JWTZ kutoa matibabu bure kwa siku tano

JWTZ kutoa matibabu bure kwa siku tano

Dar es Salaam. Katika kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwake, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), litatoa huduma za upimaji na matibabu ya afya bila malipo kwa siku tano kuanzia kesho Agosti 26, mwaka huu.

Huduma hizo kwa mujibu wa jeshi hilo, zitatolewa bure hadi Agosti 30, mwaka huu na Septemba Mosi, zitatolewa huduma za matibabu ya dharura.

Hayo yameelezwa katika taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa  leo, Agosti 25, 2024 na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ Makao Makuu, Kanali Gaudentius Ilonda.

Amesema kilele cha maadhimisho hayo ni Septemba Mosi, mwaka huu siku ambayo huduma za matibabu ya dharura zitatolewa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Huduma za jumla zitakazotolewa katika siku hizo, amesema ni ushauri na upimaji wa magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa yakiwemo Malaria, saratani ya tezi dume kwa njia ya damu, magonjwa ya kinywa na meno na saratani ya matiti na shingo ya uzazi.

Huduma hizo kwa mujibu wa Kanali Ilonda, zitatolewa katika Uwanja wa Zakhem Mbagala, Uwanja wa Bububu Unguja, Uwanja wa Magereza Arusha, Uwanja wa Tarafani Mbeya, Uwanja wa Furahisha Mwanza, Uwanja wa Chipukizi Tabora na Uwanja wa Shule ya Sekondari Morogoro mkoani Morogoro.

Maeneo mengine, amesema ni Uwanja wa Shule ya Msingi Matarawe Ruvuma, Uwanja wa Gombani Pemba, Uwanja wa Nyerere Square- Dodoma na Uwanja wa Stendi ya zamani Nachingwea Lindi.

Hata hivyo, amesema wanajeshi katika kambi zote watachangia damu salama, shughuli itakayoendeshwa na hospitali zote za jeshi kwa kushirikiana na Kitengo cha Taifa cha Damu Salama.

“Wananchi wote wanakaribishwa ili kunufaika na huduma za tiba zitakazotolewa pamoja na kujitolea kuchangia damu salama,” amesema.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Karume faults lease of Zanzibar Islets
Tanzania Foreign Investment News
Investment News Editor

Karume faults lease of Zanzibar Islets

Diplomat Ali Karume has faulted the decision by the revolutionary government of Zanzibar to lease the islets that surround the islands of Unguja and Pemba to private developers saying it was absolutely not in Zanzibar’s national interests.Continue Reading

Popular
Chief Editor

Insecurity prompts Zanzibar to review its lucrative island leasing

The Tanzanian central government is planning to boost its security presence in the Zanzibar archipelago. A commission tasked with auditing the country’s security forces was appointed in July by President Samia Suluhu Hassan. It says it is concerned about the situation in the country’s Indian Ocean islands that are under the control of the semi-autonomous Zanzibar local government.Continue Reading