Mauaji ya mtoto Asimwe yanatia doa sifa ya Tanzania

Mauaji ya mtoto Asimwe yanatia doa sifa ya Tanzania

Mei 30, 2024, mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath, umri miaka miwili, alinyakuliwa kutoka kwa mama yake, kisha watu wakatoweka naye. Juni 17, 2024, ikiwa ni siku 18 tangu alipochukuliwa pasipo haki, Asimwe alikutwa mabaki ya mwili. Roho ilishaacha mwili, kisha mwili nao ulikutwa nusu. Baadhi ya viungo vilishanyofolewa.

Asimwe, mtoto mzuri, halafu mrembo. Kisa ulemavu wake, ndivyo wanaharamu wakaona hastahili kuishi. Unaweza kupata picha mtoto akilia na machozi yake yakawa sawa na wimbo “Machozi ya Samaki” wa Dk Remmy Ongala. Wauaji wa Asimwe, hawakujali machozi yake. Hawakuuthamini urembo aliokuwanao.

Peleka fikra zako machinjio ya wanyama, jinsi ng’ombe au mbuzi anavyokatwa kutenganishwa viungo. Rejea hata nyumbani, kuku anapitishwa kisu kutawanywa sehemu za mwili, aweze kupikwa. Fikra hizohizo zipeleke kwa Asimwe. Watu wamtoa roho na kumkata viungo mithili ya kitoweo.

Elewa hakukuwa na ukatili dhidi ya binadamu kabla ya binadamu. Ile siku Kaini alipomuua Abel, ukatili dhidi ya binadamu ndipo ulianzia. Asimwe, mtoto mwema asiye na hatia yoyote, amekutana na matokeo ya usajili wa ukatili dhidi ya binadamu.

Asimwe ni mtoto mwenye ualbino. Wapo watu wanaamini viungo vyake vitawapa bahati na utajiri, vyeo na nguvu ya mamlaka. Hizo ndizo hekaya nyuma ya mauaji ya watu wenye ualbino. Unamfikiria mama yake Asimwe, ni rahisi kuyahisi maumivu yake. Ni mwenye ualbino, lakini ni mwanaye. Alimtunza tumboni miezi tisa. Akajifungua na kumlea kwa miaka miwili, kwa upendo mkubwa. Iweje mwanaye atolewe uhai na kugawanyishwa viungo mithili ya bata?

Asimwe, alichukuliwa wilayani Muleba, Kagera. Ni mkoa wa Tanzania. Nchi ambayo inastahili kupewa hadhi ya kuwa makao makuu ya kidunia kwa matukio ya ukatili dhidi ya watu wenye ualbino. Kifo cha Asimwe kinaacha ujumbe kuwa Tanzania, ukiwa na ualbino haupo salama. Ulinzi haupo. Matukio yakitokea, kelele hupigwa na kisha ukimya hurejea. Halafu, katikati ya ukimya, maharamia hurejea kazini kuua na kukata viungo wenye ualbino.

Ngano ya ualbino

Nilipokuwa mdogo, nilisikia hekaya (myths) kuwa watu wenye ualbino hawafi, bali hutoweka. Ngano hiyo ilijengewa ushahidi wa kutokuwapo makaburi ya wenye ualbino. Nikajiuliza, wanapotea kwenda wapi? Kwa nini hawafi?

Ndani ya Msahafu imeandikwa: “Kila nafsi itaonja mauti.” Biblia inaweka mkazo wa kurejea mavumbini kwa kila mja. Kama vitabu vyote vitakatifu vinaeleza kuwa hatima ya kila binadamu duniani ni kifo, vipi watu wenye ualbino wawe wanatoweka?

Yalikuwa maswali ya utotoni, kujaribu kuumiza kichwa kuhusu hatima ya wenzetu wenye ualbino. Siku hizi sijiulizi tena swali hilo. Nafahamu wenye ualbino wengi waliuawa na ikavumishwa walipotea. Natambua pia makaburi ya wenye ualbino yalivamiwa na miili kutoroshwa.

Sababu ya kila kitu ni ushirikina. Waganga wenye kuchota watu ubongo wana hekaya yao kuwa viungo vya watu wenye ualbino, hususan mifupa, huwa na maajabu mengi. Eti, hukaribisha bahati na kujaza utajiri. Koo za Kiafrika nazo zina ngano yao, kwamba watu wenye ualbino hualika mikosi ndani ya familia.

