Rais Mwinyi ateuwa watendaji wapya

Rais Mwinyi ateuwa watendaji wapya

Zanzibar:
 
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa watendaji sita katika taasisi tofauti akiwemo Samora Chacha, aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Kabla ya uteuzi huo, Chacha alikuwa mfanyakazi katika sekta binafsi.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Ijumaa Januari 20, 2023 na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema, Adil Fauz George ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa idara ya usimamizi na uratibu wa shughuli za utalii katika kamisheni ya utalii.

“Kabla ya uteuzi huo George alikuwa mfanyakazi wa sekta binafsi,” imesema taarifa hiyo.

Katibu mkuu mstaafu, Yakout Hassan Yakout ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamisheni ya utumishi wa umma huku Ali Saleh Mwinyi ameteuliwa tena kwa kipindi cha pili kuwa mwenyekiti wa bodi ya shirika la magazeti.

Taarifa hiyo imesema Dk Mwinyi amemteua Safia Ali Rijaal ambaye ni mstaafu katika utumishi wa umma kuwa mwenyekiti bodi ya shirika la huduma za maktaba Zanzibar na Ussy Khamis Debe ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa baraza la taifa la watu wenye ulemavu

Uteuzi huo unaanza leo Januari 20, 2023

 

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories

Zanzibar Commerce
Top News
Investment News Editor

Zanzibar Airports Authority enforces Dnata monopoly

. Airlines that have not joined the Zanzibar Airports Authority’s (ZAA) preferred ground handler, Dnata, at the Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA) face eviction from the Terminal Three building Dnata is the sole ground handler authorised to provide services for flights that operate at Terminal 3.Continue Reading