NIKWAMBIE MAMA: Tuipeleke Tanzania duniani

NIKWAMBIE MAMA: Tuipeleke Tanzania duniani

NIKWAMBIE MAMA: Tuipeleke Tanzania duniani

Kwanza nikupe kongole kwa jitihada za kimkakati za kumtua mama ndoo kichwani. Jitihada hizi zinaweza kuzaa matunda mapema kama zitaunganishwa na zile za kumkwamua mama kiuchumi.

Uchumi wa mama ukirekebika, atapiga ndege wengi kwa jiwe moja. Kwanza atatua ndoo, kisha ataachana na nishati chafu za kupikia. Kwa kitendo hicho mama atakuwa salama usalmini mwenye afya madhubuti.

Njia mojawapo ya kuyafikia hayo ni elimu na matangazo yanayoweza kumfunulia fursa zake. Tunafahamu kuwa akinamama ni hodari sana wa kazi za mikono.

Iwapo watapewa elimu ya ubunifu watasogea kwa urahisi. Pamoja na kinamama kuhamasishwa kujiunga na vyuo vya ufundi stadi, pia tuwafuate wale walioko vijijini wasio na uwezo wa kujiunga na vyuo hivyo. Moja ya bidhaa zinazouzika zaidi duniani ni sanaa.

Mtu wa Taifa lolote anaweza kununua sanaa ya Taifa lingine bila kujali asili au lugha ya msanii. Anaweza kuelewa mengi ya wenzake katika sanaa hiyo na pia kujifunza tamaduni za mataifa mbalimbali. Sanaa ni kielelezo cha utamaduni wa Taifa.

Kwa kupitia sanaa tunatangaza utamaduni wetu na kujifunza tamaduni za wenzetu. Tunafungua milango ya biashara kwa kubadilishana mahitaji yetu na pia tunapanua sekta za elimu na utalii kwa njia hii.

Watafiti wameweza kutambua historia za nchi na matukio yaliyopita katika sanaa zilizopo kwenye mapango ya kale. Sasa tunajua matukio makubwa kama gharika, tufani na matetemeko ya ardhi yanatoyotokana na tabia za nchi kwa kupitia vielelezo vya sanaa hiyohiyo iliyowekwa tangu kale.

Wafanyabiashara wa Kimataifa hupata fursa kwa kupitia sanaa. Huweza kutambua urithi wa asilia wa nchi kama gesi, mafuta na madini kwa kusoma tafsiri za kumbukumbu zilizoachwa miaka elfu nyingi iliyopita. Na kwa kuwa wanaweza kujua mahitaji ya msingi ya eneo hilo, basi wanaweza pia kujua ni bidhaa gani mbadala za kupeleka. Mfano mzuri ni pale tunapoona sanaa za China.

Kundi la sanaa la Kichina litapambwa na jukwaa la Kichina, litapiga muziki wa Kichina, litacheza sarakasi za Kichina na kufanya maigizo ya kikwao. Zaidi ya hapo litatangaza bidhaa na teknolojia kutoka China.

Taifa lolote linalojitambua linatambua kuwa sanaa yao inabeba utaifa wao. Ndipo penye nafasi ya kuuonesha ulimwengu urithi na utamaduni wake. Na kwa kuwa hapa duniani kila mmoja anamhitaji mwingine, yule anayejionesha anakidhi wahitaji wengi zaidi na mwisho wa siku ataongeza tija zaidi ya wale walio kimya.

Imekuwa kawaida ya kumbi za viwanja vya ndege, majumba ya makumbusho, vituo vya tamaduni na hoteli za kitalii kupambwa kwa sanaa adhimu na vito vinavyopatikana kwenye mataifa husika. Wageni wanaweza kuona utajiri wa hapo na wafanyabiashara kujua wapi pa kupeleka vinyago kubadilishana na lulu.

Biashara ya zamani ya mzunguko ilihusisha bidhaa tofauti. Kule Uhindini kulikuwa na matumizi makubwa ya viungo vya mboga kama pilipili manga, mdalasini, iliki, kitunguu saumu na kadhalika.

