Kabendera atangaza kukata rufaa dhidi ya Vodacom

Kabendera atangaza kukata rufaa dhidi ya Vodacom

Kabendera atangaza kukata rufaa dhidi ya Vodacom

Dar es Salaam. Mwanahabari, Erick Kabendera ametangaza uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya pingamizi lililozuia kuendelea kwa kesi yake anayokabiliana na Kampuni ya mtandao wa simu ya Vodacom Tanzania Ltd.

Kabendera aliifungua kesi hiyo, Julai 2024, akiituhumu kampuni hiyo kuhusika na utoaji wa taarifa za mahali alipo hadi kukamatwa kwake Julai, 2019 nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam.

Baada ya kufungua kesi hiyo namba (12799/2024), iliwekewa pingamizi lililosababisha Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuifuta.

Kabendera alitangaza uamuzi wa kukata rufaa jana Jumanne, Oktoba 1, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, akidokeza anafanya hivyo baada ya kushauriana na mawakili wake.

Alisema anatarajia kukata rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa dhidi za pingamizi lililowekwa kwa kuwa wanaamini kesi hiyo ina mashiko na inastahili kusikilizwa ili wawasilishe ushahidi.

“Kutokana na ushahidi tulioukusanya baada ya miaka mitatu ya uchunguzi, tumeona ushahidi ni mkubwa kiasi kwamba unatosha kuishitaki Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu nchini Afrika ya Kusini na Uingereza,” alisema.

Sambamba na uamuzi huo, Kabendera alisema wanasheria wake kutoka Uingereza na Afrika ya Kusini wanakamilisha utaratibu wa kufungua kesi dhidi ya Vodacom Group South Africa na Vodafone Group PLC yenye makao yake makuu nchini Uingereza haraka iwezekanavyo.

Kabendera anaibuka kutangaza uamuzi huo takribani siku 20 zimepita tangu Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam kuifuta kesi yake aliyokuwa ameifungulia kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Public Limited.

Uamuzi huo wa kuifuata kesi hiyo utolewa Jumanne, Septemba 10, 2024 na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Livin Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo, kufuatia pingamizi la awali lililowekwa na Vodacom.

Katika kesi hiyo ya madai namba 12799/2024, Kabendera aliyewakilishwa na Wakili Peter Madeleka alikuwa anaituhumu Vodacom kufanikisha kukamatwa kwake na namna hiyo anayoiita kutekwa na hatimaye kufunguliwa kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Alikuwa anadai kutokana na tukio hilo amepata madhara mbalimbali yakiwamo ya kiuchumi na yasiyo ya kiuchumi, ya kijamii, maumivu ya kiakili na kimaono, ya kutokufurahia maisha, ya maendeleo binafsi na hadhi yake katika jamii na kutokuaminiwa kitaaluma.

Hivyo, alikuwa anaitaka kampuni hiyo imlipe Dola 10 milioni za Marekani (takribani Sh28 bilioni) kama fidia ya hasara halisi na riba kwa kiwango cha Mahakama (asilimia) kuanzia tarehe ya hukumu mpaka kumaliza malipo yote.

Pia, alikuwa anaiomba Mahakama iamuru Vodacom imlipe fidia ya hasara ya jumla kadri Mahakama itakavyotathmini, gharama za kesi na nafuu nyingine kadri mahakama itakavyona inafaa.

Hata hivyo, Vodacom kupitia wakili wake Gaspar Nyika, Julai 9, 2024 kufuatia wito wa Mahakama uliyoitaka kufika mahakamani na kuwasilisha utetezi wake wa maandishi, iliwasilisha mahakamani maelezo yake ya utetezi wa maandishi.

Katika maelezo hayo ya utetezi ambayo Mwananchi iliyaona nakala yake, kampuni hiyo ilikana tuhuma zote zilizoelekezwa kwake na mwanahabari huyo kuhusu ushiriki wake kufanikisha hicho alichokiita kutekwa kwake na ikamtaka mwanahabari huyo kuthibitisha tuhuma hizo.

Sambamba na maelezo hayo ya utetezi pia kampuni hiyo iliibua pingamizi la awali dhidi ya kesi hiyo ikiiomba Mahakama isiisikilize.

Katika pingamizi lake, kampuni hiyo iliiomba Mahakama hiyo iitupilie mbali kesi hiyo bila kuisikiliza ikidai haina mamlaka ya kuisikiliza kwa madai imefunguliwa nje ya muda uliowekwa kisheria.

Katika uamuzi huo, Jaji Maghimbi amekubaliana na hoja ya pingamizi la Vodacom kuwa kesi hiyo iko mahakamani isivyo halali kwa kuwa imefunguliwa nje ya muda uliowekwa katika sheria.

Jaji Maghimbi amesema sheria inaelekeza kesi za aina hiyo zinapaswa kufunguliwa mahakamani ndani ya muda wa miaka mitatu tangu kutokea kwa jambo linalolalamikiwa, lakini Kabendera alifungua kesi hiyo baada ya muda huo kupitia.

