Kanisa jipya la Anglikana laanzishwa Tanzania

Kanisa jipya la Anglikana laanzishwa Tanzania

Dar es Salaam. Kanisa jipya la Anglikana lijulikanalo kama Episcopal Anglican Province Tanzania linatarajiwa kuzinduliwa Septemba 15 Kongwa mkoani Dodoma.

Kuzinduliwa kwa kanisa hilo kunatajwa kutawapa chaguo waumini wote wa Anglikana kuamua waabudu kanisa lipi kati ya hili jipya na lililopo nchini.

Kuanzishwa kwa kanisa hili kunatajwa kurejesha na kusimamia misingi ya Kanisa la Anglikana kama ilivyokuwa miaka 60.

Akizungumza na wanahabari, Askofu wa kanisa hilo, Elibariki Kutta amesema kuanzishwa kwa kanisa jipya hakumaaanishi kuwa kanisa la Anglikana limemeguka, bali linatanua wigo kwa waumini kuamua wasimame na imani ipi.

“Anglikana haijameguka. Ni moja, ila uhuru wa wewe unataka kuwa na mtazamo gani au njia ipi katika maono yako,” amesema Kutta.

Amesema kuanzishwa kwa kanisa hilo haimaanishi kuwa wameondoka Anglikana lakini wanajaribu kusimama katika misingi ya kanisa mama la Kianglikana.

“Sisi ndiyo tunataka kushikilia hiyo misingi, tunataka kubaki na kutunza imani iliyo safi ya kanisa la Anglikana na si mpya ni ileile iliyopanda uanglikana tangu kabla ya uhuru hadi mwaka 1965 na si kweli kuwa tunapinga imani iliyopo, bali tunakuza imani hii,” amesema Kutta.

Mbali na hilo, Kutta amesema ujio wa jimbo hilo utasaidia Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kupitia sadaka za waumini wanazotoa katika maeneo wanayoabudu.

Amesema kupitia sadaka hiyo waumini watakuwa na uwezo wa kuamua nini wafanye kwa ajili ya kuboresha huduma katika maeneo yao, ikiwemo kuanzisha vituo vya afya na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

“Miradi yetu itamilikiwa na watu waliopo katika maeneo hayo, sehemu ambayo kutakuwa na kanisa letu tutahakikisha jamii inafaidika kupitia huduma mbalimbali za kijamii zitakazoanzishwa na wao watakuwa wasimamizi wakuu,” amesema Kutta.

Amesema wao wanaamini kuwa maendeleo ni kwa ajili ya watu na si ya askofu na kufafanua kuwa askofu ni mtumishi wa watu ambaye yupo kama daraja la kuwasaidia.

“Kuwasaidia wananchi kupata maendeleo na si kwa ajili ya maisha yake bora,” amesema.

Mke wa Askofu na mlezi wa umoja wa wanawake wa kanisa hilo, Nora Kutta amesema moja ya mambo wanayofanya ni kuhakikisha wanawake wanakuwa na uwezo wa kujikwamua kiuchumi.

“Kupitia umoja huu tunahakikisha si tu wanasali bali pia wananufaika kiuchumi kwa ajili ya famikia zao,” amesema Norah.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Muslims in Pemba conduct special prayer against ZAA decision
Popular
Investment News Editor

Muslims in Pemba conduct special prayer against ZAA decision

ZANZIBAR: More than 200 Muslims in Vitongoji Village, South Pemba Region over the weekend conducted a special prayer to condemn the Zanzibar Airports Authority (ZAA) move to appoint DNATA as the sole ground handler in Terminal III of the International Airport of Zanzibar. Abeid Amani Karume.Continue Reading