Mahakama yabatilisha hukumu kesi ya State Oil na Benki ya Equity

Mahakama yabatilisha hukumu kesi ya State Oil na Benki ya Equity

Dar es Salaam: Mahakama ya Rufani imebatilisha hukumu iliyoipa ushindi kampuni ya State Oil Tanzania katika kesi ya mgogoro wa malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 18.64 milioni (zaidi ya Sh47 bilioni) dhidi ya Equity Bank Tanzania Limited (EBT) na Equity Bank Kenya Limited (EBK).

Badala yake Mahakama hiyo imeamuru kesi hiyo ya kibiashara namba 105 ya mwaka 2020 iliyofunguliwa na State Oil Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara dhidi ya Benki ya Equity tawi la Tanzania, ianze upya kusikilizwa.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu, Rehema Mkuye (Kiongozi wa jopo), Abraham Mwampashi na Zainabu  Muruke, Alhamisi, Mei 16, 2024, kutokana na rufaa iliyokatwa na benki hizo,  EBT na EBK.

Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kasoro katika mwenendo wa kesi hiyo, kuwa mahakama hiyo iliendelea kusikiliza na kuamua kesi hiyo bila hati ya madai kufanyiwa marekebisho baada ya wadaiwa kuongezeka kutoka mmoja na kuwa wawili.

Kutokana na kasoro hiyo ya kutotolewa amri ya kurekebisha ya hati ya madai, Mahakama hiyo imesema kuwa katika mazingira ya kesi hiyo kutotolewa amri ya marekebisho ya hati ya madai baada ya EBK kuongezwa katika kesi kama mdaiwa wa pili, ilikuwa ni kasoro kubwa isiyorekebishika.

Mahakama hiyo imesema kuwa kasoro hiyo inavunja masharti ya lazima ya Amri ya 1 Kanuni ya 10 (4) ya Sheria ya Kanuni za Madai (CPC) na kwamba pia kumeathiri mwenendo na vilevile hukumu iliyotokana na mwenendo huo.

Hivyo kwa mamlaka yake ya kimapitio chini ya kifungu cha 4 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Rufaa (ilivyorejewa mwaka 2019), imetangua sehemu ya amri ya Mahakama Kuu ya Desemba 10, 2020 ya kuelekeza EBK kuwasilisha maelezo ya utetezi wa maandishi.

“Na tunabatilisha mwenendo wote uliotokana na amri hiyo,” imesema Mahakama ya Rufani,  katika uamuzi wake ulioandikwa na Jaji  Mwampashi kwa niaba ya jopo la majaji hao na kuhitimisha:

“Pia tunatengua hukumu na kurejesha kumbukumbu (jalada) za kesi ya kibiashara namba 105 ya mwaka 2020, Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara kwa ajili ya kesi kusikilizwa upya baada ya kukidhi matakwa ya Amri ya 1 Kanuni ya 10 (4) ya CPC.”

Awali, State Oil ilifungua kesi hiyo dhidi ya EBT, kama wakala wa EBK, kufuatia mgogoro wa malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 18,640,000 ambazo EBK inaidai State Oil.

Kabla kesi hiyo kuanza kusikilizwa, mawakili wa EBT waliziomba mahakama iamuru EBK nayo iunganishwe katika kesi hiyo kama mdaiwa wa pili kwa kuwa nayo Ina maslahi katia kesi hiyo.

Mahakama ilikubali ombi hilo na Desemba 10, 2020 ikaamuru EBK iunganishwe katika kesi hiyo, pia ikaamuru EBK nayo iwasilishe maelezo yake ya utetezi wa maandishi.

Kwa hiyo wadaawa katika kesi hiyo waliongezeka kutoka wawili mpaka watatu, mdai mmoja yaani State Oil na wadaiwa wawili yaani EBT na EBK.

Hata hivyo, Mahakama Kuu haikuamuru hati ya madai ifanyiwe marekebisho ili kuakisi mabadiliko hayo ya wadaawa yaani kuitaja EBK katika hati ya madai kama mdaiwa wa pili.

Badala yake iliendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo kwa kutumia hati ya madai ya awali ya wadaawa wawili na ikaipa ushindi State Oil, ndipo benki hizo zote mbili EBT na EBK zikakata rufaa Mahakama ya Rufani kuupinga hukumu hiyo.

Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Aprili 13, 2024, lakini kabla ya kuanza usikilizwaji Mahakama iliibua kasoro hiyo.

Ilihoji uhalali wa Mahakama Kuu kuendelea na usikilizwaji na hatimaye kutoa hukumu bila kwanza kuamuru kufanyika kwa marekebisho ya hati ya madai baada ya mabadiliko ya wadaawa (kuongezeka mdaiwa mmoja).

Wakijibu hoja hiyo, mawakili wa pande zote mbili, Mpaya Kamara na Timon Vitalis wanaowawakilisha warufani (benki hizo) na Frank Mwalongo anayeiwakilisha State Oil, pamoja na mambo mengine waliieleza mahakama kuwa, haikuwa muhimu kufanya marekebisho hayo kwa kuwa hayakuuathiri upande wowote.

Hivyo waliiomba mahakama kutumia kanuni ya kutozingatia kasoro za kisheria ambazo hazigusi mzizi wa kesi (overriding objective principle) na badala yake iendelee kusikiliza rufaa hiyo.

