Mahitaji yapandisha bei ya umeme Zanzibar

Mahitaji yapandisha bei ya umeme Zanzibar

Mahitaji yapandisha bei ya umeme Zanzibar

Unguja. Wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), ikitangaza bei mpya elekezi kwa watumiaji wote wa umeme Zanzibar, imetaja sababu ya mabadiliko hayo ni kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya umeme Visiwani Zanzibar.

Mabadiliko hayo yamekuja ikiwa ni miaka tisa tangu yafanyike mabadiliko ya mwisho mwaka 2016 na bei hizi mpya zitaanza kutumika Januari 20, 2025 kwa makundi yote manne ya utumiaji nishati hiyo.

Kwa mujibu wa Zura, ilipokea maombi ya kubadilisha bei za umeme kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya umeme Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Zura jana jioni, bei hizo zimetoa punguzo la Sh190 kwa watumiaji wadogo ambao walikuwa wakilipa Sh480 kwa uniti kila wanapovuka matumizi ya uniti 50 kwa mwezi,  ambapo kwa sasa watalipa Sh290 badala ya Sh480 wakivuka uniti hizo.

Hata hivyo, katika kundi hili ambalo ndio la watu wa chini kabisa kwenye matumizi, gharama ya kununua uniti moja imeongezeka kutoka Sh79 hadi Sh84 sawa na ongezeko la Sh5.

Meneja kitengo cha Uhusiano  Zura, Mbaraka Haji amesema tozo ya kutoza huduma kwa watumiaji hawa wadogo kuanzia uniti 0 hadi 50 itaendelea kuwa Sh2,100.

Wateja wenye matumizi ya kawaida, uniti moja hadi 1,500 bei ya kununua uniti moja imepanda kutoka Sh266 hadi Sh280 huku kila uniti inayoongezeka ikitoka Sh288 hadi Sh310 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa Sh2,100. 

“Hawa ni wateja wenye matumizi ya kawaida hususani majumbani  wenye biashara ndogondogo, maduka, mabango, waliounganishwa katika msongo mdogo  wa umeme kwenye njia moja (230V) na njia tatu (400V),” amesema.

Kwa wateja waliounganishwa katika msongo mdogo  na msongo wa kati wa umeme, bei ya uniti moja imeongezeka kutoka Sh206 hadi Sh217 huku bei ya mahitaji ya juu (kila uniti inayoongezeka) itabaki ile ya wali Sh16,000 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa bei ileile ya Sh10,500.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, wateja waliounganishwa katika msongo mkubwa wa umeme bei ya uniti moja itakuwa Sh178 kutoka Sh169, bei ya mahitaji ya juu itaendelea kuwa Sh16,000 na bei ya tozo itaendelea kuwa ilile ya Sh150,000.

Mbaraka amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanya tathmini ya kina ikiwemo kukutana na wadau ili kupata maoni yao.

Wananchi wafunguka

Wakati bei zikibadilika, baadhi ya wananchi wameonekana kutokuwa na ufahamu, huku wakiomba kupewa elimu zaidi kuhusu mifumo hiyo.

“Hapa watu wengi watakuwa wanalipia gharama kubwa bila kujua na ndio maana kuna wakati mtu ananunua umeme anaona kidogo. Nasema hivi kwa sababu watu hawaelezwi kama kuna kiwango wanalipia ikiwa zitaongezeka uniti kwa mwezi,” amesema Haji Mbarok, mkazi wa Magogoni.

Mwananchi mwingine, Rahma Abdul amesema licha ya kupunguza kiwango cha uniti zinazozidi, bado mamlaka isingeongeza kiwango cha uniti katika matumizi ya kawaida.  

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’
Top News
Chief Editor

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Africa: Rwanda Gets a Grip Of Marburg, But Mpox ‘Not Yet Under Control’

Monrovia — The Rwanda Minister of State responsible for Health, Dr. Yvan Butera, cautioned that while the country is beginning to see positive signals in its fight against the Marburg virus, the outbreak is “not yet over”. He, however, expressed hope that  “we are headed in that direction”. The minister said the epidemiology trend, since the disease was first discovered in the country more than a month ago, is moving towards fewer cases.

Dr. Butera, who was giving updates during an online briefing yesterday, said in the past two weeks, only two deaths were recorded while 14 people recovered from the disease. He said Rwanda was expanding its testing capacity with 16,000 people already inoculated against the disease.

The priority right now, Butera said, is “rapid testing and detection”.

Marburg is a highly virulent disease transmitted through human-to-human contact or contact with an infected animal. The fatality rate of cases, which has varied over the period, is more than 50%, according to the World Health Organization.  WHO said the highest number of new confirmed cases in Rwanda were reported in the first two weeks of the outbreak. There’s been a “sharp decline” in the last few weeks, with the country now tackling over 60 cases.

At Thursday’s briefing, a senior official of the Africa Centers for Disease Control, Dr. Ngashi Ngongo, said mpox – the other infectious disease outbreak that countries in the region are fighting – was been reported in 19 countries, with Mauritius being the latest country to confirm a case. He said although no new cases have been recorded in recent weeks in several countries where outbreaks occurred previously –  including Cameroon, South Africa, Guinea, and Gabon – Uganda confirmed its first Mpox death. This, he said, is one of two fatalities reported outside Central Africa.

Dr. Ngashi revealed that there was an increase in cases in Liberia and Uganda. He said mpox cases were still on an upward trend.

“The situation is not yet under control.”

Source: allafrica.com

Continue Reading