Ngano zote mbili ni kichocheo cha mauji ya watu wenye ualbino. Wanawaua ili kupata viungo vyao, hususan mifupa, wakajenge bahati na utajiri. Wanawaua watu wenye ualbino kuondoa mikosi kwenye familia. Ripoti nyingi za mauaji ya wenye ualbino, zimethibitisha ndugu hadi wazazi kushiriki.

Mtu mwenye ualbino ni binadamu wa kawaida, ila ana ulemavu wa ngozi na macho. Hana umaalumu mwingine wowote, kiasi cha kuanza kuwawinda na kuwaua. Zilishapita nyakati Tanzania, watu wenye ualbino waliitwa “dili”. Eti, ukimuua na kumiliki viungo vyake, ni biashara yenye fedha nyingi.

Ualbino ni ulemavu. Kila bara, kisha nchi baada ya nchi, watu wenye ualbino wapo. Tofauti ni idadi. Juni 13, kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino. Juni 13, 2024, Umoja wa Mataifa (UN), walitoa ripoti yenye kuonyesha mtu mmoja kati ya 5,000, wana ualbino Kusini mwa Jangwa la Sahara, wakati mmoja kati ya 20,000, ndiyo wana ualbino Ulaya na Amerika Kaskazini.

Ripoti hiyo ya UN inabainisha Tanzania ndiyo inaongoza dunia kwa kuwa na watu wengi wenye ualbino, kwani mtu mmoja kati ya watu 1,400, wana ualbino. Maana yake, kwa hesabu ya watu milioni 62 waliopo, inaleta wastani wa watu 45,000, wanaoishi na ualbino Tanzania.

Zimbabwe ndiyo nchi yenye wastani mkubwa zaidi wa binadamu wenye ualbino, kwani katika kila watu 1,000, mmoja anaishi na ualbino. Idadi ya watu Zimbabwe ni milioni 16.3, hivyo wastani ni kwamba Zimbabwe ina watu 16,000 wenye ualbino.

Ripoti kuwa Tanzania ina watu wengi zaidi wenye ualbino kama ilivyotolewa na UN, inashabihiana kwa sehemu kubwa na utafiti uliofanywa na Shirika la Under the Same Sun, lenye makao yake makuu Canada. Shirika hilo ambalo limejikita katika utoaji wa elimu kuhusu ualbino, lilieleza katika kila watu 1,429 Tanzania, mmoja ana ualbino.

Aprili Mosi, 2014, Under the Same Sun, walitoa ripoti yenye kichwa “Reported Attacks of Persons with Albinism”, ikiwa na tafsiri ya mashambulizi yaliyoripotiwa ya watu wenye ualbino. Utafiti ulifanywa kwenye nchi 180 duniani.

Ripoti ya mauaji ilikuwa vifo 129 na mashambulizi 181, katika nchi 23, na zote ni Afrika.

Ukipitia idadi, Tanzania ina namba kubwa ya matukio ya mauaji. Sababu ni ileile; ushirikina. Taarifa zinasema migodini, wachimbaji huambiwa na waganga wapeleke viungo vya wenye ualbino ili wavune madini. Wafanyabiashara, kuna waliokata tamaa ya maisha, wanapoambiwa viungo vya wenye ualbino vitabadili nyota zao na kuwa zenye bahati, huanza msako.

Wasiwasi mkubwa upo kwa wanasiasa. Inadaiwa vipindi vya uchaguzi vinapokaribia, watu wenye ualbino huanza kupotea na hata kuuawa. Wengine hukumbana na mashambulizi, huishia kukatwa viungo. Eti, wanasiasa husaka vyeo kishirikina na viungo vya wenye ualbino ndiyo huwapa matokeo.

Lipo swali la kujiuliza; kwa nini vitendo vya kinyama dhidi ya watu wenye ualbino viibuke kila mwaka wa uchaguzi? Kati ya mwaka 2009 na mwaka 2010 nchi ilitikiswa na vitendo vya ukatili dhidi ya wenye ualbino. Rejea mwaka 2005 na mwaka 2000, yote hiyo ni miaka ambayo Uchaguzi Mkuu ulifanyika Tanzania. Na vipindi hivyo ukatili dhidi ya wenye ualbino ulikithiri, japo hali ilikuwa ya kutisha zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010.

