Dar es Salaam. Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Daniel Makaka amepewa tuzo ya uandishi bora mwaka 2022 kwa upande wa magezeti kutokana na mchango wake katika kuandika habari zinazogusa jamii.
Tuzo hizo ambazo zimeandaliwa na Kampuni ya Eangle Entertainment zimetolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu Desemba 26, 2022 zikihusisha baadhi ya waandishi wa habari wa Wilaya ya Sengerema na watu wengine mbalimbali.
Makaka amepewa tuzo hiyo kutokana na habari yake aliyoiandika ambayo ilisaidia mwanafunzi aliyekuwa ameolewa na mwalimu na kushindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.
Habari hiyo iliyompa ushindi Makaka aliiandika mwaka 2018 na kuendelea kuifuatilia, ambapo baada ya habari hiyo, mwalimu huyo ambaye alimuoa mwanafunzi huyo mwaka 2016-18, alikamatwa na baadaye mwanafunzi alifanikiwa kujiunga kidato cha tano.
Hata hivyo, baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha sita alifaulu na sasa anaendelea na masomo Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza.
Akizungumza na Mwananchi baada ya kupokea tuzo hiyo, Makaka amesema kuwa tuzo hiyo imempa ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Nimefurahi kupata tuzo hii, itazidi kunipa ari ya kufanya kazi kwa bidi, ingawa kipindi kile wakati nimeibua sakata hilo wapo ambao walinichukia lakini kwa vile niliona ni habari inayogusa jamii niliamua kuendelea nayo” amesema Makaka na kuongeza
“Kama mwandishi nitazidi kuandika habari zinazoibua changamoto za wananchi ili waweze kupata suluhu za changamoto hizo”
Mkurugenzi wa Kampuni ya Eagle Entertainment ambao ni waandaaji wa tuzo hizo, Hasani Kuku amesema kuwa wanatoa tuzo hizo ili kuleta chachu ya uchapa kazi kwa wahabari kuibua mambo yanayoihusu jamii.
Tuzo hizo pia zimetolewa kwa watu mbalimbali akiwamo, mbunge wa Sengerema Hamis Tabasamu, aliyepata tuzo ya heshima sambamba na Mkuu wa wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga naye amepata tuzo ya heshima kutokana na mchango wao wa kusimamia vema ukusanyaji wa mapato na miradi ya maendeleo.
Wengine waliopata tuzo hizo ni wasanii bora ambapo msanii Lidia Juwakali ambaye alipata tuzo mbili, MC Wilimu Buhilwa aliibuka mshindi.
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal
Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.
The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading
High Court rejects Transworld’s application
The High Court in Dar es Salaam has struck out an application in which Transworld Aviation, a ground handler at the Abeid Aman Karume International Airport (AAKIA) was seeking permission to sue the Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA).Continue Reading
Karume faults lease of Zanzibar Islets
Diplomat Ali Karume has faulted the decision by the revolutionary government of Zanzibar to lease the islets that surround the islands of Unguja and Pemba to private developers saying it was absolutely not in Zanzibar’s national interests.Continue Reading