Katika viungo hivi kuna kinga na tiba ya maradhi mengi ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza. Hivyo walipata suluhu ya maradhi sugu kama shinikizo la damu, kisukari, figo na moyo.

Katika sanaa zinazotoka India hukosi kuona jinsi wanavyozijali tamaduni zao. Na ni wazi kuwa dunia inahitaji tamaduni hizo, zikiwemo dawa zao. Hivyo wafanyabiashara wanaokwenda kununua bidhaa kule wanaona fursa mpya kutokana na mahitaji ya kule wanakotoka.

Wahindu hutumia sana kunde na mbaazi zinazopatikana kwa wingi Lindi na Mtwara. Pia hupenda sana urembo wa vito kama fedha na dhahabu.

Hivyo wafanyabiashara wanachukua hiki hapa na kwenda kubadilishana na kile cha kule. Kwa upande mwingine, Wachina pia hufanya hivyo. Wao hutangaza chai, mchele na soya kwenye filamu zao. Wakati wa matamasha yanayowajumuisha Wachina unaweza kushuhudia mauzo ya mavuno ya shamba na bidhaa za viwandani.

Kwenye onesho la msanii, mjasiriamali pia anaingia kukidhi fursa. Huo ndio Utaifa. Sekta mbalimbali za uchumi nchini zinaweza kufanikisha matumizi mazuri zaidi ya sanaa za nyumbani.

Zinaweza kuweka mikakati na hatimaye masharti ya lazima kwa waandaaji wa matamasha kutangaza bidhaa kama korosho n.k.

Kwa kuanzia, nadhani njia bora zaidi ya kumkwamua mama na Taifa, ni kutoa mafunzo ya ufundi yanayoendana na sanaa.

Kwa mfano wakati wa mavuno ya zao la korosho huko Kusini mwa Tanzania. Wakati huu waandaaji wa matamasha ya wajasiriamali wadogo wanaweza kuwekeza kwenye matangazo katika kujenga soko la sanaa na kuvutia wanunuzi wa bidhaa.

Baada ya muda itakuwa rahisi kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kuwekeza katika maeneo haya.

Biashara ni malengo. Hebu kwenye msimu ujao wa korosho tupeleke matukio ya Music Awards kule tukiwa na kaulimbiu ya “korosho ni maisha yangu”. Matangazo yafanywe na wajasiriamali wachakate bidhaa zao kwenye eneo la tukio.

Tutashangaa litakalotokea, maana hata Carribean walianza kwa kuuza ndizi kwenye maonesho ya ufukweni katika majira ya joto (Sunsplash) kwa gharama nafuu sana. Hivi sasa dunia nzima inashiriki tukio hilo kila mwaka na kuwapatia faida kubwa.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns

European Union Bans Air Tanzania Over Safety Concerns

Kampala — The European Commission added Air Tanzania to the EU Air Safety List, banning the airline from operating within European Union airspace. This decision follows the denial of Air Tanzania’s Third Country Operator (TCO) authorization by the European Union Aviation Safety Agency (EASA), citing significant safety deficiencies.

The EU Air Safety List includes airlines that fail to meet international safety standards. Commissioner Tzitzikostas emphasized the importance of passenger safety, stating: “The decision to include Air Tanzania in the EU Air Safety List underscores our unwavering commitment to ensuring the highest safety standards. We strongly urge Air Tanzania to take swift action to address these safety issues. The Commission has offered its assistance to Tanzanian authorities to enhance safety performance and achieve compliance with international aviation standards.”

Air Tanzania joins several African airlines banned from EU airspace, including carriers from Angola, the Democratic Republic of Congo, Sudan, and Kenya. Notable names include Congo Airways, Sudan Airways, and Kenyan carriers Silverstone Air Services and Skyward Express. The ban reflects the EU’s strict approach to aviation safety worldwide.

Source: allafrica.com

Continue Reading