Tanzania Dar es Salaam
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua nafasi za watendaji watano akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali (DC), Reuben Mfune anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus leo Jumanne, Januari 24, 2023, inawataja mwingine aliyetenguliwa ni Msongela Palela Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Musoma (DED), Mkoa wa Mara.
Wakurugenzi wengine wa halmashauri waliotenguliwa kwa mujibu wa taarifa hiyo ni Michael Matomora wa Iramba, Linno Pius wa Ushetu na Sunday Ndori wa Halmashauri ya Ludewa.
Januari 11, 2023, Mfune alifikishwa mahakamani akituhumiwa katika kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh51 milioni.
Source: mwananchi.co.tz
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Zanzibar airport monopoly puts 600 jobs at risk
On September 14, 2022, the director general of ZAA issued a directive that gave Dnata Zanzibar Aviation Services Limited an exclusive access to the newly constructed Terminal III, barring other operators.Continue Reading
‘Pilot error’ caused Precision Air crash
Reports says prevailing poor weather led to the pilots failing to heed warning signals.Continue Reading
Zanzibar introduces $44 insurance fee for visitors
Visitors travelling to Zanzibar will now have to pay an insurance fee of $44 (about Sh118,360) with effect from September 1.Continue Reading