Read Story in English
MFUMKO WA BEI WAONGEZA UGUMU WA MAISHA ZANZIBAR & PEMBA ISLAND, TANZANIA
Mfumuko wa bei za bidhaa muhimu Zanzibar sasa unawaumiza wananchi wanyonge.
Mchele wa Mbeya daraja la kwanza unauzwa kg shilingi 3800 wakati Daraja la pili ukiuzwa kwa kg 1 shilingi 3500, daraja la tatu unauzwa kwa kilo 3000 huku daraja la mwisho kabisa Kg 1 shilingi 2800.
Bei hizo ni katika masoko ya Mwanakwerekwe C, Soko la Mombasa na katika maduka mengi ya Mjini na Mashamba.
Bei ya maharage aina ya soya Kg 1 ni shilingi 3500, maharage mengine Kg 1 ni shilingi 3200.
Kwa upande wa bei ya sukari nayo imepanda na kufikia Kg 1 ni kati ya shilingi 2400 hadi shilingi 2600 kutegemea na aina ya sukari.
” Hali imekuwa ngumu, kila kitu bei juu, vitu havinunuliki mchele wa Mbeya hauliki” Alilalamika Hamad Faki Jabu Mkaazi wa Darajabovu aliyekuwa akinunua bidhaa Soko la Mwanakwerekwe C.
Ukitembelea katika sehemu mbalimbali madukani, bei ya mchele aina ya Mapembe nao umepanda kutoka Kg 1 shilingi 1500 hadi Kg 1 shilingi 1800.
Unga wa ngano kwa sasa Kg 1 ni shilingi 2000. Wakati Mkate wa Boflo kipenzi cha Wazanzibari wengi unauzwa kwa shilingi 250 kutoka bei ya awali ya shilingi 200.
Katika mikahawa kadhaa ya Unguja na Pemba, bei ya chapati imefikia shilingi 700.
Kwa upande wa Mafuta ya kupikia nusu lita ilikuwa shilingi 1000 bei ya sasa ni shilingi 2000
Bei ya chipsi kavu nusu sahani ni shilingi 2000 ambaoo bei ya awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 1500.
Bei ya chipsi zege sasa imefikia shilingi 3000 kutoka shilingi 2500.
Tanzania inalenga mfumuko wa bei kubaki kati ya asilimia tatu hadi tano lakini kamati hiyo ilisema bei ya juu ya vyakula, nishati na mbolea katika soko la dunia inahatarisha kupanda kwa mfumuko wa bei siku zijazo.
Baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo bei zimepanda hivi karibuni ni pamoja na unga wa ngano. Hii ni kutokana na ukweli kwamba wazalishaji wa Tanzania wengi wao huagiza nafaka ya ngano kutoka nchi za Urusi na Ukraine ambayo mauzo ya nje yalitatizwa na vita kati ya nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya sera na utafiti wa umaskini ya Repoa, Dk Donald Mmari alielezea mfumuko wa bei wa sasa kama wa kimuundo, akimaanisha kuwa unasababishwa na usumbufu wa usambazaji uliosababishwa na Covid-19 na vita vya hivi majuzi vya Urusi na Ukraine.
“Usumbufu huu umeongeza mahitaji na hivyo kuongeza bei,” alisema Dk Mmari ambaye kitaaluma ni mchumi.
Alisema uhaba wa mvua nchini Tanzania katika msimu uliopita pia unaongeza uhaba wa chakula, hivyo kupandisha bei.
“Sera ya fedha ni hatua ya muda mfupi lakini katika muda wa kati tunahitaji kuhakikisha usambazaji wa bidhaa kama vile nafaka ya ngano na mafuta ya kula yanazalishwa vya kutosha nchini,” alisema.
Bei ya petroli pia imekuwa ikiongezeka tangu kuanza kwa vita vya Urusi na Ukraine mapema mwaka huu. Kwa mfano, bei ya petroli iliongezeka kutoka Sh2,480 kwa lita Februari 2022 hadi Sh3,410 mwezi huu wa Agosti, kulingana na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
Share this news
This Year’s Most Read News Stories
Zanzibar, Tanzania: Inflation hits five-year high
With Covid-19 and the war in Ukraine being blamed after inflation in Tanzania and Zanzibar rose to 4.5 this year and is climbing – the highest rate since November 2017Continue Reading
Zanzibar airport monopoly puts 600 jobs at risk
On September 14, 2022, the director general of ZAA issued a directive that gave Dnata Zanzibar Aviation Services Limited an exclusive access to the newly constructed Terminal III, barring other operators.Continue Reading
Tanzania’s path to 4Rs: The President Samia’s era
Tanzania has embarked on a journey of resilience, rebuilding, reconciliation, and reform under the leadership of President Samia Suluhu Hassan.Continue Reading