Alivyotiwa mbaroni

Kabendera alitiwa mbaroni na askari polisi nyumbani kwake, Mbweni jijini Dar es Salaam Julai 29, 2019 na kushikiliwa kwa siku kadhaa, kisha akafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi hiyo ilimalizika kwa utaratibu wa majadiliano na makubaliano ya kukiri makosa baina yake na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) unaojulikana kisheria kama plea bargaining.

Aliachiliwa huru Februari 24, 2020 baada ya kulipa fidia ya hasara aliyodaiwa kusababisha kwa kukwepa kodi zaidi ya Sh173 milioni na faini aliyoamuriwa na Mahakama baada ya kumtia hatiani kwa kukiri makosa yake kulingana na majadiliano na makubaliano hayo na DPP.

Mwaka 2024, katikati, ikiwa ni miaka mitano baada ya kukamatwa na miaka minne baada ya kesi yake hiyo ya uhujumu uchumi kumalizika, ndipo Kabendera akafungau kesi hiyo ya madai ya fidia dhidi ya Vodacom.

Simulizi ya kutekwa, msingi wa madai

Kwa mujibu wa hati ya madai katika kesi hiyo Kabendera ameeleza matukio yaliyojiri katika simu yake kabla ya tukio la kukamatwa kwake, kuwa ilianza kupoteza mawasiliano na kumfanya ashindwe kupata huduma ya mawasiliano.

Pia, Kabendera ameelezea juhudi alizofanya kujua chanzo cha hali hiyo kwa kufanya mawasiliano na mwakilishi wa huduma kwa wateja na hata kutembelea ofisi za kampuni hiyo lakini hakupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, hali hiyo ilianza Julai 27, 2019, saa 9:00 alasiri alipoiwasha simu yake ambayo alikuwa ameizima tangu jana yake usiku na kwamba ndipo alipobaini kuwa haikuwa na mtandao.

Hivyo, aliazima simu nyingine akampigia mtoa huduma kwa mteja kujua mazingira yaliyosababisha kumkatia huduma katika simu yake bila kumjulisha kwanza.

Mwakilishi wa huduma kwa wateja wa Vodacom alimweleza kuwa namba yake ya simu ya Vodacom (+255767456796) ilikuwa na changamoto za kiufundi ambayo ilimhitaji kutoa taarifa katika kituo cha huduma kwa wateja cha karibu kilichopo Tegeta.

Kabendera alimtaka mwakilishi huyo kuelezea tatizo ni nini kabla ya kwenda huko kituoni, lakini mwakilishi huyo alikataa akidai ni suala nyeti ambalo linamtaka aende binafsi kituoni hapo.

“Hata hivyo (Kabendera alisita kwenda huko kituo cha huduma kwa wateja) kwa kuwa kulikuwa kina matukio kadhaa ya watu kutekwa ama kutiwa mbaroni walipokuwa wakitembelea kituo cha huduma kwa wateja tangu mwaka 2016,” inasomeka sehemu nyingine ya hati hiyo ya hiyo na kuongeza:

Inaendelea kueleza Jumatatu, Julai 29, 2019 saa 4:00 asubuhi Kabendera alipiga tena simu ya huduma kwa wateja akimlalamikia kuwa alikuwa akihitaji kutoa pesa kwenye simu yake hiyo kwa ajili ya kumnunulia dawa mama yake aliyekuwa mgonjwa.

Mwakilishi wa Vodacom aliyemhudumia alimweleza kuwa asubiri kidogo ili amuulize meneja wake na alirejea dakika chache baadaye na kumweleza kuwa kesi yake ilikuwa nyeti na kwamba ilikuwa juu ya uwezo wao kuitatua.

Badala yake walimshauri atembelee ofisi zao zilizoko Mliman City asubuhi hiyo.

Hata hivyo saa 9:00 alasiri siku hiyohiyo ya Julai 29, ghafla tu simu yake ilianza kufanya kazi, kisha alipoigiwa simu na mwakilishi wa Vodacom ambaye alimtaka (Kabendera) amwelezee tatizo lake na baada ya Kabendera kumuelezea kwa takribani dakika tatu, alikata simu akiahidi kumpigia baadaye kidogo.

Baada ya takribani dakika tatu Kabendera alipokea simu iliyopigwa kutoka huduma kwa wateja Vodacom ambayo aliipokea akabaini kuwa ilikuwa ni sauti ya mwanamume, ambaye alimtaka Kabendera aeleze mahali alikokuwa na kwamba simu hiyo ilikuwa ikihanikiza na kukwaruza kama vile ilikuwa inarekodiwa.

