Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imewatimua vigogo wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kwa kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi wa shirika hilo.
Mbali na hilo, kamati hiyo imewataka vigogo wa shirika hilo kuandika barua kueleza ni kwanini viongozi wakuu wa shirika hilo wameshindwa kufika katika kikao hicho cha kamati licha ya taarifa ya wito kuwafikia tangu Januari 5, 2023.
Akizungumza leo Jumatatu Januari 23, 2023 jijini Dodoma, mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerry Silaa amesema kitendo cha Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi kutofika katika kikao hicho bila taarifa ni dharau kwa Bunge.
“Barua ya kuwaita iliandikwa tangu Desemba 2022 lakini wao waliipata Januari 5, 2023 hakusema chochote leo wanakuja baadhi ya watumishi, hii ni dharau kwa Bunge,” amesema Silaa.
Kwa upande wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Silaa amesema licha riba za mikopo katika taasisi za fedha kupungua baada ya BoT kufanya usajili wa taasisi zinazotoa mikopo lakini kwa taarifa walizonazo kuna gharama nyingine anawekewa mteja.
“Inawezekana mtu akaambiwa gharama za mkopo ni Sh1 milioni, ukichukuwa gharama za mikopo, riba na gharama nyingine inarudi pale pale na wananchi wanaumia,” amesema mwenyekiti huyo wa PIC.
Amesema wameitaka BoT kujielekeza katika maeneo mengine ya mtandao, miamala ya fedha ya simu na kuhakikisha wanakuwa na mfumo bora wa malipo ya kieletroniki, mfumo ambao unahusisha mabenki, miamala ya simu na watoa huduma wengine.
Silaa ameongeza kwamba BoT inatakiwa kuhakikisha gharama za mikopo na riba zinakuwa za chini kwa ajili ya kutomuumiza Mtanzania wa chini.
Source: mwananchi.co.tz
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Tanzania’s path to 4Rs: The President Samia’s era
Tanzania has embarked on a journey of resilience, rebuilding, reconciliation, and reform under the leadership of President Samia Suluhu Hassan.Continue Reading
Dissecting the role of the insurance ombudsman in Tanzania
The basic purpose of an insurance plan is to provide financial security to you and your family in case of your misfortunes during the policy tenure.Continue Reading
Zanzibar terminates land lease offered to British developer
The Revolutionary Government of Zanzibar (SMZ) has terminated a land lease held by British property developer Pennyroyal Limited in Matemwe, the developer has announced.Continue Reading