Hata hivyo Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake huo haikushawishika na hoja za mawakili hao wa pande zote badala yake imeamua kuwa kasoro hiyo ilikuwa ni nzito.

“Baada ya kufikiria yote ni uamuzi wetu kwamba kwa kuzingatia asili ya mgogoro baina ya wadaawa hati ya madai ilipaswa kurekebishwa kukidhi matakwa ya lazima ya Amri ya 1 Kanuni 10 (4) ya CPC” imesema Mahakama.

Imefafanua kuwa kwa kuwa hati ya madai haikurekebiahwa basi State Oil haikuwa na kesi au madai dhidi ya EBK na kwamba mbali na madai kinzani iliyoyatoa katika maelezo yake ya utetezi wa maandishi, EBK iliishia kutetea kesi iliyooelekezwa kwa EBT tu.

“Kwa kuzingatia asili ya mgogoro baina ya wadaawa na kiasi cha pesa kinachohusika kuwa kikubwa, hitaji la usikilizwaji sawa ambalo ni kwa mujibu wa matakwa ya lazima ya taratibu za kisheria, ni jambo ambalo halikupaswa kupuuzwa”, imesema Mahakama ya Rufani na kusisitiza.

“Katika kesi hii si tu suala la wadaawa kutoathirika bali pia ni kwa maslahi ya haki kwamba taratibu za lazima za kisheria zinapaswa kuzingatiwa.

Historia ya mgogoro

Mwaka 2018 State Oil ilichukua mkopo wa Dola za Marekani 18.64 milioni kutoka kwa mkopeshaji wa nje, kampuni ya Lamar Commodity Trading DMMC of Dubai kwa udhamini wa EBK, huku na yenyewe ikiweka dhamana zake kwa EBK, chini ya usimamizi wa EBT.

State Oill ilipuuza kulipa mkopo huo hivyo mdhamini wake EBK ikalazimika kuulipa, na hivyo yenyewe ndio ikabaki inaidai kampuni hiyo.

Baada ya muda iliopewa kulipa deni hilo kuisha bila kulipa EBT ilipoidai State Oil kwa niaba ya EBK kama wakala wake aliyepewa dhamana hiyo, ndipo State Oil ilipokimbilia mahakamani.

Katika kesi hiyo kampuni hiyo iliiomba mahakama iiamuru EBT iirejeshee hati za mali ilizokuwa imeziweka dhamana, kwa ajili ya kupata udhamini kutoka kwa EBK, huku ikidai kuwa haidaiwi na benki hizo, kwa madai kuwa EBK haikuidhamini kupata mkopo huo.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo mwakilishi wa kampuni ya Lamar iliyotoa mkopo huo alieleza kuwa iliipa State Oil mkopo huo baada ya kudhaminiwa na EBK na kwamba ukishindwa kuurejesha, hivyo mdhamini wake, EBK akaulipa.

Hata hivyo mahakama hiyo katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Stephen Magoiga Oktoba Mosi, 2021, alikubaliana na madai ya State Oil, kuwa ilikuwa imeshalipa deni lake lote na hivyo benki hizo hazikuwa na madai dhidi yake.

Hivyo Jaji Magoiga aliamuru hati za mali zote zilizokuwa zimewekwa dhamana na State Oil, zinashikiliwa zirejeshwe kwa kampuni hiyo.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

Tanzania: Exim to Raise Fund for Mental Health Facilities Upgrades

EXIM Bank to raise 300m/- over the next three years for financing essential services and infrastructure upgrades in mental health facilities.

The bank’s Head of Marketing and Communications Stanley Kafu unveiled this when introducing Exim Bima Festival 2024 as a platform for bringing together individuals, organisations and various sectors for raising the funds.

“Exim’s initiative aligns with the government’s broader goals to ensure that every citizen has access to quality healthcare, including mental health services,” he said.

The initiative, which is one of the events for celebrating the bank’s 27th anniversary is scheduled for Wednesday this week in Dar es Salaam.

Mr Kafu highlights that this year’s festival is not only about raising awareness of the importance of insurance in the society but also focuses on enhancing access to mental health services and improving the overall well-being of the nation.

Statistics from the Ministry of Health shows a staggering 82 per cent increase in mental health cases over the past decade.

Mental cases have risen from 386,358 in 2012 to 2,102,726 in 2021, making the need for mental health services more urgent than ever.

ALSO READ: NBC’s Saving Campaign Empowers Customers Nationwide

Unfortunately, the country’s ability to address this growing challenge is hindered by a shortage of mental health professionals, infrastructure, medical equipment and essential medication.

For example, out of the 28 regions in the country, only five have facilities that provide adequate mental health services.

The most affected group is the youth aged 15 to 39, who represent the nation’s workforce, underscoring the need for intensified efforts to safeguard this generation for Tanzania’s future well-being and development.

Mr Kafu said by improving mental health services, Exim aims to contribute to the creation of a network of communities that can access care quickly and affordably.

Exim Insurance Department Manager Tike Mwakyoma said they are appreciating the support from partners in the insurance industry, who have stood by them since the last festival.

“Let’s continue this unity for the development of all Tanzanians and our nation as a whole,” the manager said.

Source: allafrica.com

Continue Reading