from Sh1.64 billion posted in a similar period last year came on the back of net investment income rising 2.5 times to Sh13.27 billion from Sh5.3 billion.

“We are confident in the growth and performance trend that Britam has achieved, supported by its subsidiaries in Kenya and the region. Our business is expanding its revenue base while effectively managing costs,” Britam Chief Executive Officer Tom Gitogo said.

“Our customer-centric approach is fueling growth in our customer base and product uptake, particularly through micro-insurance, partnerships, and digital channels.”

The investment income growth was fueled by interest and dividend income rising 34 percent to Sh9.1 billion, which the insurer attributed to growth in revenue and the gains from the realignment of the group’s investment portfolio.

Britam also booked a Sh3.79 billion gain on financial assets at a fair value, compared with a Sh1.8 billion loss posted in a similar period last year.

The increased investment income helped offset the 12.7 percent decline in net insurance service result to Sh2.13 billion in the wake of claims paid out rising at a faster pace than that of premiums received.

Britam said insurance revenue, which is money from written premiums, increased to Sh17.8 billion from Sh16.6 billion, primarily driven by growth in the Kenya insurance business and regional general insurance businesses, which contributed 30 percent of the revenue.

The group has a presence in seven countries in Africa namely Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, South Sudan, Mozambique, and Malawi.

Britam’s insurance service expense hit Sh13.6 billion from Sh11.3 billion, while net insurance finance expenses rose 2.6 times to Sh12.3 billion during the same period.

“Net insurance finance expenses increased mainly due to growth in interest cost for the deposit administration business driven by better investment performance. This has also been impacted by a decline in the yield curve, which has led to an increase in the insurance contract liabilities. The increase has been offset by a matching increase in fair value gain on assets,” said Britam.

Britam’s growth in profit is in line with that of other Nairobi Securities Exchange-listed insurers, which have seen a rise in profits.

Jubilee Holdings net profit in the six months increased by 22.7 percent to Sh2.5 billion on increased income from insurance, helping the insurer maintain Sh2 per share interim dividend.

CIC Insurance Group posted a 0.64 percent rise in net profit to Sh709.99 million in the same period as net earnings of Liberty Kenya nearly tripled to Sh632 million from Sh213 million, while Sanlam Kenya emerged from a loss to post a Sh282.2 million net profit.

Continue Reading