“Kabla ya simu hiyo kukatwa mteja wetu alimsikia huyo aliyempigia simu hiyo akinong’ona kuwa alikuwa nyumbani kwake na kuongeza kuwa sogea karibu na nyumba yake,” inasomeka sehemu nyingine ya hati hiyo ya madai.

Kwa mujibu wa hati hiyo, maelezo hayo yalimstua Kabendera, akakimbia sehemu ya juu ya nyumba yake ambako aliweza kuona magari kadhaa ambayo hakuyafahamu, karibu ya nyumba yake.

Kisha lilitokea gari lingine aina ya Toyota Alphard lililoegeshwa mbele ya magari hayo upande wa kulia mwa nyumba yake, halafu wakashuka watu wanne ambao walijitambulisha kuwa maofisa wa polisi lakini walikataa kutoa utambulisho. Walimpiga pingu kumshikilia kizuizini kwa siku mbili.

Hati hiyo inaendelea kueleza wakati wa mahojiano, maofisa wa polisi walifika katika chumba cha mahojiano wakiwa na karatasi zilizochapishwa kutoka katika kompyuta za akaunti za pesa ya simu na za namba simu alizokuwa amezipiga kwa mwaka mzima.

Hivyo, walimhoji lengo la kila muamala alioufanya kwa mwaka mzima nyuma yake na pia walimhoji uhusiano wake na watu aliokuwa amewasiliana nao miaka kadhaa.

Kabendera analalamika polisi na Serikali walitoa taarifa kadhaa zenye mgogoro kwa umma kuhusiana na ‘kutekwa’ kwake na kwamba walimtuhumu kwa kutokuwa raia na kumkashfu Rais (wa wakati huo) John Magufuli.

“Hatimaye alishtakiwa mahakamani kwa makosa ya utakatishaji fedha, uhujumu uchumi na ukwepaji kodi na matokeo yake walimuweka chini ya ulinzi mkali katika mahabusu ya Gereza la Segerea,” inasomeka hati hiyo ya madai.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Top News
Investment News Editor

ZSSF money not for projects, says Ali Karume

Unguja. Veteran politician and diplomat Ali Karume has called on authorities of the Zanzibar Revolutionary Government (SMZ) to refrain from using the Zanzibar Social Security Fund money for establishing commercial projects.Continue Reading

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms
Tanzania Foreign Investment News
Chief Editor

Tanzania: Samia Hands Over NBC’s 354m/ – Crop Insurance Compensation to Farmers Affected By Hailstorms

President Samia Suluhu Hassan, has handed over a cheque of 354m/- from the National Bank of Commerce (NBC) as compensation to tobacco farmers, who were affected by hailstorms during the previous farming season in various regions across the country.

Handing over the cheque in Dodoma, the compensation is part of the crop insurance service provided by NBC in collaboration with the National Insurance Corporation (NIC).

Furthermore, President Samia has also handed over health insurance coverage to members of the Lindi Mwambao Cooperative Union based in Lindi Region, through the Farmers’ Health Insurance service provided by the bank in partnership with Assurance Insurance Company.

While visiting the bank’s pavilion at the Nanenane Agricultural Exhibition and being received and briefed by the bank’s Managing Director, Mr. Theobald Sabi, she said: “This crop insurance is one of the crucial solutions in ensuring farmers have a reliable income, without fear of challenges such as natural disasters, including hailstorms.

“I call upon all farmers in the country to make the best use of this important opportunity by accessing these kinds of insurance services. I also highly commend NBC and all the stakeholders participating in this programme.”

Elaborating further on the crop insurance service, the Minister of Agriculture, Hussein Bashe, stated that it will help to recover the loss farmers incurred, especially in various calamities beyond their control.

Citing them as floods, fires, and hailstorms, which have significantly affected the well-being of farmers and caused some to be reluctant to invest in the crucial sector, Mr Bashe added: “However, our President, this step by NBC is just the beginning, as this is the second year since they started offering this service, and the results are already visible.

“As the government, we promise to continue supporting the wider implementation of this service, with the goal of ensuring that this crop insurance service reaches more farmers.”

ALSO READ: NBC participates in TFF 2023/24 awards, promises to enhance competition

On his part, Mr Sabi said that the farmers who benefited from the compensations are from 23 primary cooperative unions in the regions of Shinyanga, Geita, Tabora, Mbeya, Katavi, and Kigoma.

He added: “In addition to these insurance services, as a bank, through this exhibition, we have continued with our programme of providing financial education and various banking opportunities to farmers, alongside offering them various loans, including loans for agricultural equipment, particularly tractors, to eligible farmers.:

At the NBC booth, President Samia also had the opportunity to be briefed on the various services offered by the bank to the farmers namely crop insurance and health insurance services.

There, the President had the chance to speak with some of the beneficiaries of the services, including the Vice-Chairman of the Lindi Mwambao Primary Cooperative Union, Mr. Hassan Mnumbe, whose union has been provided with a health insurance card from the bank.

Source: allafrica.com

Continue Reading