Siku zote malalamiko yanaelekezwa kwa wasaka utajiri wa haraka na wachimba madini, wasaka vyeo maofisini, kuwa ni washirikina, na kwa imani yao na kwa mwongozo wa waganga wao, eti ndiyo watafanikiwa kwa haraka. Tunaweza kukubaliana kuhusu dhana hiyo. Hata hivyo? Swali; kwa nini hali inakuwa mbaya sana nyakati za karibu na uchaguzi?

Inawezekana kuna wanasiasa washirikina wa kutupwa. Pengine ndiyo sababu ya ukatili dhidi ya wenye ualbino nyakati za karibu na uchaguzi.

Hii ni mbaya, ni hatari, kwa sababu wanasiasa ndiyo tabaka linalotengeneza viongozi wa nchi, wanaotegemewa kuongoza, kuifanya nchi kuwa salama kuishi kila raia na hata wageni. Je, kiongozi aliyeshinda uchaguzi, akiwa na imani kuwa viungo vya wenye ualbino ndivyo vilimsaidia, ataweza kusimama kidete kukomesha ukatili dhidi ya watu wenye ualbino?

Si ajabu ndiyo maana ukatili dhidi ya wenye ualbino hauishi. Unaota mizizi. Hapo katikati palipoa. Mwaka huu (2024), unafanyika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani (2025), Uchaguzi Mkuu utachukua nafasi. Ghafla, matukio ya ukatili dhidi ya wenye ualbino yamerejea upya. Je, watu wanasaka vyeo vya kuongoza nchi kwa damu ya wenye ualbino? Taifa lipo salama kweli?

Ona sasa, mauaji ya mtoto Asimwe yanatia doa sifa ya Tanzania. Siku 26 kabla Asimwe hajachukuliwa na watu waovu, ilikuwa Mei 4, 2024, Katoro, Geita, mtoto Julius Kazungu, umri miaka 10, alinusurika kifo baada ya kushambuliwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mikononi.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms

President Samia Suluhu Hassan, has handed over a cheque of 354m/- from the National Bank of Commerce (NBC) as compensation to tobacco farmers, who were affected by hailstorms during the previous farming season in various regions across the country.

Handing over the cheque in Dodoma, the compensation is part of the crop insurance service provided by NBC in collaboration with the National Insurance Corporation (NIC).

Furthermore, President Samia has also handed over health insurance coverage to members of the Lindi Mwambao Cooperative Union based in Lindi Region, through the Farmers’ Health Insurance service provided by the bank in partnership with Assurance Insurance Company.

While visiting the bank’s pavilion at the Nanenane Agricultural Exhibition and being received and briefed by the bank’s Managing Director, Mr. Theobald Sabi, she said: “This crop insurance is one of the crucial solutions in ensuring farmers have a reliable income, without fear of challenges such as natural disasters, including hailstorms.

“I call upon all farmers in the country to make the best use of this important opportunity by accessing these kinds of insurance services. I also highly commend NBC and all the stakeholders participating in this programme.”

Elaborating further on the crop insurance service, the Minister of Agriculture, Hussein Bashe, stated that it will help to recover the loss farmers incurred, especially in various calamities beyond their control.

Citing them as floods, fires, and hailstorms, which have significantly affected the well-being of farmers and caused some to be reluctant to invest in the crucial sector, Mr Bashe added: “However, our President, this step by NBC is just the beginning, as this is the second year since they started offering this service, and the results are already visible.

“As the government, we promise to continue supporting the wider implementation of this service, with the goal of ensuring that this crop insurance service reaches more farmers.”

ALSO READ: NBC participates in TFF 2023/24 awards, promises to enhance competition

On his part, Mr Sabi said that the farmers who benefited from the compensations are from 23 primary cooperative unions in the regions of Shinyanga, Geita, Tabora, Mbeya, Katavi, and Kigoma.

He added: “In addition to these insurance services, as a bank, through this exhibition, we have continued with our programme of providing financial education and various banking opportunities to farmers, alongside offering them various loans, including loans for agricultural equipment, particularly tractors, to eligible farmers.:

At the NBC booth, President Samia also had the opportunity to be briefed on the various services offered by the bank to the farmers namely crop insurance and health insurance services.

There, the President had the chance to speak with some of the beneficiaries of the services, including the Vice-Chairman of the Lindi Mwambao Primary Cooperative Union, Mr. Hassan Mnumbe, whose union has been provided with a health insurance card from the bank.

Source: allafrica.com

Continue Reading