Makamba ataja mambo manne yanayombeba Rais Samia

Makamba ataja mambo manne yanayombeba Rais Samia

Tanga. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, amemtaja Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo manne yanayomfanya kuwa bora duniani.

Mbali na hilo, amesema Tanzania ina marafiki wengi, haina maadui kokote duniani na ndiyo maana mambo yanakwenda vizuri nchini.

Makamba ambaye ni mbunge wa Bumbuli, amesema hayo leo Jumamosi, Juni 8, 2024 katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika Lomera, Tanga Mjini.

Ni mkutano wa kuhitimisha ziara ya wajumbe wa sekretarieti ya CCM katika mikoa mitano ya Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga iliyoanza Mei 29, 2024.

Lengo ni kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi, kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuangazia maandalizi ya chaguzi ujao.

“Kuna mambo manne makuu ambayo ni matendo ya kiongozi, maneno ya kiongozi, mafanikio ya kiongozi na haiba ya kiongozi na huyu ni Rais Samia anayefanya tuendelee kuheshimika, kuaminika na kusifika duniani na ili haya yaendelee tuendelee kuiunga mkono CCM,” amesema.

“Ukiweka vigezo vyote hivyo, je, ni nani mwenye kauli na matendo na haiba ya kuheshimisha nchi yetu duniani upande wa pili (upinzani), simuoni na chini ya uongozi wa sekretarieti hii hakuna mwingine,” amesema.

Amempongeza Dk Nchimbi na wajumbe wote wa Sekretarieti ya CCM waliopata dhamana ndani ya chama hicho, kwani ni nafasi kubwa na za heshima zilizowahi kushindwa na viongozi waandamizi.

“Nafasi ya Katibu Mkuu ni nafasi kubwa na nyeti sana. Sisi tuna imani nanyi kwa sababu ninyi ni matokeo ya malezi ya CCM na tunaamini urithi wa chama chetu, uongozi bora, amani na utulivu mtaendelea kuubeba,” amesema.

Dk Nchimbi amesema katika kipindi cha miaka mitatu na nusu madarakani ya Rais Samia, mafanikio  kwenye sekta ya maji, afya, elimu na barabara ni makubwa.

Amesema Watanzania wanataka uaminifu, wanataka haki, upendo na kuwatumikia kwa kukitoa kwa moyo.

Katika ziara hiyo CCM imewapokea wanachama wa vyama vya siasa wakiwemo kutoka Chadema, ACT-Wazalendo na CUF, huku akiwakaribisha wengine akisema wote watakaojiunga watakuwa na haki sawa.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema ziara ya mikoa mitano imekuwa na mafanikio na wameona jinsi Ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa kishindo.

Makalla amesema kutokana na mafanikio makubwa, wamewaomba wananchi kuwaunga mkono wagombea wa CCM mara uchaguzi utakapowadia.

“Sisi na wenzetu tuna tofauti, tuna kile tulichokifanya. Ila wao hawana walichofanya,” amesema.

Alichosema Aweso, Ummy

Mbunge wa Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema kiongozi sahihi ni yule anayejua mahitaji ya watu wake.

“Dk Nchimbi anajua mahitaji ya wana-CCM na anajua mahitaji ya watu. Dk Nchimbi umeaminiwa na kweli imani hiyo inaonekana kila unapopita,” amesema.

“Sisi ambao tumepewa dhamana serikalini tutachapa kazi na hatutakuwa kikwazo kutekeleza ilani ya uchaguzi,” amesema.

Amesema changamoto kubwa ya Jimbo la Pangani kwa kipindi cha miaka mingi ilikuwa barabara ya Tanga- Pangani- Saadan lakini kwa sasa imejengwa na wananchi wanachekelea.

Amesema changamoto ya maji ilikuwa kubwa na ziara za viongozi huko nyuma walikuwa wanapokelewa na madumu ya maji lakini amefuatilia ziara za Dk Nchimbi katika mikoa 11, hajaliona hilo.

“Nikuhakikishie hadi kufika 2025 upatikanaji wa maji mijini utakuwa asilimia 95,” amesema.

Mbunge wa Tanga Mjini ambaye pia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema mambo mengi yamefanyika ikiwemo upanuzi wa Bandari ya Tanga na sasa anafanya kazi ya kutafuta wafanyabiashara kushushia mizigo bandari hapo.

Amesema katika sekta ya afya mambo mengi yamefanyika mkoani humo na nchi nzima kwa ujumla na kuanza kwa bima ya afya kwa wote kutaondoa changamoto kadhaa.

Mbunge wa Muheza, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema kuna matatizo na haja zinazofanana katika majimbo ya mkoa mzima wa Tanga.

Hata hivyo amesema: “Changamoto ni chache kuliko mafanikio. Kila mtu anaona na Rais Samia sisi tukimweleza anatuelewa.”

Mbunge huyo ambaye ni Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema mambo mengi yamefanyika na kuna mradi wa maji wa miji 28 ambao Waziri Aweso ameusimamia na Muheza ni miongoni mwa wilaya wanufaika na zaidi ya Sh40 bilioni zimetengwa na mwisho wananchi watanufaika.

Mbunge wa Mkinga, Dustan Kitandula ambaye ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,amesema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ndani ya jimbo lake ni mkubwa kwenye sekta ya maji ambapo zaidi ya Sh42 bilioni zimetolewa, kwenye elimu sekondari nne zimejengwa, madarasa  ujenzi wa miundombinu mbalimbali.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Karume faults lease of Zanzibar Islets
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

Karume faults lease of Zanzibar Islets

Diplomat Ali Karume has faulted the decision by the revolutionary government of Zanzibar to lease the islets that surround the islands of Unguja and Pemba to private developers saying it was absolutely not in Zanzibar’s national interests.Continue Reading

Popular
Chief Editor

Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal

Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.

The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading