Mukansanga ‘kufungua mlango’ kwa marefa wa kike nchini Qatar

Mukansanga ‘kufungua mlango’ kwa marefa wa kike nchini Qatar

Mwamuzi  wa Rwanda Salima Mukansanga anatumai kuchaguliwa kuwa refa katika Kombe la Dunia la 2022 kutasaidia kufungua milango kwa marefa wengine wa kike wanaotaka kuwa wasimamizi wa mechi barani Afrika.

Mapema mwaka huu, alikuwa mwanamke wa kwanza kuchukua jukumu la kusimamia mechi katika Kombe la Mataifa ya Afrika miongoni mwa wanaume, huku mwaka jana akiongoza Michezo ya Olimpiki huko Tokyo.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 34 anatumai kuwa mmoja wa wanawake sita waanzilishi – pamoja na waamuzi wenzake Stephanie Frappart na Yoshimi Yamashita na waamuzi wasaidizi watatu – katika mashindano ya kimataifa ya wanaume kutatoa fursa kwa wanawake zaidi.

“Ni heshima na fursa kwa sababu haijawahi kutokea,” Mukansanga aliambia BBC Sport Africa.

“Inamaanisha kuwa utakuwa wa kwanza na utafungua milango kwa wanawake wengine, haswa wanawake barani Afrika.

“Unabeba mengi mabegani na unahitaji kubeba vizuri, ili wengine waone mlango uko wazi na wao pia waweze kupitia.

“Ni furaha na fursa ambayo wanawake wanapata. Ina maana fursa zipo – na ni juu yetu kuzichukua na kuwa na tija kutoka kwao.”

Mwamuzi huyo wa shirikisho la soka duniani Fifa tangu 2012, Mukansanga alikaidi kukataliwa mapema maishani akielekea kuchukua nafasi yake kwenye jukwaa kuu la michezo barani Afrika nchini Cameroon.

Akiwa msichana mdogo, aliambiwa kuwa umri wake ni mdogo kwa yeye kuwa sehemu ya timu ya taifa ya mpira wa vikapu ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 hivyo aliamua kujikita zaidi kwenye soka badala yake.

Muda mfupi akiwa mchezaji ulimuongoza kwenye tangazo la mafunzo ya waamuzi, ambapo – si mara ya kwanza – alichukua nafasi yake.

Aliwasiliana na FA ya Rwanda (Ferwafa) kuhusu kujiunga na kozi ya waamuzi mara baada ya kutoka shule ya upili lakini alikataliwa, pia kwa sababu ya umri wake.

Hivyo Mukansanga alijifundisha misingi ya uchezeshaji, Sheria za Mchezo, na hatimaye akapewa nafasi ya kusoma na waamuzi wengine wanaotaka kuwa waamuzi  na Ferwafa.

Mwanzo huo mgumu umemchukua tangu kuwa msimamizi wa michezo ya ligi ya wanaume katika nchi yake ya asili ya Rwanda, hadi Kombe la Mataifa ya Wanawake 2016, Kombe la Dunia la Wanawake 2019 na Olimpiki ya Tokyo iliyocheleweshwa.

Alisimamia mechi za wanawake za Timu ya GB dhidi ya Chile na Australia huko Japan, na mechi kati ya Uholanzi na Uchina.

Kisha akaweka historia  – akiwa katikati ya mechi ya ushindi wa Zimbabwe dhidi ya Guinea, ambapo alichezesha vyema, kwenye Kombe la Mataifa ya Wanaume nchini Cameroon mnamo tarehe 18 Januari.

‘Historia alioweka’

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

 
Maelezo ya picha,

Mukansanga alionyesha kadi sita za njano katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika ,miongoni mwa Wanaume mwezi Januari.

 

Baada ya kushughulikia kukataliwa kwa awali na mapokezi baridi katika uwanja unaotawaliwa na wanaume, Mnyarwanda huyo amekumbatia changamoto zinazoletwa na kazi hiyo.

“Tunapaswa kufanya kazi kwa bidii, haswa katika uwanja unaotawaliwa na wanaume. Unahitaji kuimarisha kazi yako maradufu,” alielezea.

“Na basi uwe na mapenzi na mchezo , bila mapenzi hayo utachoka halafu utaacha .Lakini hatutaki kuacha.

“Tunahitaji kuwa hatua moja mbele na tukifanya kazi pamoja, tufanikiwe na tupigane pamoja.”

Mkufunzi wa waamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf) Jerome Damon anaamini Mukansanga amepata mafanikio yake, baada ya kuchezesha sio tu hatua kubwa zaidi ya bara hilo bali pia Ligi ya Mabingwa Afrika miongoni mwa Wanawake.

“Ni hatua ya kushangaza kabisa – yuko katika nafasi ya kipekee ambapo yeye ni mmoja wa watu wachache wanaoweza kwenda Kombe la Dunia la wanaume na Kombe la Dunia la Wanawake wakubwa,” alisema Damon.

“Haijafanyika hapo awali, kwa hivyo inazungumzia pakubwa  juu ya waamuzi na maendeleo ya waamuzi barani Afrika.”

Damon, ambaye aliongoza katika Fainali nne za Kombe la Mataifa ya Afrika, anasema maafisa sita wa mechi za wanawake walioteuliwa kwa mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Dunia la wanaume walipata nafasi zao kwenye fainali – na kwamba lengo linabakia kwenye kazi yao badala ya jinsia yao.

“Tunapaswa kuelewa kuwa kuingizwa kwa wanawake kwenye mashindano si kwa sababu ni wanawake, ni kwa sababu ni wasimamizi wa mechi wenye uwezo, wa daraja la juu,” alisisitiza.

Kuwasaidia wanawake ‘kutazaa matunda’

.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

 
Maelezo ya picha,

Salima Mukansanga akiongoza michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2021

 

Mukansanga ataungana nchini Qatar na Frappart wa Ufaransa na Yamashita wa Japan, pamoja na waamuzi wasaidizi Neuza Back kutoka Brazil, Karen Diaz Medina kutoka Mexico na Kathryn Nesbitt kutoka Marekani.

“Tunasaidiana kwa sababu tunatoka mashirikisho tofauti lakini tunaenda kufanya kazi pamoja kwa ajili ya mafanikio ya wanawake,” Mukansanga alisema.

“Ikiwa mwanamke anamsaidia mwanamke mwingine, bila shaka utaona matunda.

“Kuna vizuizi, vikwazo na changamoto. Tutakabiliana na haya. Hakuna cha kufanya juu yao zaidi ya sisi kupigana tukiwa na mawazo madhubuti, kujitolea na ushiriki kamili – na kisha tutashinda.”

Mukansanga, ambaye pia alisimamia mchezo wa mpira wa miguu katika eneo la juu zaidi duniani kwenye Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania miaka mitano iliyopita, anajua kutakuwa na uchunguzi wa ziada nchini Qatar kutokana na umakini wa dunia kulenga michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka.

“Siku zote watu hawatafurahi na wewe, haswa timu inayopoteza. Hivyo ni juu yako kufanya unachotakiwa kufanya – kaa kwenye mstari, usitoke nje ya tafsiri ya Sheria za Mchezo, fuata kile mchezo unahitaji.

“Na kisha, mwisho wa siku, watu watasema, ‘Ndio, alikuwa sahihi’.”

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories