Magonjwa nyemelezi yanavyowatesa vijana wenye VVU

Magonjwa nyemelezi yanavyowatesa vijana wenye VVU

Magonjwa nyemelezi yanavyowatesa vijana wenye VVU

Dar es Salaam. Wakati dunia ikiadhimisha siku ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo Januari 30, 2025 nchini Tanzania, hali ya waviu wasiotambua hali zao mpaka kufikia hatua ya kupata magonjwa nyemelezi (Ukimwi) bado ipo huku vijana wakitajwa kuathirika zaidi.

Magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU) hatua ya juu kitaalamu yakitambulika kama Advanced HIV Diseases au AHD, hivi karibuni yameingizwa katika orodha ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), mviu atahesabika amepata AHD ikiwa kiwango cha kinga mwili au CD4 kitashuka mpaka chini ya 200 inayoitwa hatua ya tatu au ya nne ya ugonjwa, ikijumuisha wanaokuja kupata matibabu kwa mara ya kwanza wakiwa hawajaanza matibabu ya kufubaza makali ya VVU (ARV) na wale wanaorejea kwenye matibabu baada ya kukatisha tiba.

Wakati changamoto hiyo ikitajwa, imani za dini, tabia ya kujitibu na imani za kishirikina vimetajwa kuwa chanzo kwa vijana wengi kutofika mapema katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa uchunguzi, huku wengi wakifikishwa na wazazi, ndugu wakiwa na dalili za Ukimwi.

Simulizi za wahanga

Ni zaidi ya mshtuko! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wazazi wa Johari Johnson (si jina lake halisi) kuelezwa na daktari kuwa binti yao alikuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

“Sikuamini. Nilimpigia mume wangu akaja hosptali na wakati huo sikujua nitamweleza vipi anielewe, binti yangu wakati huo alibainika pia na kifua kikuu (TB),” anaanza kusimulia mama wa Johari ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Mama wa Johari amesema hili lilikuwa jaribio pekee, ili yeye na mumewe wapewe upya majibu mbele ya mtaalamu wa afya.

Johari (20) alibainika kuwa na maambukizi ya VVU baada ya kuugua kifua kwa muda za miezi miwili huku uzito wake ukizidi kupungua.

“Mwanangu alikua msiri sana, lakini alipofikia hatua ya kurudi nyumbani na kuacha masomo hali yake ilikuwa imedhoofu sana, nilihisi ni kifua pekee lakini baada ya vipimo zaidi tuliambiwa CD4 zake zimeshuka sana na hivyo alianza kutibiwa kifua kikuu na kuanzishiwa dawa.

“Alikuwa na afya nzuri kilo zake zilikuwa 64 wakati wote. Lakini aliporudi nyumbani wakati ule nakumbuka alikuwa amefikisha kilo 49,” amesema.

Johari anasema hakuwahi kudhani kama ana maambukizi ya VVU na alipoanza kuumwa miezi sita nyuma kabla ya kuzidiwa alikuwa akijitibu kwa dawa za famasi kabla ya kuamua kwenda hospitali.

“Nilianza kupata vipele vidogo vidogo nikahisi losheni niliyoitumia. Nilipewa vipodozi vingine lakini hali haikutulia. Nikahisi mabadiliko ya mwili.

“Baadaye nikaanza kuona sina hamu ya kula, na ghafla nikaanza kupungua uzito. Nilidhani sababu sipendi kula lakini kama unavyojua vyuoni nikajikuta sasa napendelea vyakula vile ninavyoona ninaweza kula.

“Nilikuwa na kilo 63 mpaka 64 lakini ilifika hatua mpaka nguo zilianza kunivuka. Wengi walidhani hali yangu ilitokana na kusoma sana lakini haikuwa hivyo, nikaanza kupata wasiwasi. Miezi michache baadaye nilianza kukohoa kifua kisichopona hata nilipoenda kupata tiba famasi. Ilibidi niende hospitali nako walinipa dawa za kunywa antibaotiki,” anasimulia.

