Othman: Jiandikisheni kwenye daftari la mpigakura tulete mabadiliko Zanzibar

Othman: Jiandikisheni kwenye daftari la mpigakura tulete mabadiliko Zanzibar

Othman: Jiandikisheni kwenye daftari la mpigakura tulete mabadiliko Zanzibar

Unguja. Wakati awamu ya pili ya uandikishaji wa daftari la mpigakura ikitarajia kuanza Februari Mosi, Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo taifa, Othman Masoud amewataka wananchi wote kuitumia vyema awamu hii ya mwisho ya uandikishaji ili wapate fursa ya kupiga kura na kukichagua chama hicho kushika dola.

Awamu, hiyo ya pili itaanzia Wilaya ya Micheweni na unatarajiwa kumalizika Machi 17, 2025 wilayani Mjini Unguja.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), inatarajia kuandikisha wapiga kura 78,922.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika ziara ya chama hicho aliyoianza jana Janauri 28, 2025 katika majimbo ya Tumbe na Mapofu Wingwi Pemba, Othman amesema mabadiliko ni muhimu kupitia sanduku la kura.

Amesema ni lazima wananchi wa Zanzibar kuutambua mwaka huu wa uchaguzi kwamba ni muhimu kwa mabadiliko na ni lazima kuutumia vyema kwa kukiunga mkono ACT ili kuinusuru Zanzibar na kuweza kupata maendeleo.

“Wananchi lazima kufahamu kwamba silaha kubwa ya chama chochote cha siasa kuweza kuleta mabadiliko ni kuwa na viongozi imara na wanachama kushiriki katika uchaguzi kwa kuandikishwa rasmi kuwa wapiga kura na kwachagua viongozi wanaowataka ili kuleta maendeleo, tujitokeze kujiandikisha,” amesema Othman.

Amesema Zanzibar inaweza kupiga hatua iwapo itaweza kumiliki na kuvitumia ipasavyo vyanzo vyake mbalimbali vya uchumi vilivyopo.

Amesema hilo litawezekana kwa kuwapo mabadiliko ya kisiasa nchini asa kwa vile wananchi wote wa Zanzibar wameamka na wapo tayari Unguja na Pemba kuungana katika kupambania kuleta mabadiliko ya nchi na mageuzi ya uongozi wa kisiasa na kuweza kuharakisha maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.

Amesema Wazanzibari kuamka na kuungana kukiunga mkono chama hicho ni kuitikia wito wa viongozi ili chama cha ACT kiweze kutimiza dhamira ya kuisaidia Zanzibar kubadili maisha ya watu kwa kupambana na umasikini na kuleta uchumi imara.

“Uchumi imara utakaosaidia kupatikana ajira za heshima na kupata mishahara inayowiana na kazi yao kwa vijana mbalimbali hapa Zanzibar,” amesema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Omar Ali Shehe, amesema kwamba uchaguzi wa mwaka huu ni maalumu katika kuinusuru Zanzibar na kwamba ujumbe huo unapaswa kuwafikia watu wote ili waungane pamoja katika kujali Uzanzibari na mapenzi kwa nchi yao.

Amesema utu na ubinadamu umepotea na kwamba kuinusuru Zanzibar ni kuwapa wananchi uhakika wa kuishi maisha ya wananchi bila wasisiwasi sambamba na kuondokana na umasikini kwa wananchi ambapo hali zao zinaendelea kudorora kwa umasikini siku hadi siku na kwamba uchaguzi ujao ni turufu na fursa ya mwisho kuinusuru zanzibar.

Amesema ACT Wazalendo ni chama chenye sera bayana na kwamba itahakikisha kuzitekeleza katika kuipa Zanzibar mamlaka kamili kupitia viongozi sahihi waliopo katika chama hicho ambao pia wanazijua vyema shida za waznzibari za kijamii na kiuchumi.

Othman yupo kisiwani Pemba kwa ziara maalumu ya chama na masuala mbalimbali ya kijamii katika mikoa yote huko Kisiwani Pemba ikiwa ni pamoja na kuwaelezea Wazanzibari umuhimu wa kujiandikisha katika awamu ya mwisho ya daftari la kudumu kwa matayarisho ya uchaguzi mkuu kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms

President Samia Suluhu Hassan, has handed over a cheque of 354m/- from the National Bank of Commerce (NBC) as compensation to tobacco farmers, who were affected by hailstorms during the previous farming season in various regions across the country.

Handing over the cheque in Dodoma, the compensation is part of the crop insurance service provided by NBC in collaboration with the National Insurance Corporation (NIC).

Furthermore, President Samia has also handed over health insurance coverage to members of the Lindi Mwambao Cooperative Union based in Lindi Region, through the Farmers’ Health Insurance service provided by the bank in partnership with Assurance Insurance Company.

While visiting the bank’s pavilion at the Nanenane Agricultural Exhibition and being received and briefed by the bank’s Managing Director, Mr. Theobald Sabi, she said: “This crop insurance is one of the crucial solutions in ensuring farmers have a reliable income, without fear of challenges such as natural disasters, including hailstorms.

“I call upon all farmers in the country to make the best use of this important opportunity by accessing these kinds of insurance services. I also highly commend NBC and all the stakeholders participating in this programme.”

Elaborating further on the crop insurance service, the Minister of Agriculture, Hussein Bashe, stated that it will help to recover the loss farmers incurred, especially in various calamities beyond their control.

Citing them as floods, fires, and hailstorms, which have significantly affected the well-being of farmers and caused some to be reluctant to invest in the crucial sector, Mr Bashe added: “However, our President, this step by NBC is just the beginning, as this is the second year since they started offering this service, and the results are already visible.

“As the government, we promise to continue supporting the wider implementation of this service, with the goal of ensuring that this crop insurance service reaches more farmers.”

ALSO READ: NBC participates in TFF 2023/24 awards, promises to enhance competition

On his part, Mr Sabi said that the farmers who benefited from the compensations are from 23 primary cooperative unions in the regions of Shinyanga, Geita, Tabora, Mbeya, Katavi, and Kigoma.

He added: “In addition to these insurance services, as a bank, through this exhibition, we have continued with our programme of providing financial education and various banking opportunities to farmers, alongside offering them various loans, including loans for agricultural equipment, particularly tractors, to eligible farmers.:

At the NBC booth, President Samia also had the opportunity to be briefed on the various services offered by the bank to the farmers namely crop insurance and health insurance services.

There, the President had the chance to speak with some of the beneficiaries of the services, including the Vice-Chairman of the Lindi Mwambao Primary Cooperative Union, Mr. Hassan Mnumbe, whose union has been provided with a health insurance card from the bank.

Source: allafrica.com

Continue Reading

Popular
Swahili News Editor

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading