Jinsi vituo vya umahiri Tanzania vitakavyochochea mapinduzi ya teknolojia

Jinsi vituo vya umahiri Tanzania vitakavyochochea mapinduzi ya teknolojia

Dar es Salaam. Ujenzi wa vituo vya umahiri nchini Tanzania vinatajwa kuleta mapinduzi katika utoaji wa elimu na kuzalisha wataalamu wa kutosha katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), usafirishaji, utengenezaji wa bidhaa za ngozi pamoja na nishati jadidifu.

Pia, katika kuwapa ujuzi vijana utakaowawezesha kuendana na matakwa ya soko la ajira lililopo sasa pamoja na namna ya kutumia fursa zilizopo katika mazingira yao kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.

Vituo hivyo vya umahiri vimejengwa kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi kwa Maendeleo na Uingiliano wa Kikanda katika Afrika Mashariki (EASTRIP) uliofadhiliwa na Benki ya Dunia na kuanza kutekelezwa tangu mwaka 2019 na kugharimu zaidi ya Sh172 bilioni.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu, Septemba 9, 2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Elimu Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Fredrick Salukeke katika kikao kazi kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa mradi huo.

Salukeke amesema moja ya lengo la mradi na vituo hivyo vya umahiri ni kuongeza upatikanaji na kuboresha ubora wa programu katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi vya Kikanda (TVET).

Amesema uboreshaji huo unafanyika kwa kufanya mambo mbalimbali, ikiwemo kusomesha wakufunzi, kuwawezesha kupata uzoefu kutoka katika taasisi nyingine ndani na nje ya nchi, kuboresha mitaala na kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo na viwanda ili wanafunzi watakaomaliza wapate ujuzi unaotakiwa viwandani.

“Moja kati ya changamoto tulioigundua ni pamoja na kutokuwa na muunganiko wa moja kwa moja kati ya wakufunzi na waajiri, hivyo kupitia mradi huu tunataka kuimarisha ushirikiano huo wenye lengo la kuboresha elimu ya ujuzi wanaopatiwa wanafunzi,” amesema.

Amesema kwa sasa mradi huo hapa nchini umewezesha kujengwa kwa vituo vya umahiri vinne ambavyo ni kituo cha umahiri cha mafunzo ya Tehama (RAFIC) katika Taasisi ya Teknolojia kampasi ya Dar es Salaam (DIT).

Pia kituo cha umahiri cha mafunzo ya taaluma za anga na operesheni za usafirishaji (CoEATO) katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Kituo cha mafunzo na utafiti wa nishati jadidifu (Kikuletwa) katika chuo cha ufundi Arusha pamoja na kile  cha Uchakataji Ngozi (CELPAT) kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam kampasi ya Mwanza.

“Pamoja na nchi ya Tanzania, mradi huo pia unatekelezwa katika nchi ya Kenya pamoja na Ethiopia,” amesema.

Kwa upande wake, mkuu wa kituo cha umahiri cha mafunzo ya taaluma za anga na operesheni za usafirishaji (CoEATO) katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk Chacha Ryoba amesema kupitia mradi huo imewezesha kupatikana kwa vifaa na mitambo mipya ya kisasa ya kufundishia na kujifunzia, ili kitoe mafunzo yanayoendana na teknolojia ya kisasa na kuzalisha wataalamu watakaoweza kushindani katika soko la ajira.

Pia amesema kuanzishwa kwa vituo hivyo ni kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuwa kila kimoja kitakuwa na mchango chanya katika kutatua changamoto za jamii na pia kuchochea maendeleo ya taifa

Naye mkaguzi wa mradi kutoka kituo cha umahiri cha uchakataji ngozi (CELPAT) kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza, amesema pamoja na kusaidia kuboresha utolewaji wa elimu ya ufundi nchini, pia itasaidia katika kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa.

Hiyo itawezekana kutokana na uboreshwaji wa miundombinu, ikiwemo ujenzi wa madarasa pamoja na hosteli kwa ajili ya malazi kwa wanafunzi.

“Hilo litasaidia kuongezea uwezo vyuo ambayo vina vituo hivyo vya umahiri kuongeza uwezo wake wa kupokea wanafunzi, jambo ambalo litasaidia katika kuchochea kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika vyuo hivyo,” amesema.

Ametolea mfano katika kampasi hiyo mradi ukikamilika wanatarajia kupokea wanafunzi takribani 2500, 2100 wakiwa wa kozi ndefu na 400 kozi za muda mfupi.

Source: mwananchi.co.tz

Original Media Source

Share this news

Facebook
Twitter
LinkedIn
WhatsApp

This Year's Most Read News Stories

Popular
Swahili News Editor

MGAO WA MAJI WAWATESA WAZANZIBARI

Wananchi wengi hasa katika maeneo ya Mjini Unguja, wanalalamikia ukosefu wa maji safi na salama huku Mamlaka ya Maji Zanzibar ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ujuzi na wataalam katika masuala ya uandisi wa Maji na fani nyengine.Continue Reading

Popular
Chief Editor

Zanzibar airport operators decry job losses over Dubai deal

Tanzania air operators say over 600 workers are set to lose their jobs after the semi-autonomous government of Zanzibar awarded a Dubai-based company exclusive rights to handle ground services at a refurbished airport.

The Tanzania Air Operators Association (Taoa) said in a statement that the contract awarded to Dnata, which is registered at the London Stock Exchange, was in breach of the law banning any company from having exclusive rights to ground-handling services at major airports.Continue Reading