Kuanguka kwa roketi katika kijiji cha Poland cha Przewodow. Nini kinafahamika hadi sasa?

Kuanguka kwa roketi katika kijiji cha Poland cha Przewodow. Nini kinafahamika hadi sasa?

Siku mojabaada ya roketi ku kuanguka katika kijiji cha  Przewoduv  mashariki mwa Poland karibu na mpaka na Ukraine, na kuwauwa watu maafisa nchini Poland wanasema lilitengenezwa na Urusi. Hatahivyo  Shirika la habari la Associated Press, likiwanukuu maafisa wa Marekani, limeandika kwamba kombora hilo limedaiwa kuwa lilifyatuliwa na Ukraine kwa lengo la kudungua kombora la Urusi. 

 Ukweli kwamba kombora lililoangushwa halikufyatuliwa kutoka Urusi  pia ulielezewa na rais wa Marekani Joe Biden.

“Kombora lililotengenezwa Urusi “

Wizara ya mambo ya nje ya Poland ilikuwa ya kwanza kutangaza kuwa kombora lililotengenezwa Urusi limeanguka nchini mwake majira ya saa nne na dakika 54 asubuhi.    

 Kufuatia kuanguka kwa kombora hili, Waziri wa Poland wa mashauri ya  Zbigniew Rau alimuita balozi wa Urusi  kumtaka maelezo ya moja kwa moja kuhusiana na kisa hicho, imesema taarifa ya shirika la  AP.

Maelezosawa na hayo pia yalitolewa  rais wa Andrzej Duda. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba kombora lilitengenezwa na Urusi, lakini uchunguzi bado unaendelea ,” aliwaambia waandishi wa habari , kulingana na shiruka la habari la  Reuters. 

Rais Duda alisema kwamba hakuna ushahidi  kuhusu ni nani hasa aliyefyatua kombora hilo , na akaelezea matumaini kwamba hili lilikuwa ni suala la kipekee. 

Maelezo kuhusu ulinzi wa anga  wa Ukraine   

Ruka Twitter ujumbe

Maelezo ya video,Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa Twitter ujumbe

Jumatano asubuhi  shirika la habari la Associated Press, liliwanukuu  maafisa watatu wa Marekani ambao halikuwataja majina, wakisema kuwa kombora lililoanguka Poland linaaminiwa kuwa lilifyatuliwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine.

 Maelezo kwamba kombora lilifyatuliwa na Urusi awali yalihojiwa na Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye aliitisha mkutano wa dharura wa viongozi wanchi wanachama wa  G7 na  NATO, walioshiriki mkutano wa G20  mjini  Bali.

 “Kulingana na mtazamo wa mambo yalivyo,  huenda Urusi haikufyatua kombora, lakini tutaona ,”  alisema Bide baada ya mkutano. 

Waziri mkuu wa Uingereza  Rishi Sunak, akizungumza na waandishi wa habari mjini Bali, hakurudia maeneo ya Biden kwamba huenda kombora halikuwa la Urusi. Alisisitizia juu ya haja ya kubaini ukweli kwanza, lakini akasema : “Lazima sote tuwe wazi: hakina kitu kama hiki kingetokea kama hapangekuwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.” Ukweli kwamba jeshi la NATO liliweza kuifuatilia roketi iliyolipuka katika Poland.

Kulingana na CNN, ndege ya kombora ilirekodiwa na ndege ya  uchunguzi ya NATO, ambnayo ilikuwa ikifanya upelelezi katika anga la Poland.  

Kuhusu ni nani aliyefyatua kombora hili, haikuelezwa na CNN, ambayo ilieleza tu kwamba walikusanya ujasusi, ikiwa ni pamoja na kuona mabaki ya kombora vyaliyoachwa na rada, ambavyo vilihamishiwa katika nchi za NATO na Poland. 

G

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

 
Maelezo ya picha,

Kijiji cha  Poland cha Pshevoduv  kiko karibu na mpaka na Ukraine  

 

Roketi ilianguka katika Poland  mchana wa tarehe 15 Novemba  saa   tis ana dakika 40 (17:40 kwa saa za Moscow ),  wakati jeshi la Urusi lilipokuwa likiupiga makombora mji wa Kyiv  na miji mingine, ikiwemo ya magharibi. Lilipiga  na kuwauwa watu wawili.  

 Kijiji cha Pshevoduv, ambako tukio lilitokea, kiko kilomita tano kutoka kwenye mpaka na Ukraine.

 Wizara ya ulinzi ya Ukraine ilisema kuwa hakuna mashambulio  ya Ukraine ambayo yalilenga karibu na mpaka wa Ukraine na Poland siku ile, na picha zilizochapishwa za vifusi hazikuhusiana na silaha za Urusi. Taarifa kwamba kombora la Urusi huenda liliangukia upande wa Poland zilitajwa kama  “uchokozi wa makusudi ili kuifanya hali kuwa mbaya zaidi ”  katika wizara ya ulinzi ya Urusi. 

 Baadaye , wizara ya ulinzi ya Urusi pia ilisema kuwa vipande vya roketi vilitambuliwa na wataalamu wa Urusi kweney picha  kama sehemu ya  kombora aina ya  S-300 la kuzuia mashambulio ya anga ambalo ni la vikosi vya Ukraine.   

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katika hotuba yake ya jioni siku moja kabla, alisema kwamba “Ni mara ngapi Ukraine imesema kwamba nchi gaidi haitakomea katika nchi yetu? Poland, nchi za  Baltic – ni muda tu kabla ugaidi wa Urusi ufike mbali zaidi ,” alisema Zelensky.

 Jumatano , mshauri katika ofisi ya rais Zelensky, Mikhail Podolyak, alisema kwamba urusi kwa vyovyote vile inahusika kwa vifo vilivyotokea katika Przevoduv.

 “Lengo, njia za kuua, hatari, kuongeza mzozo – haya yote ni Urusi pekee. Na hakuna maelezo mengine ya sababu ya kupiga makomboraya ziada.  

 Kwasababu wakati nchi inayochokoza inapofyatua makombara mengi ya ya masafa mengi kuvuka eneo zima la Ulaya kwa silaha zake zilizopitwa na wakati za  Soviet   (class X missiles),  maafa yanatokea haraka au baadaye katika maeneo ya mataifa

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories