MRUNDIKANO WA MAKONTENA BANDARI YA ZANZIBAR WATISHIA UCHUMI

MRUNDIKANO WA MAKONTENA BANDARI YA ZANZIBAR WATISHIA UCHUMI

SWAHILI News Exclusive:

 

Mrundikano mkubwa wa makontena unaoonekana katika Bandari ya Malindi- Zanzibar unatajwa kuwa unaweza kuzorotesha juhudi za lujenga uchumi imara Visiwani humo.

Hali iliyopo sasa katika Bandari ya Malindi Zanzibar ni ya kuvunja moyo kwani Meli za mizigo zinachukua muda mrefu kupata ukuta kufunga gati Bandarini.

” Kama unavyoona pale kwenye ukuta, kwa sasa ni Meli moja tu Makontena inaweza kuingia kwa wakati mmoja” Alisema Mfanyakazi Mmoja wa Bandari Zanzibar ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Bandari ya Malindi Zanzibar iliyojengwa karne ya 19, ina uwezo wa kuhudumia makontena 80,000 tu kwa Mwaka ambapo wastani wa huduma inachukua siku tatu na hadi siku 15 kupakia mizigo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa muda wa kusubiri baharini kwa meli za mizigo ni baina ya siku tatu hadi siku kumi.

Meli nyingi zinazoleta mizigo katika Bandari ya Malindi Zanzibar ni kutoka Bandari ya Mombasa Kenya na baadhi Dubai.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Shirika la Bandari Zanzibar linakabiliwa na uhaba mkubwa wa vitendea kazi jambo ambalo pia linachangia sana huduma zisizoridhisha katika bandari hiyo.

Habari za uhakika zinaeleza kuwa Bandari hiyo kwa sasa ina Korongo moja tu maalum inayofayakazi ktk mfumo wa kisasa ( Automatic) ambapo tegemeo kubwa ni Korongo zinazoendeshwa kwa mikono na Korongo za Meli zenyewe.

Hali hiyo inachelewesha kazi na pia inasababisha gharama kwa Makampuni yenye kuleta meli.

Mfanyakazi mmoja wa Meli ya Mizigo anasema kwamba kama Shirika la Bandari wangekuwa na Kreni moja zaidi wangeweza kupakua Kontena 15 badala ya kontena 3 kwa saa.

Katika Bandari ya Malindi Zanzibar kwa sasa hakuna Matrekta Maalum ( Reach-Stackers).

Aidha, wafanyabiashara wanalalamikia pia makontena kupakiwa bila mpangilio maalum.

Changamoto nyengine inayotajwa na Wafanyabiashara ni pamoja na urasimu usiokuwa na ulazima katika kutoa vibali na nyaraka nyengine katika Kituo cha Huduma na hivyo kuchelewesha wateja kupata mizigo yao.

Juhudi za kumpata Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Nahaat Mahfoudh hazikuweza kufanikiwa kwani mara kadhaa simu yake imekuwa haipokelewi.

Mwisho.

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year’s Most Read News Stories