Johari anasema hakupata nafuu na alianza kukohoa mfululizo mpaka miezi miwili, hali hiyo ilimfanya niamue kurudi nyumbani kwa ajili ya matibabu.

Kisa cha Johari, kinaungwa mkono na Mratibu wa Kitengo cha huduma za tiba na matunzo ya Ukimwi CTC katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Amana, Dk Joshua Kajula anayesema changamoto hiyo huwakuta baadhi ya vijana.

Amesema mwaka 2023 mpaka 2025 wagonjwa wote kwa ujumla walikuwa 390 ambao walianza huduma waliokutwa na Advanced HIV Disease walikuwa 170 watu wazima na watoto ambao ni chini ya miaka 24  walikuwa 42 na ambao walikuwa na ugonjwa huo ni 12.

“Kwanza wengi wanakuwa wamejipima na kugundua hali zao kiakili, wengi wanaogopa majibu. Anaumwa lakini kwenda kupima anaogopa, hivyo anajikuta anakwenda kwa namna mbili.

“Wwingine atapita kwenye kila aina ya waganga, hataanzia hospitali anaenda kwa waganga wa kienyeji anatibiwa famasi kwa kununua dawa na wengine wanakwenda kwenye imani za kidini huko kwa manabii mbalimbali.

“Wanapoona imeshindikana na wengi unakuta hajaja mwenyewe ameletwa na ndugu,  wamekuja naye  akifika hospitali hajiwezi kwahiyo ndiyo tunaanza kumtibu na kuona namna ya kupandisha CD4 zake,” amesema Dk Kajula.

Kwa upande wa watoto amesema wanawatambua mpaka miaka 24 kuanzia mwaka sifuri, huku akisema wengi wamepata maambukizi ukubwani na wengine wamezaliwa nao kutoka kwa wazazi.

Amesema baadhi ya watoto wazazi wengine wameshindwa kuwaambia watoto hali zao za kiafya hivyo wakifariki mtoto hapati tiba na hivyo kupata magonjwa nyemelezi.

“Wengine baba, mama wamefariki wapo kwa bibi na babu, kwahiyo bibi hasa ndiyo anakabaki na watoto hawana muda wa kuwapa huduma, hivyo akija anakuja na hali mbaya.

Mtu anakuja na kifua kikuu na wengine wanakuja tayari wana saratani ya ngozi.

“Wiki hii nilimuona mmoja ana saratani ya ngozi kabisa na alienda kupima miaka mingi nyuma,  alipoambiwa amekutwa na virusi vya ukimwi  akakataa akasema yeye hana ni mlokole.

“Akaoa. Anapoenda kuoa wakaenda kupima na mke wake, akakutwa ameambukizwa na mwanamke hana maambukizi. Mwenzake akajua kabisa akamwambia yeye anahangaika na maisha ya ndoa,” amesema.

Dk Kajula amesema mgonjwa huyo amerudi na dalili ya  saratani ya ngozi.

“Nilipomuona moja kwa moja nikawaambia tukampime, wakanidanganya danganya, baadaye tukaenda kuwapima tukakuta tayari ana saratani ya ngozi lakini tukakuta ameathirika na kumpima  mwanamke naye ameshaathirika,” amesema na kuongeza;

“Tukamrudia mwanamke tunamwambia labda tumpe ushauri aanze dawa, naye akasema ‘hapana hakuna shida Yesu atahangaika nayo  situmii chochote, kwa sababu hata mwanzo nilijua naolewa na mwanaume ameathirika, mimi nilisema hii ni ndoa na mimi ndoa yangu nilisema sitatumia na sitatumia’ alitujibu hivyo tukamuacha.”

Dk Kajula amesema huo ni mfano na mviu huyo amegoma kutumia dawa, lakini atakuja kuletwa na ndugu wakati amezidiwa.

Amesema wagonjwa wa aina hiyo huwa wanakutana nao sana, kwa sababu hawana uwezo pia wa kuwalazimisha kuanza dawa, hufikishwa kituo cha afya akiwa katika hatua mbaya.

