Rais Mwinyi akerwa na matokeo mabaya ya mitihani Zanzibar

Rais Mwinyi akerwa na matokeo mabaya ya mitihani Zanzibar

Unguja, Zanzibar:

Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi, amesema matokeo ya mitihani visiwani humo hayaridhishi hivyo anataka kuona mabadiliko zaidi baada ya Serikali kuboresha miundombinu ya shule.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Januari 6, 2023 wakati akifungua shule ya msingi ya ghorofa ya Salum Turky Mpendae kwa Bint Hamrani ikiwa ni mwendelezo wa kusherehekea miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yataadhimishwa Januari 12, 2023.

Hata hivyo, mwaka huu hakutakuwa na gwaride badala yake fedha zake zimeelekezwa katika sekta ya elimu.

“Naamini baada ya kuyakamilisha mambo haya, kinachofuta sasa ni kupata matokeo mazuri, hivi sasa matokeo ya wanafunzi hayaridhishi tunataka kuona matokeo mazuri zaidi huku tukiendelea kuboresha maslahi ya walimu,” amesema.

Mbali na hayo, amebainisha kuwa njia pekee ya kujenga taifa ambalo lina maendeleo ni elimu, hivyo ni lazima kipaumbele kiwe kwenye elimu na ndiyo maana serikali inafanya kila linalowezekana katika sekta hiyo.

Amesema, shule hiyo ya ghorofa ndiyo mfano wa shule zote za msingi zinavyotakiwa kuwa Zanzibar na sio za ghorofa tu bali ziwe na maabara za sayansi, maktaba, vyumba vya kompyuta na madarasa ambayo wanafunzi hawatazidi 45 kwa kila chumba.

“Hayo ndiyo Mapinduzi ya kweli ambayo tunayataka na sasa serikali inatimiza lengo likiwa ni watoto wetu wapate elimu bora na naamini ifikapo mwaka 2025 sekta hii itakuwa imepiga hatua kubwa,” amesema.

Hivyo, aliwaasa wazazi kuzingatia kuwa elimu ndiyo urithi mzuri na wenye thamani kubwa ambao mzazi anaweza kumuachia mtoto wake.

Akimkaribisha Rais Mwinyi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla amesema bado wana deni kubwa; Wizara ya Elimu, wazazi, walimu na wananchi kuhakikisha wanashirikiana ili kupata matokeo mazuri kwa watoto wao.
“Haitasaidia kuwa na jengo zuri halafu matokeo yakawa mabaya hivyo naamini mkakati wa wizara, wazazi, viongozi wa jimbo utatuwezesha kushirikiana pamoja kuhakikisha tunabadilisha matokeo ya watoto wetu kwani miundombinu bora ya elimu ameshatuwekea kiongozi wetu,” amesema

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa, amesema kupitia fedha za Uviko 19, wizara imejenga shule za msingi mpya 45 za ghorofa, kati ya hizo Unguja 23 na 22 Pemba.

Amesema tayari Wizara imeshajenga vyumba vya madarasa 1,200 kati ya vyumba vya madarasa 1,500 vilivyoahidiwa katika ilani ya CCM ya mwaka 2020/25.

Katibu Mkuu Wizara hiyo, Khamis Abdulla Said, amesema shule hiyo ya ghorofa mbili imegharimu Sh4 bilioni na ina vyumba vya madarasa 29, uwezo wa kubeba wanafunzi 1305 kwa wastani wa wanafunzi 45 kila darasa.

Amesema ina maabara, chumba cha kopyuta, viti vya kukalia maktaba, ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya msaidizi mwalimu mkuu, Ofisi tatu za walimu wakuu na vyoo 25.

“Pamoja na miundombinu hiyo pia serikali imeipatia viti na meza 1,305 kwa ajili ya wananfunzi na hakuna mwanafunzi atakayekaa chini,” amesema.

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories

High Court rejects Transworld’s application
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

High Court rejects Transworld’s application

The High Court in Dar es Salaam has struck out an application in which Transworld Aviation, a ground handler at the Abeid Aman Karume International Airport (AAKIA) was seeking permission to sue the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).Continue Reading