“Kwa mfano toka mwaka 2023/24 walikuwa 42 lakini kati yao 12 waliokutwa na ugonjwa wa juu wa Ukimwi walikuwa na kifua kikuu TB wengine walikuja wakiwa CD4 ambazo zimefikia hatua mbaya na wengi waliletwa na ndugu lakini tukiwaangalia kwa status za HIV hatua ya juu ya ugonjwa yaani hatua ya nne na tatu,” amesema Dk Kajula.

Hata hivyo Dk Kajula anasema wagonjwa wenye advanced HIV deseases wengi huwa wanakuwa hawako vizuri, kiafya na afya ya akili.

Kwa mujibu wa WHO upimaji wa kiwango cha seli za CD4, ingawa hauhitajiki tena ili kuanzisha matibabu, bado ni nyenzo muhimu kwa kubaini watu walio na AHD.

Watoto wote walio chini ya miaka mitano wanachukuliwa kuwa na AHD kwa sababu ya hatari yao kubwa ya maendeleo ya ugonjwa na vifo.

Watu wenye AHD wako kwenye hatari kubwa ya kifo, hata baada ya kuanza ARV,  hatari hii huongezeka kadri kiwango cha CD4 kinavyopungua.

Sababu za kawaida za magonjwa makali na vifo ni kifua kikuu (TB), maambukizi makali ya bakteria na ugonjwa wa meningitis unaosababishwa na fangasi wa cryptococcus.

Ili kupunguza magonjwa na vifo kwa watu wanaopatikana na AHD, WHO inapendekeza kutoa kifurushi cha afua zikiwemo uchunguzi, matibabu na kinga dhidi ya maambukizi makuu nyemelezi, kuanzisha ART kwa haraka na kuimarisha msaada wa ufuasi wa matibabu. Kifurushi cha AHD kinalenga kupanua upatikanaji wa dawa na vipimo muhimu vya kushughulikia sababu za kawaida za magonjwa na vifo.

WHO ina mwongozo maalum kwa watoto na vijana wenye ugonjwa wa VVU hatua ya juu na kwa usimamizi wa kifua kikuu, ugonjwa wa cryptococcal meningitis, histoplasmosis, na hali za ngozi na mdomo zinazohusiana na VVU.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

‘No Marburg Confirmed In Tanzania’, But Mpox Remains ‘Public Health Emergency’

Monrovia — The Director General of the African Centers for Disease Control, Jean Kaseya, has said the center stands ready to support Tanzania and other countries in the region where suspected cases of the infectious Marburg Virus Disease have been identified. The World Health Organization earlier this week issued an alert warning of a possible outbreak in the country, although the Tanzanian Health Ministry has said tests conducted on available samples did not show the existence of Marburg in the East African nation.

“As of the 15 of January 2025, laboratory results from all suspected individuals were negative for Marburg Virus,” Tanzanian Health Minister Jenista Mhagama said in a statement. This would have marked the country’s second experience with the highly infectious disease that recently killed over a dozen people in neighboring Rwanda. Tanzania previously reported an outbreak of Marburg in 2023 in the  Kegara region, said to have been the epicenter of the new suspected cases.

At the Africa CDC online briefing on Thursday, Kaseya also said another infectious disease, Mpox, “remains a public health concern”. He said that while in December 2024, the disease had afflicted 20 countries, a new country – Sierra Leone – has been added to the number after recent outbreak there. Sierra Leonean health authorities said on January 10 that two cases of Mpox had been confirmed in the country and dozens of contacts are being traced.

With thousands of confirmed cases of Mpox across Africa and more than 1000 people having died of the disease  – mainly in Central Africa – Kaseya emphasized the need to increase testing, a theme he’s heralded before. The Africa CDC boss said over the next few months the continental health watchdog will deploy additional epidemiologists and community health workers to areas considered hot spots of infectious diseases in the region.

Source: allafrica.com

Continue Reading

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

CCM ready to task state organs on Zanzibar Airport deal

Ruling party Chama Cha Mapinduzi-Zanzibar has said it is ready to task state organs to investigate some of the claims against its government that have been raised by opposition politicians on the Abeid Amani Karume International Airport (AAKIA).Continue Reading